Kitwanga sikio la kufa

Mambo mapya yameibuka kuhusiana na kuvuliwa uwaziri kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, aliyevuliwa wadhifa huo Mei 20, 2016 baada ya kuingia bungeni akiwa amelewa. Vyanzo vya habari vya uhakika vimeiambia JAMHURI kuwa Kitwanga alikunywa pombe akiwa na wageni wake (wakiwamo madiwani), waliotoka jimboni kwake na kuachana nao…

Read More

Mabilioni yatafunwa NIP

Mradi wa uendelezaji viwanja viwili vilivyoko Mtaa wa Ohio (Plot 775/39 na 776/39) vya Shirika la Tija la Taifa (NIP), unaonekana kuwa ni ‘hewa’ kutokana na kutokamilishwa kwa mujibu wa makubaliano ya wabia wawili waliojitokeza kuendeleza viwanja hivyo kwa nyakati tofauti. Ujenzi wa mradi huo ulilenga kujenga ghorofa 35 ambazo ujenzi wake ungegharimu kiasi cha…

Read More

Barua ya elimu kwa Rais Magufuli

Mheshimiwa Rais, nianze kwa kukupa pole kwa majukumu mazito uliyonayo ya kulijenga taifa letu. Wananchi wanyonge wamekuwa na imani kubwa na wewe kutokana na juhudi zako ambazo umeishazionyesha katika kuwaletea maendeleo tangu uingie madarakani. Tunakutia moyo na kukuombea uendelee na juhudi hizo na tunaahidi kuwa nyuma yako katika kulijenga taifa letu. Mheshimiwa Rais, nina mambo…

Read More

Rais Magufuli epuka ushauri huu!

Wiki iliyopita nilikuwa katika kipindi cha ‘Malumbano ya Hoja’ kinachorushwa ‘live’ na ITV. Mjadala kadiri ulivyoendelea nilipata shida kidogo. Niliwaona baadhi ya wachangiaji wakizungumza lugha ya hatari, ambayo ninaisoma katika baadhi ya magazeti. Wanasema Rais John Magufuli anahujumiwa.  Sitanii, neno hili linaweza kuonekana dogo, lakini tunakoelekea lisipokemewa linaweza kudumaza maendeleo ya nchi. Kwa sasa nchi…

Read More

CCM chama tawala kilichoshindwa kutawala

Majuzi, aliyekuwa Spika wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, alisema kwamba ushindi wa Rais Dk John Magufuli katika Uchaguzi Mkuu 2015 umenusuru Watanzania na machafuko. Amesema kwamba machafuko yangeweza kutokea kutokana na tofauti kubwa ya kipato kati ya matajiri na maskini. “Kuna watu walikuwa haifahamiki wanafanya kazi gani lakini mamilionea.”…

Read More

Kiwanda cha Saruji chatesa wakazi Dar

Wakazi wa kata za Boko na Bunju, Dar es Salaam wamekilalamikia Kiwanda cha Saruji cha Twiga Cement (Wazo) kwa uharibifu wa mazingira ambao umeathiri makazi na uharibifu wa mali zao. Wakazi hao wameieleza JAMHURI kwamba maporomoko ya maji kutoka katika mabwawa ya kiwanda hicho yaliyoko katika eneo linalochimbwa miamba kwa ajili ya uzalishaji wa saruji,…

Read More