Monthly Archives: November 2017

Zaidi ya Million 20 Zapatikana Kusaidia Watoto Wenye Ulemavu

Zaidi ya milioni 20 zimetolewa na wananchi pamoja na Taasisi mbalimbali hapa  nchini ikiwa ni mchango wa kusaidia matibabu na kununua vifaa tiba kwa ajili ya  watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi. Ikiwa Jana ni Jumanne ya kutoa (GIVING TUESDAY) kote duniani na Taasisi ya Foundation for Civil Society iliadhimisha kwa kuwasaidia watoto hawa kwa kuwapatia vitu hivyo,huku kauli ...

Read More »

LHRC Yabaini Mapungufu Kibao Uchaguzi wa Madiwani

  MKURUGENZI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga, amesema kuwa kituo hicho kimefuatilia kwa ukaribu uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 ulifanyika Novemba 26 mwaka huu, katika halmashauri 36 kwenye mikoa 19 nchini. Katika uchaguzi huo tume ya haki za binadamu imebaini matukio mbalimbali ya uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu, vikiwemo vitendo vya ...

Read More »

Katibu wa CHADEMA Manyara Arejea CCM

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Manyara, Meshack Turento ametangaza kujivua wadhifa huo na kujiunga na Chama cha Mapinduzi akidai chama hicho (CHADEMA) imewatelekeza. Akizungumza jijini Arusha Turento alidai kuwa, kabla ya kujiunga na CHADEMA alikuwa mwanachama wa CCM, lakini baadae aliona chama hicho kimepoteza mwelekeo na kujiunga na CHADEMA, ila sasa ameamua ...

Read More »

Samia Suluhu Amtembelea Tundu Lissu Nairobi Hospital

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi. Samia amtembelea Lissu baada ya kumalizika kwa hafla ya kumwapisha Rais Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Mhe. Samia Suluhu Hassan alimwakilisha Rais wa Jamhuri ...

Read More »

MAJALIWA: Tutawashughulikia Wote Wanaotumia Vibaya Fedha Za Ukimwi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitawavumilia watu wote wanaotumia vibaya fedha za umma ambazo zinapaswa kuleta maendeleo kwa wananchi, zikiwemo na za Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi. Amesema mfuko huo unalenga kufanikisha ukusanyaji wa fedha za kutosha amabazo ni muhimu kwa Taifa wakati huu tunapoazimia kumaliza ukimwi ifikapo mwaka 2030..   Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo leo (Jumanne, Novemba ...

Read More »

Waziri Mkuu Apokea Vifaa Vya Mashindano Ya Majimbo

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 50 kwa ajili ya kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu kwa majimbo ya mkoa wa Dar es Salaam.   Vifaa hivyo vimetolewa na Muwakilishi wa Jimbo la Uzini, Mohammed Raza na Muwakilishi wa kuteuliwa Bw.Ahmada Yahya Abdulwakili, ambapo mara baada ya kupokea vifaa hivyo alivikabidhi kwa ...

Read More »

Wananchi Wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki Kuingia Kenya Kwa Kitambulisho Cha Taifa Tu

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza neema kwa wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuruhusu kuingia nchini humo kwa kutumia kitambulisho cha taifa tu na kupewa haki zingine kama raia wa Kenya. Taarifa hiyo imetolewa leo na Rais Uhuru Kenyatta alipokuwa akilihutubia taifa mara baada ya kuapishwa , na kusema kwamba raia wa Afrika Mashariki watahudumiwa kama raia wa Kenya na ...

Read More »

Samia Suluhu Amwakilisha Rais Magufuli Kenya

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta zitakazofanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Kulia ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons