Daily Archives: December 6, 2017

Kilimanjaro Stars Uso kwa uso Na Zanzibar Heroes Michuano ya CECAFA

Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kesho Alhamis Desemba 7, 2017 inatupa karata yake ya pili kwenye michuano ya CECAFA dhidi ya Zanzibar Heroes ya Zanzibar kwenye mchezo wa kwanza utakaoanza saa 8.00 mchana kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos. Mchezo huo unatarajiwa kushuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. Pindi Hazara Chana ambaye anaiwakilisha nchi katika Kenya. ...

Read More »

Vladimir Putin Atangaza Nia ya kuwania tena urais 2018

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza kuwa atawania kiti cha urais kwa mara nyingine tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao wa 2018. Alitangaza hayo alipokuwa akiwahutubia wafanyikazi huko Nizhny Nov-gorod. Rais Putin ambaye ana umri wa miaka 65 alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Rais wa Urusi mwaka 2000. Baada ya kuhudumu kwa mihula miwili alichaguliwa kama Waziri mkuu ...

Read More »

Rais Trump Sasa Aitambua Yerusalem ni Mji Mkuu wa Israel

Akiongea katika Ikulu ya Marekani, Rais Trump ameutambua mji wa Yerusalem kama mji mkuu wa Israel, maamuzi ya kihistoria yanayopindua sera za miaka mingi za Marekani. Rais Donald Trump ametangaza kuwa Ubalozi wa Marekani utahamishwa kutoka katika eneo la sasa la Tel Aviv kwenda Yerusalem. Amesema kuwa uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za kuleta amani katika ...

Read More »

Haya ndiyo Makazi mapya Ya Mama Samia Suluhu Mjini Dodoma

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua matengenezo ya makazi ya muda yanayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan pindi atakapohamia Dodoma. Waziri Mkuu amefanya ukaguzi huo katika eneo la Kilimani, mjini Dodoma ambako yalikuwa makazi ya Mkuu wa Mkoa huo. Akitoa taarifa ya ujenzi huo, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Wenye Ulemavu na ...

Read More »

Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi 6

Rais Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi 6 za taasisi za Serikali baada ya wenyeviti waliokuwepo kumaliza muda wao. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 06 Desemba, 2017 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kwanza Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Monica Ngenzi Mbega kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko kuanzia tarehe 30 Novemba, 2017. Pili, Mhe. ...

Read More »

TANZIA: Mkuu wa Mkoa Joel Bendera Afariki Dunia

Mkuu wa Mkoa wa Manyara mstaafu, Joel Bendera amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo Jumatano Desemba 6,2017 . Msemaji wa Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema, “Ni kweli Joel Bendera amefariki. Aliletwa leo na gari la wagonjwa saa 6:30 mchana na ilipofika saa 10:24 jioni alifariki.” Aligaesha amesema Bendera alipokewa hospitalini hapo akitokea Bagamoyo mkoani Pwani. Kuhusu chanzo cha kifo ...

Read More »

Madabida Atiwa Tena Mbaroni

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano wamekamatwa tena leo baada ya muda mfupi kufutiwa mashtaka ya kusambaza dawa feki za kufubaza makali ya ukimwi (ARV) na kujipatia Sh milioni 148 kwa njia ya udanganyifu. Madabida na wenzake wamefutiwa mashtaka hayo katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, na baada ya ...

Read More »

Hivi Ndivyo Rais Mstaafu Aly Hassan Mwinyi alivyomtembelea Tundu Lissu Hospitalini Nchini Kenya

Rais mstaafu Aly Hassan Mwinyi amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya. Rais Mwinyi akiambatana na mkewe na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Kenya, wamemtembelea Lissu hospitalini hapo alipolazwa tangu Septemba 7  anakotibiwa baada ya kuuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma. Rais Mwinyi anakuwa ...

Read More »

Mambosasa: Hatuna Mpango wa Kuendelea na Kesi ya Dk Shika

Lazaro Mambosasa ambaye niKamanda wa Polisi Kanda Maalumu yaDar es Salaam, amesema kesi ya Dk Louis Shika hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba tatu za mfanyabiashara maarufu Said Lugumi alizoahidi kuzinunua zote zipo. Novemba 9, 2017 kampuni ya udalali ya Yono kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliendesha mnada wa nyumba mbili za Lugumi zilizoko Mbweni JKT na moja ...

Read More »

MAAGIZO 5 YA WAZIRI MHAGAMA KWA PROGRAMU YA MIVARF KUOGEZA THAMANI YA BIASHARA ZA MIFUGO WILAYANI LONGIDO

Waziri wa Nchi Ofisi  ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira ,Kazi,  Vijana na Watu wenye Ulemavu ) Mhe.Jenista Mhagama ameielekeza Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), kuongeza Thamani Biashara za Mifugo wilayani Longido kwa kutatua  kero zote  za wafanyabiashara wa mifugo wilayani humo. Mhagama ametoa maagizo hayo baada ya kukagua  Soko ...

Read More »

Waziri Mkuu Akagua Makazi ya Makamu wa Rais

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua matengenezo ya makazi ya muda yanayotarajiwa kutumiwa Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan pindi atakapohamia Dodoma.   Waziri Mkuu amefanya ukaguzi huo leo mchana (Jumatano, Desemba 6, 2017) katika eneo la Kilimani, mjini Dodoma ambako yalikuwa makazi ya Mkuu wa Mkoa huo. Akitoa taarifa ya ujenzi huo, Waziri wa Nchi (OWM) anayeshughulikia Sera, Uratibu, ...

Read More »

Marekani Yaionyeshea Ubabe wa Kivita Korea Kaskazini

Jeshi la Marekani limerusha ndege yake aina ya B-1B bomber katika anga ya Korea Kusini kama sehemu ya mazoezi ya pamoja ya angani katika hatua inayoonekana kama onyo kwa Korea Kaskazini. Mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika wiki moja baada ya Korea Kaskazini kurusha kombora ililodai kuwa ni la masafa marefu ambalo linaloweza kushambulia nchini Marekani. Marekani awali imerusha ndege hizo ...

Read More »

Mbunge wa Chadema Azungumzia Hali ya Kisiasa kwa Upande Wake

Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Said Kubenea amewataka wananchi wa jimbo lake na nchi nzima kwa ujumla kupuuzia taarifa zinazosambazwa dhidi yake kuhusu yeye kutaka kukihama chama chake. Kebenea amesema kuwa ataendelea kuwa Mbunge wa jimbo la Ubungo na hana mpango wowote wa kuondoka CHADEMA kuhamia CCM. Kubenea ameyasema hayo baada ...

Read More »

Chadema Kukutana, Kuzungumza Yanayoendelea Nchini

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana katika kikao cha dharura, kwa mujibu wa Katiba ya Chama, siku ya Jumatano, Desemba 6, mwaka huu, jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho cha siku moja, pamoja na masuala mengine, Kamati Kuu ya Chama itapokea na kujadili agenda ya Mwenendo wa Hali ya Kisiasa nchini, kipekee kuhusu; i.Taarifa na ...

Read More »

Mzanzibar Ashinda Tuzo ya Turner Prize

Profesa Lubaina Himid ni mzaliwa wa Zanzibar ambaye ni mtanzania ametangazwa kuwa mshindi wa ‘Turner Prize 2017’katika tuzo kubwa za Sanaa nchini Uingereza. Majaji wamempa Tuzo kwa maonesho matatu yaliyofanyika Oxford, Bristol na Nottingham ambapo waliisifu kazi yake ambayo inaangazia Afrika duniani kote pamoja na ubunifu wa mtu mweusi jambo ambalo wameliita namna nzuri ya ubunifu. Profesa Himid ambaye ni ...

Read More »

Man United, Yatinga 16 Bora Klabu Bingwa Ulaya

Michezo nane ya kwanza ya hatua ya mwisho ya makundi ya klabu bingwa barani ulaya imechezwa usiku huu na jumla ya timu kumi na mbili tayari zimefuzu kwa hatua ya kumi na sita bora. Katika kundi A Manchester United, wameibuka vinara wa kundi hilo kwa kuwa na alama 15,baada ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya CSKA Moscow, nao Fc Basel ...

Read More »

Urusi Yapigwa Kitanzi Kushiriki Michuano ya Olimpiki 2018

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki, imeifungia nchi ya urusi kushiriki michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi itayofanyika katika jiji la Pyeongchang nchini Korea kusini mwakani. Rais wa IOC Thomas Bach na bodi yake walitangaza adhabu hiyo jana jioni baada ya kukutana katika mji wa Lausanne nchini Switzerland, maamuzi hayo yamefikiwa baada ya uchunguzi wa miezi kumi na saba. Serikali ...

Read More »

Mnyika Anena Kuhusu Barua Inayosambaa Mitandaoni

Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (CHADEMA) amekanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba amejiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara ndani ya CHADEMA Kupitia mitandao ya kijamii imesambazwa barua inayodaiwa ni ya Mnyika ambayo imedai amejiuzulu nafasi yake ili aweze kupata muda wa kutosha kuwatumikia wapiga kura wake. Mnyika masema barua hiyo ni batili na kuwataka wanachama wa CHADEMA ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons