Tujenge Uzalendo Kupitia Uchumi
Wiki iliyopita nchi yetu imesherehekea miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara). Wakati tunapambana kupata uhuru, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyeongoza harakati hizo, alisema nchi yetu ilikuwa inapambana na maadui watatu; ujinga, maradhi na umaskini. Na alisema ili nchi ipate mafanikio inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Ukipima kigezo cha siasa za…