Monthly Archives: January 2018

TCRA yafafanua Mtumizi ya Alama za Vidole Kwenye Usajili wa Laini

“Ndugu mteja katika kuboresha usajili wa laini za simu alama za vidole zitatumika kuanzia Februari 5, 2018. Kwa mawasiliano zaidi tembelea maduka yetu,”  ni ujumbe ambao watumiaji mbalimbali wa mitandao ya simu nchi wametumiwa kuanzia juzi kutoka katika mitandao yao. Kuhusu ujumbe huo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema kuwa imetoa kibali kwa makampuni ya simy nchini upya kadi ...

Read More »

Hawa Hapa Wanafunzi 10 Bora Na Wasichana 10 Bora Kitaifa, Kidato Cha Nne 2017

Baraza la Mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya kidato cha nne iliyofanyika Novemba 2017 ambapo jumla ya watahiniwa 385,767 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2017 wakiwemo wasichana 198,036 (51.34%) na wavulana 187,731 (48.66%).   Kati ya watahiniwa 385,767 waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 323,332 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 62,435. Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watahiniwa wa shule waliofaulu ...

Read More »

MENGI AIPA TWCC JENGO LAKE KUENDELEZA UJASIRIAMALI

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr. Reginald Mengi akifurahi jambo na Mwakilishi wa TRA, Rose Mahendeke (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake nchini TWCC, Bi. Noreen Mawalla (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake nchini (TWCC), Bi. Jaqueline Mneney Maleko (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu kufungua ...

Read More »

Haya Hapa Magazeti ya Leo Januari 31, 2018

Kama upo mbali na meza za magazeti mtaani kwako basi husipitwe na kilichoandikwa kwenye magazeti ya leo Jumatano Januari,31, 2018 nimekuekea hapa

Read More »

Tunahitaji Amani Kwenye Kampeni

NA MICHAEL SARUNGI Katika chaguzi ndogo za udiwani zilizofanyika mwaka jana, kuliripotiwa uwepo wa vurugu kiasi cha kusababisha baadhi ya vyama vya siasa kususia chaguzi zilizofuata katika majimbo ya Songea Mjini na Singida Kaskazini. Taarifa za uwepo wa vurugu katika chaguzi hizo hazikuwa nzuri kwa kila mpenda demokrasia nchini, na kuanza kuashiria mgogoro wa kisiasa huku lawama nyingi zikielekezwa kwa ...

Read More »

MOROCCO YAJITOSA KOMBE LA DUNIA 2026 

NA MTANDAO Morocco imewasilisha rasmi maombi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2026, huku tayari ikiwa imezindua kampeni ya kuandaa michuano hiyo. Ikumbukwe kuwa hiyo haitakuwa mara ya kwanza kwa taifa hilo la Afrika Kaskazini kuomba kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa; kwa mara ya kwanza liliwasilisha maombi yake mwaka 1994, 1998, 2006 na ...

Read More »

JE, ALIYETEULIWA NA MAREHEMU KWENYE WOSIA KUSIMAMIA MIRATHI ANAHITAJI KUTHIBITISHWA NA MAHAKAMA?

Na Bashir Yakub Wako wasimamizi wa mirathi wa aina mbili. Kwanza ni yule ambaye marehemu mwenyewe amemteua kabla ya kufa kwake na akaandika/kusema kwenye wosia kuwa fulani ndiye  atakayesimamia  mirathi  yangu  baada  ya  kuondoka. Pili, ni yule ambaye  hakuteuliwa  na  marehemu mwenyewe bali  ameteuliwa na wanafamilia kwenye kikao  cha  familia. Kwa walio wengi  huyu  ndiye  tunamjua kuwa ni lazima jina lake lipelekwe  mahakamani  kwa  ajili  ya  kuthibitishwa  ili  aweze kuwa  msimamizi  kamili.  Makala itapitia Sheria  ya  Usimamizi  wa Mirathi, Sura ya 352  na kanuni zake. 1.   HAKI NA WAJIBU WA WASIMAMIZI WA MIRATHI Haki  na  wajibu  wa  msimamia  mirathi  aliyeteuliwa  na  marehemu kabla ya kifo na  ambaye  ...

Read More »

SMS 331: STENDI YA TABATA CHAFU

Watu wanaweza kusema hakuna stendi Tabata Kimanga kwani kinachoonekana pale ni dampo la uchafu. Diwani na Serikali ya Mtaa tusaidiane. Fakhii Mohamedy, 0673774241 Serikali isiue demokrasia  Ombi langu kwa Serikali yetu ya Awamu ya Tano ione uwepo wa vyama vya upinzani nchini ni moja ya njia ya kuikosoa serikali pale inapokosea kutekeleza masuala muhimu ya wananchi. Kayai Mdoe, Kiteto, Manyara ...

Read More »

TANROADS: TUMIENI MICHEPUKO KUEPUKA FOLENI TAZARA

DAR ES SALAAM NA CLEMENT MAGEMBE Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) umehimiza matumizi sahihi ya alama zinazoonesha barabara za mchepuko kwa magari yanayopita makutano ya barabara za Nyerere na Mandela, ili kuepuka foleni zinazoweza kuzuilika. Makutano hayo ndipo panapojengwa barabara ya kupita juu maarufu kama Tazara fly over, lengo likiwa ni kupunguza foleni za magari hususani yanayopita kwenye barabara hizo. Kutokana ...

Read More »

UKO WAPI USALAMA VIWANJANI?

NA MICHAEL SARUNGI Mamlaka husika zinapaswa kuhakikisha ubora wa viwanja kabla ya timu kuruhusiwa kutumia viwanja hivyo ili kudhibiti fujo na kuepusha matatizo yanayoweza kutokea kati ya washabiki na wachezaji. Wakizungumza na JAMHURI, baadhi ya wapenzi wa michezo nchini wamesema wachezaji ni wanadamu kama walivyo wengine, wanaoweza kupandwa na hasira na kujikuta wakitenda vitendo visivyotakiwa michezoni. Ernest Bujiku, bondia mstaafu ...

Read More »

YAH: SIMULIZI YA TANZANIA NIIJUAYO

Sijasimulia kiasi cha kutosha juu ya nchi yangu niipendayo, nchi ambayo nimeiishi kwa maisha na matendo, nchi ambayo ninaijua ‘ndani nje’, iwe kiuchumi, siasa, utamaduni, teknolojia, uzalendo na zaidi ya yote kiuongozi. Ni nchi ambayo labda inaweza ikawa ni historia kwa nchi nyingine kama wakiwa waungwana wa kukumbuka fadhila za ujirani mwema. Wapo ambao wanaijua vizuri nchi yangu, na wapo ...

Read More »

MJANE ATIMULIWA KWENYE NYUMBA KWA MABAVU

DAR ES SALAAM NA MICHAEL SARUNGI Mary Njogela (70), mjane anayehifadhiwa kwenye jumba bovu lililoko Mikocheni ‘B’ jijini Dar es Salaam baada ya kuondolewa kwa nguvu na watoto wa kufikia wa marehemu mume wake, anaomba msaada wa Serikali ili arejeshewe mali hiyo.   Amesema nyumba aliyonyang’anywa alikuwa akiishi na mumewe, Said Hamza (marehemu) kwenye kiwanja namba 483, kilichopo kitalu ‘B’ huko ...

Read More »

USITISHAJI MICHANGO MASHULE ‘WAITIKISA’ DODOMA

NA EDITHA MAJURA Dodoma Agizo la Rais John Magufuli kuzuia wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule za msingi na sekondari zinazomilikiwa na Serikali wasitozwe michango, limeibua changamoto katika uendeshaji wa shule hizo mkoani hapa, imebainika. JAMHURI limebaini hayo baada ya kuzungumza na baadhi ya wanafunzi, walimu na wazazi walio walengwa katika utekelezaji wa agizo hilo. Hali iliyopo kwenye shule kadhaa ...

Read More »

JAJI ROBERT KISANGA: NYOTA YA HAKI SAWA ILIYOZIMIKA

Mashaka Mgeta Alikuwa gwiji wa haki za binadamu, mwelekezi wa misingi ya utawala bora, mtetezi wa uhuru wa mihimili ya dola na mpigania haki za watu wanaoonewa; Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Robert Kisanga, amefariki dunia. Januari 23, mwaka huu, mauti yalimkuta Jaji Mstaafu Kisanga akiwa amelazwa kwenye Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Msemaji wa familia ya ...

Read More »

ANGELA MERKEL AANZA KUUNDA SERIKALI

NA MTANDAO Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema anakamilisha utaratibu wa kuangalia namna ya kuunda serikali ya mseto kwa kushirikiana na viongozi wa vyama vya Social Democratic na SPD. Amesema wanatarajia kwenda mbele katika jitihada zao za kuunda serikali na ndiyo maana ana matumaini juu ya majadiliano yanayoendelea, huku akisema  anaamini hilo linaweza kufikiwa kwa wakati. Amesema Wajerumani wanahitaji uwepo wa ...

Read More »

MAFANIKIO YANA SABABU YOYOTE (7)

Na Padre Dkt. Faustin Kamugisha Mtazamo chanya ni sababu ya mafanikio. Mtazamo chanya unakufanya uyaone matatizo kuwa ni baraka katika sura ya balaa. Mtazamo chanya unakufanya kuhesabu siku zako kwa saa za furaha na si kwa saa za karaha. Mwenye mtazamo chanya akijikuta katika maji anaamua kuoga. Washindi wengi wana mtazamo chanya. Kuna aliyesema “Mshindi kila mara ni sehemu ya ...

Read More »

TANZANIA NINAYOITAKA NA TANZANIA NISIYOITAKA

NA ANGALIENI MPENDU Binadamu anapokuwa na tabia ya kuaminika, anapenda haki na anafuata utaratibu mzuri wa kufanya kazi, anajijengea sifa ya uaminifu, uadilifu na nidhamu. Huyu ndiye binadamu ninayemfahamu na ninayemkubali kwa Tanzania niitakayo. Binadamu mwenye upungufu wa sifa hizi, hutambuliwa na kuonekana hayawani na mpenda kufanya mambo ya dhuluma na ufisadi, hiana na choyo, uwongo na utovu wa nidhamu. ...

Read More »

BARABARA YA VUMBI MGODI WA NGAKA INAVYOATHIRI UCHUMI NA MAZINGIRA

Na Albano Midelo WAKAZI wa vijiji vya Kata ya Ruanda vilivyopo barabarani kutoka mgodi wa makaa ya mawe Ngaka Wilaya Mbinga Mkoa wa Ruvuma wanapata athari za kimazingira zinazosababishwa na uchimbaji wa madini hayo. Kwa mujibu wa sensa ya makazi ya mwaka 2012 Vijiji vinavyounda Kata ya Ruanda vina jumla ya wakazi 7374 ambao wanatoka katika vijiji vya Ukombozi, Ntunduwaro, ...

Read More »

BURIANI GWIJI WA MUZIKI WA JAZZ HUGH MASEKELA

Na Moshy Kiyungi Tabora Mwanamuziki mashuhuri wa kimataifa wa Afrika Kusini, Hugh Masekela, amefariki dunia Januari 24, 2018 jijini Johannesburg, Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 78. Chanzo cha kifo chake ni ugonjwa wa tezi dume alioupata miaka kadhaa iliyopita. Bendi yake ilitoa taarifa ikisema, Masekela amekuwa akiuguza ugonjwa huo tangu mwaka 2008. Machi 2016, Masekela alifanyiwa upasuaji wa ...

Read More »

JIBU LA UPENDO NI UPENDO

Mwanaharakati Martin Luther King Jr amewahi kusema, “Nimeamua kujishughulisha na upendo. Chuki ni mzingo mzito sana ambao haubebeki.’’ Katika jamii yetu tunayoishi, tumeshuhudia au tumekutana na tunaendelea kukutana na watu ambao hawana furaha katika maisha yao. Tunakutana na watu wanaojilaumu na kuwalaumu wengine. Tunakutana na watu wanaotamani kujiua. Tunakutana na watu ambao wanahisi jamii imewatenga. Tatizo ni nini? Tuwasaidieje watu ...

Read More »

KUPATA HEDHI INAYODUMU HADI KWA KIPIDI CHA WIKI MOJA KUNAASHIRIA TATIZO LINALOHITAJI UANGALIZI

Ni kawaida kwa mwanamke aliyepevuka kupata hedhi ya kila mwezi katika mzunguko wake, kutokana na mabadiliko ya homoni ambapo mfuko wa uzazi unatengeneza ukuta mpya kwa ajili ya mapokezi ya utungishwaji wa mimba. Kwa kipindi hicho, mwanamke anapitia siku kadhaa za utokwaji wa damu kupitia uke. Idadi ya siku hizi imetofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine, kulingana na mfumo ...

Read More »

SERIKALI YABUNI PROGRAMU YA KUDHIBITI MAISHA YA KUBAHATISHA

  NA CLEMENT MAGEMBE Upungufu wa ujuzi wa shughuli za uzalishaji mali, umetajwa kuwa chanzo cha vijana wengi ‘kuwekeza’ zaidi katika michezo ya kubahatisha ili kujipatia kipato. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Ridhiwani Wema, amesema licha ya vijana wengi kuhitimu masomo kwenye vyuo na taasisi za elimu ya juu, ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons