Daily Archives: February 8, 2018

MPINA APANGUA HOJA ZA WABUNGE KUHUSU NAMNA WIZARA YAKE INAVYOPAMBANA KUTOKOMEZA UVUVI HARAMU NCHINI

 Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina,  Injinia Arcard Mutalemwa (Mwenye shati jeupe), kufanya tathmini ili kujua  uwekezaji uliopo katika Ranchi za Taifa (NARCO) akikabidhi  ripoti ya kazi hiyo jana  kwa Waziri Mpina na viongozi wakuu wa Wizara hiyo. Mhe. (Picha na John Mapepele)  Picha ya pamoja  baina ya Kamati iliyoundwa na Waziri wa  ...

Read More »

MTULIA ATAJA KERO ATAKAYOANZA NAYO AKIWA MBUNGE

MGOMBEA ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Abdallah Mtulia ameendelea kuomba kura huku akiwaambi wananchi yeye hana tofauti na wao. Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni jana jioni katika viwanja vya Vegas,Makumbusho,Kinondoni jijini Dar. Baadhi ya Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamekusanyika kwenye kampeni katika viwanja vya ...

Read More »

Kesi ya Jamal Malinzi Yapigwa Tena Karenda

Kesi inayomkabili aliyewahi kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira nchini Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ya kuhujumu uchumi imeahirishwa mpaka Feburuary 22, 2018 ya mwaka huu. Chanzo cha kuahirishwa kwa kesi hiyo ni kutokana na DPP kushindwa kukamilisha kusaini hati ya mashtaka hayo. Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri ambaye anasimamia kesi hiyo ameutaka upande wa Jamhuri kuhakikisha hati ...

Read More »

DIAMOND NA HAMISA MOBETTO WAFIKISHANA TENA MAHAKAMANI

Mwanamuziki Diamond Platnumz na mzazi mwenzake, Hamisa Mobetto wamefika katika Mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza shauri linalohusu matunzo ya mwanao. Novemba 10 ,2017 Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto alitupilia mbali kesi hiyo juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul. Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi ...

Read More »

TANZIA: MWANASIASA TAMBWE HIZZA AMEFARIKI DUNIA

  TANZIA Mwanasiasa Tambwe Hizza amefariki dunia leo alfajiri akiwa nyumbani kwake jijini Dar es salaam. Tambwe Hizza alikuwa katika timu ya waratibu wa kampeni za mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu.

Read More »

WATU ZAIDI YA 20 WAUAWA KATIKA SHAMBULIO LA ANGA NCHINI SYRIA

Takriban watu 23 wameuawa hadi sasa katika mashambulio ya anga ya vikosi vya serikali nchini  Syria katika eneo la mashariki mwa Ghota karibu na mji wa Damascus, kuna kodaiwa kuwa ni ngome ya waasi. Waangalizi wa haki za binadamu kutoka Uingereza waliopo katika maeneo hayo wameelezea hali hiyo na madhara kwa watu kutokana na mashambulio hayo. Umoja wa mataifa umetoa ...

Read More »

KOREA KASKAZINI KUONYESHA UIMARA WA JESHI LAKE KABLA YA OLIMPIKI

Korea Kaskazini linatarajiwa kuandaa maadhimisho ya 70 ya gwaride la jeshi lake kabla ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini. Gwaride la kila mwaka la Pyongyang linaloadhimisha kuanzishwa kwa jeshi la Korea Kaskazini limekuwa likifanywa kila mwezi Aprili kwa kipindi cha miaka 40. Hatahivyo vyombo vya habari nchini humo vilitangaza mapema mwaka huu kwamba ...

Read More »

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YATEKELEZA MWONGOZO WA HUDUMA KWA WATUMISHI WA UMMA WENYE ULEMAVU

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Bw. Abbas Mpunga kabla ya kumkabidhi Bajaji ili kumwezesha mtumishi huyo kutekeleza majukumu yake. Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa ofisi yake wakati wa tukio la kumkabidhi Bajaji kwa mmoja wa watumishi ...

Read More »

POLE POLE AMTAKA MKURUGENZI HALMASHAURI ILALA KUTOA UFAFANUZI MIKOPO WANAYOTOA

KATIBU wa Nec Itikadi na uenezi Taifa wa Chama cha Mapinduzi, Humphrey Polepole ameuagiza uongozi wa Chama hicho wilaya chini ya Ubaya Chuma kumuita mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala na wasaidizi wake ili kupata ufafanuzi kuhusu mikopo wanayotoa. Amesema kuwa pamekuwepo na malalamiko mengi juu ya eneo hilo hivyo lazima viongozi hao wachama Wilaya kuwaita viongozi hao wa Halmashauri ili ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons