Daily Archives: February 12, 2018

SERIKALI IMESEMA ITAENDELEA KUIMARISHA MFUMO WAKE WA UTOAJI DAWA

div dir=”ltr” style=”text-align: left;” trbidi=”on”> Na Mwandishiwetu Serikali imesisitiza kwamba itaendelea kuimarisha mifumo yake ya utoaji huduma za dawa kutokana na ukweli kwamba baadhi ya dawa zinatumika kwa wanyama na binadamu na kuleta usugu wa ugonjwa husika kwa mgonjwa na  gharama kubwa kwa taifa.   Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na watoto,Dr Faustine ...

Read More »

NEC: Maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Marudio Yanakwenda Vizuri

Zikiwa zimebaki siku 6 kabla ya uchaguzi mdogo wa ubunge Siha na Kinondoni na kata nane kufanyika, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema maandalizi yanaendelea vizuri. NEC imesema maandalizi hayo ni pamoja na ufumbuzi wa changamoto ndogondogo zinazojitokeza. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima amesema hayo baada ya mkutano wa watendaji wa Tume na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo ...

Read More »

MWAKYEMBE: KWA SIMBA HII, SASA TANZANIA TUNAELEKEA KUWA KICHWA CHA MUUNGWANA, NA SI CHA MWENDAWAZIMU

    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe ameeleza kufurahishwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Africa kati ya Simba SC na Gendarmerie ya nchini D’jbout ambapo Simba iliibuka kidedea kwa kuichapa timu hiyo mabao 4 – 0, mechi iliyochezwa katika uwanja wa taifa Dar es Salaam. Waziri Mwakyembe alieleza kuwa kwa kiwango cha soka kilichoonyeshwa ...

Read More »

MZEE AKILIMALI ALITOLEA UVIVU BENCHI LA YANGA SC, CHIRWA KUKOSA PENATI MFULULIZO

KATIBU wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Ak­ilimali, amelitaka benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Mzam­bia, George Lwandamina, kuhakikisha wanatafuta mbadala wa mchezaji atakayekuwa anapiga pen­alti badala ya Mzambia, Obrey Chirwa. Mzee Akilimali ameyasema hayo kufuatia mshambuliaji huyo kuwa na mfululizo wa kukosa penalti ambapo juzi Jumamosi alikosa tena wakati Yanga iliposhinda bao 1-0 dhidi ya ...

Read More »

RAIS WA ZAMANI WA LIBERIA ELLEN JOHNSON SIRLEAF ASHINDA TUZO YA KIONGOZI BORA WA AFRIKA INAYOTOLEWA NA MO IBRAHIM

Rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ameshinda tuzo ya mwaka ya Mo Ibrahim kwa Uongozi wa Afrika – ambayo hupewa viongozi wa Afrika ambao wameonekana kuwa na utawala mzuri. Ellen Johnson Sirleaf amekuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya Urais mwaka 2006 na kumaliza muda wake mwezi uliopita baada ya kuhudumu kwa mihula miwili. Kamati ya ...

Read More »

MAN UNITED YAPIGWA, LIVERPOOL YATAKATA EPL

Klabu ya soka ya Manchester United jana imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa klabu ya Newcastle United. Bao pekee katika mchezo huo wa ligi kuu ya soka nchini England uliomalizika jana jioni kwenye uwanja wa Saint James Park limefungwa na Matt Ritchie dakika ya 65.   Kwa upande wa kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameendelea kuwa na rekodi ...

Read More »

ANGALIA MADHARA YA KUJIPIGA PICHA MWENYEWE (SELFIE) UKIWA KWENYE MAENEO YA HATARI

Mwanamke mmoja amefariki akipiga picha aina ya Selfie na rafikiye katika barabara ya treni nchini Thailand. Rafikiye alisema kuwa walikuwa wamekunywa pombe na kuamua kujipiga picha hiyo na treni lakini hawakuona treni nyengine iliokuwa ikija kutoka barabara nyengine ya treni, kwa mujibu wa polisi. Miguu yake ilikatika na kufariki hospitalini ambako alikuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi. Rafikiye wa kiume alipata ...

Read More »

HATMA YA RAIS JACOB ZUMA KUNG’ATUKA MADARAKANI KUJULIKANA LEO

  Kiongozi wa Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama kitafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya Rais Jacob Zuma. Akizungumza kaika mkutano wa hadhara mjini Cape Town, Ramaphosa amedokeza kuwa Rais Zuma atatakiwa kujiuzulu. Amesisitiza kuwa wala rushwa wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema Nelson Mandela, baba wa taifa ...

Read More »

CHADEMA : Mawakala wetu wamenyimwa viapo Kinondoni

Jana ilikuwa ndiyo siku ya kuwatambulisha na kuwaapisha mawakala kwa ajili ya Uchaguzi wa Marudio Jimbo la Kinondoni, Mawakala wa CHADEMA wamekataliwa kuapishwa. Awali tulibaini tatizo hilo Kata ya Hananasif ambapo Mtendaji wa Kata aitwae Richard Supu (0655998777), aligoma kuwaapisha mawakala hao akiwataka waache majina yao hadi atakapowaita siku tatu kabla ya siku ya kupiga kura. Jambo ambalo ni kinyume ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons