Lala Salama ya Ubunge kwa Chadema, CCM
Na Waandishi Wetu Vyama vyenye ushindani mkubwa wa kisiasa nchini, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) vinaingia wiki ya mwisho kwa kampeni za uchaguzi mdogo katika majimbo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na Siha mkoani Kilimanjaro. CCM imewasimamisha Dk Godwin Mollel (Siha) na Maulid Mtulia (Kinondoni) wakati wagombea wa…