Daily Archives: March 1, 2018

Wafaulu bila kujua kusoma wala kuandika

Na Alex Kazenga MVOMERO Wakati matokeo ya darasa la saba kwa mwaka jana nchini yakionesha ufaulu kuongezeka kwa asilimia 72.76 ikilinganishwa na 70.36 ya mwaka 2016, imebainika kuwapo waliofaulu bila kujua kusoma wala kuandika. Uwepo wa hali hiyo ya watoto kufaulu bila kujua kusoma wala kuandika, imebainika hivi karibuni kupitia uchunguzi uliofanywa na JAMHURI katika Kijiji cha Kambala, Wilaya ya ...

Read More »

Tusipoziba ufa, tutajenga ukuta…

NA ANGELA KIWIA Ni wiki moja sasa tangu nchi yetu ikumbwe na kilio cha kumpoteza mpendwa ndugu yetu, Akwilina Akwilini. Sitaki kabisa kukumbuka tukio hilo lililojaa simanzi na taharuki katika bongo zetu. Maisha ya Mtanzania sasa yanaanza kuogofya. Tunaishi kwenye nchi ya amani iliyoanza kumea vilio vya kukosekana na kutoweka kwa amani. Tunamzika binti yetu huku Mtanzania mwingine akiuawa kwa ...

Read More »

Oliver Mtukudzi mwanamuziki mkongwe Afrika

Na Moshy Kiyungi Oliver Mtukudzi ni mwanamuziki mkongwe, anayevuma sana hata nje ya mipaka ya nchi yake ya Zimbabwe. Nyimbo zake zinazohamasisha amani na kutoa burudani barani Afrika, zimesababisha yeye kutumika kama alama katika taifa hilo hususan kwa upande wa sanaa ya nchini mwake. Wasifu wa Oliver ‘Tuku’ Mtukudzi unaeleza kuwa alizaliwa Septemba 22, 1952 mjini Highfield, Harare. Ni mwanamuziki ...

Read More »

Frostan yasalimu amri, yateketeza nyama mbovu

NA MICHAEL SARUNGI Hatimaye Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), imeteketeza kilo 1,103.58 za nyama mbovu, mali ya kampuni ya Frostan Limited ya Dar es Salaam. Kuteketezwa kwa nyama hiyo kumefanyika Februari 21, mwaka huu, ikiwa ni baada ya JAMHURI kuwa gazeti pekee lililoibua biashara hiyo haramu kwa mujibu sheria za nchi, lakini pia ikihatarisha afya na uhai wa watu. ...

Read More »

Wafugaji wa sungura wa kisasa ‘walizwa’ Moshi Vijijini

Na Charles Ndagulla, Moshi Tegemeo la kutajirika kwa wakazi zaidi ya 20 katika halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini kupitia mradi wa ufugaji wa sungura wa kisasa, limetoweka baada ya kuachwa na wawezeshwaji wao, kampuni ya Rabbit Bilss Tanzania. Viongozi wa kampuni hiyo iliyoanza kuhamasisha na kuwahudumia wakazi hao tangu mwaka 2016, hivi sasa hawawafikii wafugaji hao na sasa wafugaji ...

Read More »

Utumikishwaji: Bomu linalowalipukia watoto Dodoma

Na Zulfa Mfinanga, Dodoma Vitendo vya utumikishwaji wa watoto bado vinaendelea nchini licha ya kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 193 zilizokubaliana juu ya ukomeshaji wa ajira kwao. Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN) waliosaini azimio la kulinda haki za mtoto maarufu kama UN Convention on the Rights of the Child lililopitishwa mwaka 1990. Mkutano ...

Read More »

Mateso ni mwalimu katika maisha

“Bila mateso na kifo maisha ya binadamu hayawezi kukamilika.”-Viktor Frankl “Tunapewa baadhi ya mateso kwa ajili ya kutuadabisha na kutusahihisha kwa sababu ya namna yetu mbaya ya kuishi. Mateso mengine tunapewa si kwa ajili ya kutusahihisha makosa yetu ya zamani lakini ili kuzuia ya kesho. Mateso mengine hayana lengo lingine isipokuwa kumfanya mtu ampende Mungu zaidi kwa moyo.” -Tim Keller. ...

Read More »

Wachezaji walioitendea haki jezi namba 10

DAR ES SALAAM NA MICHAEL SARUNGI Katika jambo la upigaji kura kutoka kwa mashabiki wote duniani lililofanywa na mtandao wa soka wa Sokaa Africa, Wayne Rooney aliibuka mshindi katika nafasi ya kwanza akiwa na kura 60 huku akifuatiwa na Ronaldinho aliyepata kura 38. 1. Wayne Rooney Mchezaji huyu anaweza asiwe amefanikiwa kuchukua tuzo ya mwanasoka bora duniani, lakini anahesabika na ...

Read More »

Ndugu Rais siku ya kumuaga Akwilina ilikuwa nzito

Ndugu Rais, sijui niilaumu nafsi yangu au nimlaumu Mwenyezi Mungu aliyenifanya niishuhudie siku ya Alhamisi tarehe 22/2/2018 pale Chuo cha Usafirishaji, siku ambayo mwili wa Akwilina ulipokuwa unaagwa. Yaliyonigusa moyoni naapa hayatakuja kunitoka katika kifua changu siku zote zilizobakia katika maisha yangu, baba nchi imepinda! Ni nani asimame ainyooshe? Hakika siku hiyo ilikuwa ni siku ya kihoro! Nilishindwa kwenda kumwangalia ...

Read More »

Uchovu mara kwa mara – 2

Karibu tena msomaji wangu wa Safu hii ya Afya. Leo tutaendelea na mwendelezo wa mada yetu ya wiki iliyopita kama nilivokuahidi. Kwa kukukumbusha tu msomaji, wiki iliyopita nilieleza kuhusu sababu zilizo nyuma ya uchovu uliokithiri. Uchovu ambao mara nyingi huwa unakuja bila kujua hasa chanzo chake; na wiki iliyopita nilikueleza sababu mbili kati ya nyingi tutakazoendelea nazo wiki hii ambazo ...

Read More »

TFF itumie vyema fursa ya FIFA

DAR ES SALAAM NA MICHAEL SARUNGI Ujio wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino, hapa nchini unaweza kuwa na matokeo mazuri katika soka la nchi hii endapo viongozi watakuwa na utashi wa kutenda. Wakizungumza na JAMHURI kwa nyakati tofauti juu ya ziara hiyo, wadau wa mchezo huo wamesema ziara hiyo ya kiongozi huyo mkuu wa ...

Read More »

Mapitio ya sheria za kazi nchini Tanzania

Na Wakili Stephen Malosha Asiyefanya kazi na asile. Hayo ni maneno maarufu sana katika utawala huu wa awamu ya tano. Maneno haya yamekuwa yakitamkwa mara kwa mara na Rais John Magufuli katika kuhimiza Watanzania wafanye kazi. Hii inaonesha kwa namna moja au nyingine umuhumu wa dhana ya kazi katika nchi yetu, na kwamba anayefanya kazi anastahili kupata ujira (ili apate ...

Read More »

TPA inathamini mizigo ya wateja

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imefanya mambo mengi katika utoaji huduma bora kwa wateja wake. Ili kuhakikisha TPA inawahudumia wateja wake vizuri iliamua kuwa na Mkataba wa Huduma kwa Mteja, kuanzisha Kituo cha Huduma kwa Wateja na kufungua Dawati la kushughulikia malalamiko ya wananchi.   Ndugu msomaji, katika makala hii tunakujulisha hatua ambazo mteja anapaswa kuchukua iwapo mzigo ...

Read More »

Ya Jacob Zuma ni ya kwetu pia

Kwenye hotuba aliyotoa ndani ya Bunge la Afrika Kusini baada ya kuanguka kwa utawala wa kibaguzi wa nchi hiyo, Mwalimu Julius Nyerere alilalamika jinsi ulimwengu unavyoiona Afrika, siyo kama bara linalojumuisha nchi zaidi ya 50, ila kama nchi moja. Ulimwengu, hasa wa nchi zilizoendelea umechagua kuliona Bara la Afrika kama moja, na huzungumzia masuala ya Afrika kufanana kuanzia Misri hadi ...

Read More »

Tanzania iongeze kasi ya ukuaji wa uchumi wake – 1

Na Frank Christopher Kwa zaidi ya muongo mmoja, uchumi wa Tanzania umeweza kukua wastani wa asilimia 7 na kufanikiwa kutajwa kati ya nchi 10 zinazoshuhudia ukuaji wa kasi zaidi wa uchumi barani Afrika huku nyingine zikiwa Ethiopia, Ivory Coast, Senegal, Kenya kwa kuzitaja chache (Taarifa ya Benki ya Dunia, 2017). Licha ya kuwa na uchumi uliokua kwa wastani wa asilimia ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons