Daily Archives: March 8, 2018

NIDA KUZINDUA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KIGOMA, RUKWA NA KATAVI

Kaimu Ofisa Uhusiano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Rose Joseph akielezea mikakati ya kuzindua usajili wa vitambulisho Kigoma, Rukwa na Katavi sambamba na ndani ya mgodi wa Tanzanite. MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA)  inatarajia kuzindua usajili na utoaji wa  vitambulisho hivyo katika mikoa mitatu ya Katavi, Kigoma na Rukwa. Pia  NIDA  kwa kushirikiana na  Wizara ya Madini , imeanza  ...

Read More »

Zifahamu taratibu Kombe la Dunia Urusi

MOSCOW, URUSI Michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika nchini Urusi kuanzia Juni hadi Julai mwaka huu, ni tofauti na michuano mingine ya miaka iliyopita kwa sababu ya sheria za nchi hii ambazo ni tofauti na nyingine. Kanuni na sheria za nchi hii zina utofauti mkubwa ambao umesababisha mabadiliko kadhaa katika masuala ya usafirishaji na usalama; ikiwa ni miongoni mwa ...

Read More »

Ndugu Rais, amani kwanza mengine tutayapata kwa ziada

Ndugu Rais, lengo la maandiko yetu siku zote siyo kukosoa. Udhaifu wa kuandika kwa sababu unampenda mtu au unamchukia mtu, Mwenyezi Mungu katuepusha nao. Hatuandiki kwa ushabiki wa kumshabikia mtu au chama fulani. Wala hatuandiki hapa kwa lengo la kusifia au kupongeza. Tunaandika kile ambacho tunaamini kuwa ni ukweli mtupu, kwa lengo la kushauri tu. Tunaamini kuwa kwa hizi busara ...

Read More »

Bandari ya Dar kuhudumia kontena milioni 16

Na Michael Sarungi Ukarabati unaofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam, umewezesha ongezeko la kuhudumia shehena za mizigo kutoka tani milioni 10 kufikia tani milioni 16 kwa mwaka. Kiwango hicho kinatarajiwa kuongezeka kufikia tani milioni 25 mwaka 2030, ikichochewa na kasi ya ukuaji wa biashara ya bandari inayolazimu kuwapo mageuzi yanayogusia ukarabati huo. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari ...

Read More »

Dekula Kahanga ‘Vumbi’: Mcongo anayemiliki bendi yake Sweden

Na Moshy Kiyungi Dekula Kahanga ni mwanamuziki aliyetokea nchini na kujikita katika jiji la Stockholm nchini Sweden. Ameweza kutafuta mafanikio hadi kuunda bendi yake anayojulikana kama Dekula band. Kabla ya kwenda nchini humo, Kahanga alikuwa mpigaji wa gitaa la solo katika bendi ya Maquis Original, iliyokuwa ikipiga muziki wake katika ukumbi wa Lang’ata,  Kinondoni jijini Dar es Salaam katika kipindi ...

Read More »

Mipaka ya Tanzania, Kenya ‘kutafuna’ Sh bilioni nne

Na Charles Ndagulla, Moshi Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, amesema Serikali imepata Sh bilioni nne zitakazotumika kurekebisha mipaka iliyopo kwa nchi za Tanzania na Kenya inayoharibika na mingine kuwa na umbali mrefu. Mabula ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya kutembelea eneo la mpaka wa nchi hizo katika tarafa ya Tarakea mkoani Kilimanjaro. ...

Read More »

Dawa za nguvu za kiume bila ushauri wa daktari ni hatari

“Samahani daktari, asubuhi ya siku tatu zilizopita kaka yangu alikutwa amekufa chumbani kwenye nyumba ya wageni alipokwenda kupumzika na mpenzi wake…” “Lakini baada ya kumhoji huyo mpenzi wake, alisema wakati wameingia chumbani alikunywa vidonge kadhaa ambavyo baadaye, wataalamu waligundua vilikuwa vya kuongeza nguvu za kiume. Je, ni kweli dawa za kuongeza nguvu za kiume zinaweza kusababisha kifo?” Hilo ni swali ...

Read More »

Urusi yalaumiwa

Marekani imeishutumu Urusi kwa kukiuka hadharani mikataba iliyoafikiwa katika enzi za Vita Baridi, kwa kuunda kile Rais wa Urusi, Vladimir Putin, alichokitaja kuwa kizazi kipya cha silaha madhubuti. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeghadhabishwa na tamko la Putin na kusema kuwa Rais huyo wa Urusi amethibitisha madai ambayo yamekuwako kwa muda mrefu kuhusu mpango wake wa nyuklia. Msemaji ...

Read More »

Wahamiaji waandamana Israel

Mamia ya wahamiaji wa Kiafrika waishio nchini Israel wameandamana huku wakiendelea na mgomo wa kutokula wakipinga sera mpya ya Israel yenye utata ya kutaka ama kuwafunga na kisha kuwarejesha makwao. Wahamiaji hao walitembea umbali mfupi kutoka kituo cha wazi cha Holot hadi gereza la Saharonim, wakipaza sauti na kutoa ishara za kutaka kuachiwa kwa wafungwa wenzao ambao wapo magerezani nchini ...

Read More »

Fomu muhimu unapotoa gari bandarini

Na Mwandishi Maalum Katika Makala ya “Njia rahisi ya kutoa gari bandarini” ambayo iliwahi kuchapishwa na gazeti hili, tulielezea hatua mbalimbali ambazo wakala wa forodha anatakiwa kuzifuata ili aweze kutoa gari la mteja wake kutoka bandarini. Lengo la makala hii tunaelezea umuhimu wa fomu za Vehicle Discharge Inspection Transfer Tally (VDITT) na ile ya makabidhiano ya gari (Hand Over Form) ...

Read More »

Dodoma yakabiliwa na upungufu wa nyuma

NA EDITHA MAJURA Dodoma Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kuandikwa, amesema wenye uwezo wa kujenga nyumba za kupangisha, kufanya hivyo mkoani Dodoma ili kusaidiana na Serikali kuwapatia  makazi bora watumishi wanaohamia mjini humo. Kuandikwa amesema licha ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kumiliki nyumba 960 za kibiashara mkoani humo, hawajakidhi mahitaji ya nyumba yaliyopo kwa sasa. Kaimu ...

Read More »

Mafanikio yoyote yana sababu (12)

Na Padre Dk. Faustin Kamugisha Kujali ubora (excellence) ni sababu ya mafanikio. Kutia fora ni sababu ya mafanikio. Ni kufanya jambo liwe bora zaidi. “Hakuna aliyewahi kujutia kwa kutoa kitu kilicho bora zaidi,” alisema Sir George Stanley Halas (1895 – 1983). Huyu aliitwa “Bwana Kila Kitu” alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu, kocha na mmiliki wa Timu ya “Chicago Bears” ...

Read More »

Mfumo wetu wa elimu haufai

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa takwimu tunazopawa kuzitumia kutafakari hatima yetu kama Taifa. Sasa inakadililiwa kuwa idadi ya Watanzania ni milioni 54.2. Mwaka 2021 idadi hiyo itapaa hadi kufikia watu milioni 59. Hili ni ongezeko kubwa. Lakini imebainishwa na NBS kuwa kati ya Watanzania 100, watu 92 ni tegemezi! Hii ni hatari kwa watu na kwa Serikali yenyewe. ...

Read More »

Miaka 61 Uhuru wa Ghana: Tunajifunza?

Hotuba ya rais wa kwanza wa Ghana, Kwame Nkrumah siku ya uhuru wa nchi yake Machi 6, 1957 ilikuwa na ujumbe mmoja mzito: Uhuru wa Ghana hautakuwa na maana yoyote iwapo nchi nyingine za Afrika zitabaki chini ya utawala wa kikoloni. Aliona jukumu la Ghana ni kusaidia kulikomboa Bara la Afrika kupata uhuru kamili. Miaka sita baadaye kwenye kikao cha ...

Read More »

Siasa zimetosha, tuingie viwandani

Na Deodatus Balile   Miaka ya 1950 wakati Tanganyika inapigania Uhuru lengo kuu lilikuwa ni kukomboa watu wetu kutokana na unyanyasaji wa hali ya juu waliokuwa wanafanyiwa na Wakoloni. Hali ilikuwa hivyo hivyo kwa upande wa Zanzibar dhidi ya Waarabu. Wakoloni hawa walikuwa wanatulimisha kwa faida yao binafsi. Watu wetu walilima pamba, korosho, karafuu, mbaazi, karanga, kahawa na mazao mengine ...

Read More »

‘Bandari ya Dar itumike kuboresha biashara’

DAR ES SALAAM NA CLEMENT MAGEMBE Wafanyabishara katika soko la Kariakoo wameiomba Serikali kuweka mazingira mazuri yatakayowawezesha kuitumia bandari ya Dar es Salaam kwa ufanisi na kuboresha biashara zao. Wakihojiwa na JAMHURI wiki iliyopita, wafanyabiashara hao wamesema kuwapo kwa mazingira hayo kutawachochea kuagiza kwa wingi bidhaa kutoka nje ya nchi, hivyo kuchangia ongezeko la pato linalotokana na kodi na ushuru. ...

Read More »

‘Utitiri wa kodi unaua biashara’

DAR ES SALAAM NA CLEMENT MAGEMBE Wafanyabishara katika Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam wameiomba Serikali kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara wote nchini wapate fursa kubwa ya kuitumia Bandari ya Dar es Salaam, badala ya kuikimbia. Wafanyabiashara hao wamelieleza JAMHURI kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba kama mazingira mazuri ya biashara yataandaliwa yatatoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo na ...

Read More »

‘Wakorea Weusi’ watishia amani Mbeya

Na Thompson Mpanji, Mbeya   KUIBUKA kwa kundi kubwa la vijana wanaofanya uhalifu bila woga huku wakijiamini kutenda makosa ya jinai hata kutishia maisha na mali za wakazi wa Jiji la Mbeya wanaojiita “Wakorea Weusi”, limezidi kutia hofu na kuwalazimisha wananchi walio wengi kujiuliza maswali yasiyo na majibu kuwa ni akina nani hao? Wametumwa au ni wao wenyewe waliojiunga kwa kutumia zana ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons