UJUMBE WA PASAKA KUTOKA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA (KKKT)
TAIFA LETU, AMANI YETU A. UTANGULIZI “Fumbua Kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao; Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; uwapatie maskini na wahitaji haki yao” (Mithali 31: 8-9). Wapendwa wana KKKT, Watukuka, watu wote na familia ya Mungu katika Taifa letu, “Amani iwe kwenu!; Kristo Amefufuka (Yohana 20:19)….