April 30, 2018
Yah: Naamini wengi wetu ni bendera fuata upepo
Kuna wakati niliwahi kuandika barua mahususi katika uga huu, nikijaribu kuelezea madhara ya watu kuiga mambo na kushabikia bila kujua kile ambacho wanaiga kina madhara gani, wapo waigaji wa mambo bila kujua labda wanakoiga wanaigiza na siyo uhalisia. Mimi ni Mtanzania wa kuzaliwa, najivunia Utanzania wangu na ninaweza kuusema mahali popote pale bila kuwa na…
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kulakiwa na Donald Trump Marekani
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari atakuwa kiongozi wa kwanza wa taifa la kutoka bara Afrika kulakiwa na Rais wa Marekani Donald Trump White House atakapokutana na kiongozi huo kwa mashauriano rasmi mjini Washington baadaye leo. Marais wengine wa Afrika wamewahi kukutana na Bw Trump akiwa rais, wakiwemo Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa…
Adhabu iliyotangazwa kwa watakaokamatwa wametupa takataka hovyo Jijini Dodoma
Siku tatu baada ya Rais Dkt Magufuli kuipandisha hadhi Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema kuwa, mtu yeyote atakayekamatwa akitupa takataka hovyo, atakamatwa na kutozwa faini ya TZS 50 milioni, ikiwa ni kwa mujibu wa sheria ndogo za usafi. Mkurugenzi Kunambi ameyasema hayo jana Aprili 29 wakati akizungumza…
SIMBA YAPATA HARUFU YAUBINGWA BAADA YA KUITANDIKA YANGA 1-0
Bao pekee la Erasto Nyoni limeipa Simba ushindi dhidi ya watani zao wa jadi Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam . Nyoni alifunga bao hilo katika dakika ya 37 kwa kichwa, kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa kushoto mwa Uwanja na mshambuliaji Shiza Kichuya. Katika mchezo…