Daily Archives: May 1, 2018

Nchi inavyoliwa

*Wajanja watajirika huku serikali ikiambulia ‘makombo’ *Wachimbaji Mirerani wavamia Epanko *Mkuu wa Mkoa akiri udhaifu, asema wamewasiliana na mamlaka   NA ANGELA KIWIA Wakati serikali ikirekebisha sheria ya madini ili kunufaika na rasilimali  hizo za taifa, hali ni tofauti kabisa kwenye machimbo ya madini ya Spinel yanayochimbwa Epanko, Ulanga, mkoani Morogoro. Uchunguzi wa gazeti la JAMHURI, umebaini kwamba wafanyabiashara wa ...

Read More »

Raia maskini wakimbilie wapi?

Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, imethibitisha taarifa za polisi wake kumuua mtuhumiwa aliyekuwa mikononi mwao. Kijana ameuawa kwa kuchomwa kisu mgongoni. Hiyo pekee inajenga mazingira ya kutuaminisha kuwa kijana yule hakuwa tishio kiasi cha kutumika nguvu kubwa kumtoa uhai. Kuchomwa kisu mgongoni kunaweza kutujengea mazingira ya kuamini kwamba hakuwa kwenye mapambano na aliyemuua. Laiti kama kisu kile kingekuwa kimemwingia kifuani ...

Read More »

Tunawapongeza wafanyakazi

Wafanyakazi wa Tanzania leo wanaungana na wenzao duniani kote katika maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi). Siku ya leo ni muhimu kwa sababu inasaidia kutambua mchango mkubwa na wa kipekee wa wafanyakazi katika ustawi wa jamii yote duniani. Tunachukua fursa hii kuwapongeza wafanyakazi wote nchini ambao kwa juhudi zao Taifa letu limeweza kupiga hatua kubwa katika maendeleo. Wakati ...

Read More »

Mafanikio yoyote yana sababu (20)

Mafanikio yoyote yana sababu (20) Padre Dk Faustin Kamugisha Kutenda au kuchukua hatua ni siri ya mafanikio.  Ahadi ni wingu, kutenda ni mvua. Ni methali ya Kiarabu. “Kutenda ni ufunguo wa msingi wa mafanikio yote,” alisema Pablo Picasso (1881-1973), mwandishi wa maigizo, mpaka rangi na mchongaji wa sanamu wa Hispania. Matendo yana kauli kuliko maneno. Watu wanaofaulu wanafika juu ya mlima kwa ...

Read More »

Sokous Stars inavyochachafya

NA MOSHY KIYUNGI Tabora Kundi la wanamuziki wa Soukous Stars limekuwa likifanya vyema pindi wanapopata mchongo popote pale Duniani. Hawa ni wanamuzikia raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huishi katika nchi tofauti duniani, kila mmoja huko aliko anayo shughuli ya kuendesha maisha yake. Mfano wa karibu ni wanamuziki Lokassa ya Mbongo ambaye ni maarufu kwa kulicharaza gitaa la rhythm, ...

Read More »

MFAHAMU MMILIKI HALISI WA KINYWAJI CHA ALIKIBA

Siku ya juzi jumapili April 29, 2018 msanii Alikiba katika sherehe ya harusi yake iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, alizindua kinywaji chake kipya kinachojulikana kama Alikiba Mofaya. Kinywaji hicho ambacho hakina kilevi na chenye kuongeza nguvu (energy drink) kimewashangaza wengi kutokana na kuzinduliwa hafla tofauti na weni walivyotaraajia kuwepo kwa matangazo mbalimbali kabla ya uzinduzi wake. ...

Read More »

Bandari ya Tanga fursa muhimu kwa uchumi wa Tanzania

Katika toleo la wiki iliyopita tuliwaletea makala iliyohusu bandari ya Mtwara kwa jinsi ilivyobeba fursa ya viwanda kwa ukanda wa kusini mwa Tanzania na taifa kwa jumla. Pia bandari ya Mtwara inatarajiwa kuwa tegemeo kwa nchi jirani hasa baada ya uboreshaji na upanuzi wa bandari ya Mtwara kukamilika kwa jinsi utakavyokuwa chachu ya kufungua milango katika kuhudumia shehena kutoka nchi ...

Read More »

Timu za vijana zaibeba Afrika

NA MICHAEL SARUNGI Kufanya vyema kwa timu za taifa za vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes, na ile ya chini ya miaka 17 Serengeti Boys katika michezo yao ni mwendelezo wa matokeo mazuri kwa timu za taifa za vijana barani Afrika. Wakizungumza na JAMHURI kwa nyakati tofauti, wadau wa mchezo huo nchini wamesema matokeo hayo ni mwendelezo wa kile ambacho ...

Read More »

Hatimae historia yaandikwa

Kim Jong-un amekuwa kiongozi wa kwanza kutoka Korea kaskazini kuingi Korea kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea mwaka 1953 na kuandika historia mpya baina ya mataifa hayo mawili. Kim katika mkutano huo aliandamana na maafisa tisa , ikiwemo dadake ambaye aliongoza ujumbe wa Korea Kaskazini katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini mapema mwaka huu. ...

Read More »

Bomu la watu laja Afrika – 3

Balile

Na Deodatus Balile Kwa wiki ya tatu sasa nafanya mapitio ya kitabu kiitwacho “Making Africa Work”. Tafsiri isiyo rasmi jina la kitabu hiki linamanisha “Mbinu za Afrika kujikwamua kiuchumi.” Kitabu hiki kimeandikwa na Greg Mills, Olusegun Obasanjo (Rais mstaafu wa Nigeria), Jeffrey Herbst na Dickie Davis. Kimechapishwa na Taasisi ya Brenthurst Foundation ya Johannesburg, Afrika Kusini. Rais (mstaafu) Benjamin Mkapa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons