Daily Archives: May 15, 2018

JINSI RAIS MAGUFULI ALIVYOFANYA ZIARA YA GHAFLA BANDARINI DAR ES SALAAM KUKAGUA MATANKI YA MAFUTA YA KULA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa ...

Read More »

Harbinder Singh Sethi Aondolewa Kwenye Kampuni ya IPTL

Mwenyekiti wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Singh Sethi ameondolewa katika nafasi yake ya uenyekiti na bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo, baada ya kushindwa kuhudhuria vikao vya bodi kwa miezi sita mfululizo tangu Juni 16, 2017. Vilevile, Sethi ameondolewa katika orodha ya wakurugenzi wa bodi ya kampuni hiyo kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao ...

Read More »

Platinum Credit

  Vita ya mafuta Yahusisha wafanyabiashara vigogo Kamati ya Bunge sasa ‘yagawanyika’ Wajumbe baadhi waomba waondoke NA WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM Mpasuko umejitokeza ndani ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira; sababu kuu ikitajwa kuwa ni biashara ya mafuta ya mawese kutoka Indonesia na Malaysia. Hatua hiyo imewafanya baadhi ya wabunge waoneshe kusudio la kumwomba ...

Read More »

Platinum Credit yawaliza Watanzania

DAR ES SALAAM NA CLEMENT MAGEMBE Wafanyakazi wa Kampuni ya Mikopo ya Platinum Credit Ltd Tanzania wamelalamikia kitendo cha kampuni hiyo kuwatoza wateja wake riba kubwa na kushinikiza taasisi za umma kuingia katika mikataba ya mikopo kwa rushwa. Wafanyakazi hao ambao hawakutaka majina yao kuandikwa wamelieleza JAMHURI kuwa Kampuni ya Platinum inatoza riba kubwa ya mikopo tofauti na taasisi nyingine ...

Read More »

Tusi gani la kututoa usingizini?

Desemba 6, mwaka jana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alitangaza uamuzi wa Serikali wa kuundwa chombo maalumu ili kusimamia eneo la kilometa za mraba 1,500 katika Pori Tengefu la Loliondo. Akasema: “Baada ya kupitia mifumo mbalimbali, timu ya wataalam ilipendekeza kuwa utumike mfumo maalum utakaounda chombo maalum, kwa kuwa una maslahi mapana kwa pande zote husika na unalenga kuleta amani na ...

Read More »

Bandari ya Kyela yang’arisha Nyanda za Juu Kusini

Na Mwandishi Maalum   Katika makala ya wiki iliyopita tuliwaelezea umuhimu wa Bandari ya Kigoma katika kukuza maendeleo ya uchumi wa taifa letu ambalo lipo katika mapinduzi ya kuifanya Tanzania kuwa nchi inayotegemea uchumi wa viwanda. Katika makala hii tutawaelezea nafasi ya Bandari ya Kyela katika kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa Nyanda za Juu Kusini na nchi jirani za Malawi ...

Read More »

Ufisadi kwenye Miradi ya Maji

DODOMA. EDITHA MAJURA. Ufisadi kwenye Miradi ya Maji Madai ya baadhi ya watendaji wasiyo waadilifu kushirikiana na wakandarasi, kuiba fedha zinazoidhinishwa na Bunge na kutolewa na serikali kwa ajili ya kujenga miradi ya maji, ni miongoni mwa hoja zilizounganisha wabunge wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Wakati wengine wakitaka iundwe Kamati Maalumu ya Bunge kuchunguza ...

Read More »

Fally Ipupa anatamba kwa muziki wa Kongo

NA MOSHY KIYUNGI Tabora Sifa za mwanamuziki Fally Ipupa zimeenea kila pembe kuliko na wapenzi wa muziki wa dansi. Yeye pamoja na mwenzake, Ferre Golla; wanatajwa kuelekea kuchukua nafasi za wanamuziki wakubwa waliomtangulia. Hawa ni wanamziki vijana wanaotamba katika anga ya muziki Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wanapishana kwa mwaka mmoja wa kuzaliwa – Ferre Gola alizaliwa Machi 3, 1976 ...

Read More »

Mnunuzi wa ardhi yako ameshindwa kumaliza malipo?

NA BASHIR YAKUB Umemuuzia mtu kiwanja au nyumba. Mmeandika mkataba na kuusaini tena mbele ya mwanasheria. Kwenye mkataba mmeweka vipengele vingi lakini kimojawapo kinahusu umaliziaji wa pesa ya manunuzi. Hii ni kwa sababu mnunuzi amelipa kiasi kidogo na kiasi kingine ameahidi kwenye mkataba kukimalizia baada ya muda fulani. Mkataba umesainiwa na umekamilika. Muda umekwenda na kufika ule ambao mnunuzi alitakiwa ...

Read More »

Mafuta yapatiwe jawabu la kudumu

Mjadala unaohusu mafuta ya kula ya mawese yanayoingizwa nchini kutoka Indonesia na Malaysia, umechusha. Kila mwaka kelele kwenye biashara hii imekuwa jambo la kawaida-mvutano ukiwa Serikali kwa upande mmoja dhidi ya wafanyabiashara kwa upande mwingine. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mara kadhaa imesema mafuta ya mawese yanayoletwa kutoka katika mataifa hayo si ghafi, lakini wafanyabiashara wamekuwa na msimamo tofauti. Yamekuwapo ...

Read More »

Ndugu Rais wamekunywa sumu mbona hawadhuriki?

Ndugu Rais waasisi wa nchi zetu hizi tatu, Tanganyika, Kenya na Uganda waliwajengea fikra ya umoja wananchi wake. Tuliopata nafasi ya kufanyakazi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ile iliyovunjika tunaweza kuthibitisha kuwa wananchi sisi na hasa tuliokuwa kwenye mashirika yake tulikuwa wana ndugu pasipo shaka. Watanzania wanaofanyakazi leo katika Jumuiya Afrika Mashariki wana Utanzania zaidi kuliko Uafrika Mashariki. Na Wakenya ...

Read More »

Bomu la watu laja Afrika – 4

Balile

Wiki tatu zilizotangulia kabla ya wiki iliyopita, nilichambua kitabu kinachohusu njia mbadala za kufufua uchumi wa Afrika. Nilikisitisha wiki iliyopita tu, kutoa fursa ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani. Kitabu hiki kinaitwa “Making Africa Work”. Tafsiri isiyo rasmi ya jina la kitabu hiki inamanisha “Mbinu za Afrika Kujikwamua Kiuchumi.” Kitabu hiki kimeandikwa na Greg Mills, Olusegun Obasanjo ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons