Monthly Archives: June 2018

Mmiliki wa Mabasi ya Zacharia Akamatwa

MMILIKI wa mabasi ya ‘Zacharia’, Peter Zacharia, anashikiliwa na vyombo vya dola mkoani Mara kwa tuhuma za kuwapiga risasi maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wakiwa katika majukumu yao. Maofisa hao wanasemekana wako hospitali ya mjini Tarime wakipata matibabu ambapo mmiliki huyo wa mabasi anategemewa kufikishwa mahakamani wakati wowote.

Read More »

Mali ya Yahya Jammeh kupigwa mnada

Serikali ya Gambia inapanga kuuza ndege za kifahari pamoja na magarai ya rais wa zamani Yahya Jammeh kwa njia ya mtandao. Nchi majirani waliingilia kati kumtimua madarakani Rais Jammeh baada ya kushindwa kwenye uchaguzi Disemba mwaka 2016 ambapo alikataa kuondoka madarakani. Aliacha nyuma ndege tano na magari 30 ya kifahari, yakiwemo ya Rolls-Royce na Bentley pamoja na mashamba manne, kwa ...

Read More »

Zari: Diamond Alipokuja Alilala chumba kingine na mimi nikalala chumbani kwangu.

ALIYEKUWA mpenzi wa Diamond Platinumz, Zarina Hassan “Zari The Bosslady”, amefunguka kuhusu alivyoombwa msamaha mara kibao na watu mbalimbali akiwemo Babu Tale ambaye hivi karibuni alisafiri hadi Afrika Kusini kumshawishi arudiane na staa huyo.   “Babu Tale alikuja Pretoria, alitaka turudiane na Diamond kwa ajili ya watoto, sikuona ubaya katika hilo, lakini mambo ya mapenzi hapana tena, watu haohao wa ...

Read More »

VITA YA 16 BORA URUSI LEO: ARGENTINA VS UFARANSA HUKU URUGUAY VS URENO

Kimbembe cha michuano ya Kombe la Dunia hatua ya 16 bora kinaendelea leo kwa mechi mbili kushika kasi huko Urusi. Kunako majira ya saa 11 jioni, Urafansa itakuwa inacheza dhidi ya Argentina, mechi ambayo itakuwa na msisimko wa aina yake kutokana na timu hizo mbili kuzungukwa na nyota wawili wakubwa. Ufaransa watakuwa wanaingia dimbani wakiwa na nyota wao anayekipiga Atletico ...

Read More »

SERIKALI YATENGA 4.3bn/- KUJENGA VITUO VYA KUHIFADHI DAMU SALAMA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 4.3 ili kujenga vituo vya kuhifadhi damu (satellite blood banks) kwenye mikoa 12.   Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Manyara, Katavi, Rukwa, Ruvuma na Njombe. Mingine ni Tanga, Arusha, Pwani, Singida, Songwe, Geita na Simiyu.   Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Juni 29, 2018) bungeni jijini Dodoma katika hotuba yake aliyoitoa wakati ...

Read More »

Waziri Mkuu Awasilisha Hoja ya Kuahirishwa Bunge la Bajeti

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa hoja ya kuahirishwa kwa mkutano wa 11 wa Bunge la Bajeti ulioanza Aprili 3 na kumalizika leo Ijumaa Juni 29, 2018. Akiwasilisha hoja hiyo leo bungeni, Majaliwa amesema maswali 530 ya msingi na 1705 ya nyongeza yameulizwa na wabunge. Pamoja na mambo mengine, Majaliwa amezungumzia masuala mbalimbali, zikiwemo halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya ...

Read More »

Diamond Platinumz: Daylan ni mwanangu halisi ‘msiniletee’

Msanii wa Tanzania Diamond Platnumz amewapuuzilia mbali wanaodhania kwamba yeye sio baba wa kweli wa mtoto wake wa kiume wa mwanamitindo Hamisa Mobetto. Diamond alichapisha ujumbe mkali katika mtandao wake wa Instagram akithibitisha kuwa Daylan ni mwanawe anayempenda sana. Hatua hiyo inajiri baada mwanamuzilki huyo kuchapisha kanda fupi ya video akivumisha ziara yake ya Marekani. Kanda hiyo fupi ya video ...

Read More »

Rooney Atimka Everton, Akimbilia Marekani

Aliyekuwa mshambuliaji wa Everton, Wayne Rooney (32) amesaini kandarasi ya miaka mitatu na nusu kuitumikia Klabu ya DC United inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Marekani. Rooney ambaye atakamilisha uhamisho wake huo wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa Julai 10 mwaka huu, atalipwa mkwanja kiasi cha Pauini Milioni 10 (sawa na Tsh. Bilioni 26.47) ambapo atakuwa ni mchezaji mwenye kulipwa pesa ndefu ...

Read More »

Tetesi za Usajili

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 26, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake katika klabu ya Uturuki ya Fenerbahce siku ya Jumatatu. (Sabah – via Talksport) Chelsea inakaribia kuipiku Real Madrid katika kumsajili kipa wa Roma Alisson katika mkataba ambao unaomthamini mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 kuwa na thamani ya £62m. (Marca – via Metro) Arsenal inatarajiwa ...

Read More »

Ratiba ya 16 Bora Kombe la Dunia 2018

Alhamisi ya June 28 tumeshuhudia michuano ya Kombe la Dunia 2018 hatua ya makundi ikimalizika kwa Afrika kupoteza timu zote 5 katika hatua ya makundi kutokana na kukosa point za kutosha kuingia hatua ya 16 bora. Katika hatua hiyo ya makundi timu zote 5 za Afrika zimeyaaga mashindanl hayo kutokana na kukosa alama za kuwavusha kwenye hatua hiyo ya makundi. ...

Read More »

Watu watano wauawa kwa shambulio la risasi Maryland Marekani

Polisi katika jimbo la Maryland nchini Marekani wanasema watu watano wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la risasi lililofanyika katika ofisi za kampuni ya Capital Gazette inayomiliki magazeti ya kila siku katika mji wa Annapolis. Wafanyakazi wa gazeti hilo wanasema mshambuliaji huyo ambaye ni mzungu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 ambaye alijiharibu vidole vyake ili kuepusha kutambulika ...

Read More »

Filimbi ya Kagame Cup Kuanza Kupulizwa Leo

Michuano ya Kagame Cup inaanza rasmi leo kwa mechi tatu kupigwa ambapo saa 8 mchana JKU ya Zanzibari itaanza kibarua chake dhidi ya Vipers SC kutoka Uganda. Baadaye saa 10 mechi ya rasmi ya ufunguzi itakuwa baina ya mabingwa watetezi, Azam FC dhidi ya Kator FC kutoka Sudan Kusini. Baada ya mechi hiyo majira ya saa 1 jioni, Singida United ...

Read More »

Belgium v England: Romelu Lukaku kuikosa mechi muhimu Kombe la Dunia

Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku anatarajiwa kuikosa mechi muhimu katika Kombe la Dunia dhidi ya England Alhamisi. Mechi hiyo itakayochezewa mjini Kaliningrad inatarajiwa kuamua nani atamalizakileleni katika Kundi G. Mchezo huo utaanza saa tatu saa za Afrika Mashariki. Mshambuliaji huyo wa Manchester United mwenye umri wa miaka 25 aliumia kwenye kifundo cha mguu wakati wa mechi ya Jumamosi dhidi ya ...

Read More »

UONGOZI GOR MAHIA WAJA JUU KUHUSIANA NA KAGERE, WAELEZA ALIDANGANYA

Imeelezwa uongozi wa Gor Mahia FC umeshangazwa na kitendo cha mshambuliaji wao tegemeo, Meddie Kagere kujiunga na klabu ya Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili. Wakati Kagere akiwa nchini Kenya ikiwa ni wiki kadhaa zimepita baada ya mashindano ya SportPesa Super Cup kumalizika, aliomba ruhusa kuelekea kwao Rwanda kwa ajili ya masuala yake binafsi. Lakini kilichokuja kuwashangaza ni Kagere ...

Read More »

Ujeruman Yaendeleza Record ya Bingwa Mtetezi Kutolewa Htaua ya Makundi

Imekuwa kawaida kwa bingwa wa Kombe la Dunia kutolewa hatua ya makundi, lakini hakuna aliyetegemea hilo lingetokea kwa Ujerumani. Ujerumani haikuwahi kutolewa katika hatua ya makundi katika miaka 80 iliyopita. Korea Kusini wameilaza kwa mabao 2-0 na kuitupa nje katika Kombe la Dunia katika hatua ya makundi. Maana yake wameivua ubingwa. Kipigo hicho kimezua hofu kubwa kwa mashabiki wa timu ...

Read More »

Baba Mzazi wa Michael Jackson Amefariki

Baba mzazi wa Micheal Jackson, Joe Jackson amefariki dunia jioni ya jana akiwa na umri wa miaka 89 alikuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa saratani. Ikumbukwe June 25 ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka mitano ya kifo cha mtoto wake Michael Jackson.

Read More »

Maskini Akwilina: Ndiyo basi? (2)

Sehemu ya kwanza ya makala hii ilitoka katika toleo na. 347. Tangu wakati huo hapakuwa na nafasi kwa makala hii na safu nyingine nyingi kutokana na nafasi zake kuwekwa hotuba za bajeti za wizara mbalimbali. Tunaomba radhi kwa usumbufu huo. Sehemu ya kwanza, mwandishi alitetea hatua ya Mwendesha Mashitaka (DPP) kufuta kesi ya mauaji iliyokuwa ikiwakabili polisi waliotuhumiwa kumuua mwanafunzi ...

Read More »

Uhusiano wa Kombe la Dunia na umeme

Kombe la soka la FIFA (Kombe la Dunia) limeanza kwa wiki zaidi ya moja sasa. Lilianza kwa kuwakutanisha wenyeji Russia dhidi ya Saudi Arabia kwenye uwanja wa Luzhniki jijini Moscow. Nimekumbuka jamaa yangu mmoja ambaye, tofauti na mimi, hana ushabiki hata kidogo wa soka. Miaka michache iliyopita nilimsikia akishangaa wenzake wakizungumzia kwa hamasa kubwa wachezaji wa timu mashuhuri za Ulaya. ...

Read More »

Ndugu Rais ‘National Breakfast Prayer’ itufunze

Ndugu Rais ni kweli kwamba ukiwa mkweli sana unaweza ukafika mahali ukasema, bora baba yangu angekuwa ni huyu mzee jirani yetu kuliko huyu baba niliyenaye! Kuna baba wengine ni kero kwa watoto wao. Na wengine kama mkosi! Tunaziona nyumba nyingi na kina baba tofauti tofauti. Utakuta baba wengine ni walevi wa kupindukia. Wengine wamepagawa kwa michepuko huku wengine kwenye uzezeta ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons