Serikali itengeneze matajiri wapya
Na Deodatus Balile, Mtwara Leo naandika makala hii nikiwa mjini Mtwara. Nimefika Mtwara Ijumaa asubuhi. Ni mwaka wa tatu sasa tangu nimetoka Mtwara. Naikumbuka Mtwara ya mwaka 2015, taarifa za ugunduzi wa gesi zilipoenea kila kona. Nakumbuka magari makubwa niliyokuwa nakutana nayo katikati ya mji wa Mtwara na ghafla mji ulivyobadilika ukawa kama Dar es…