Daily Archives: July 10, 2018

Maandiko ya Mwalimu Nyerere: Ujamaa Sehemu ya 3

Leo Tanganyika ni nchi masikini. Hali ya maisha ya umma iko chini kiasi cha kuaibisha. Lakini kama kila mtu katika nchi, mke kwa mume, atatambua hayo na kufanya kazi ukomo wa nguvu zake, kwa faida ya nchi nzima, basi Tanganyika itaendelea; na maendeleo hayo kila mtu atayapata. Lakini mafanikio haya lazima yagawanywe kwa watu wote. Mtu mwenye kuamini Ujamaa kikwelikweli ...

Read More »

Asante sana Lukuvi, wengine wakuige

Wahenga walisema: “Tenda wema nenda zako.” Wahaya na Wanyambo wanasema: “Ekigambo kilungi kigambwa.” Nao Wahehe wanasema: “Uwema kigendelo” au “Utende wema ubitage”; na kadhalika. Sasa ni miezi minne tangu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (pichani), alipofanya ziara ya kihistoria katika wilaya za Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera. Lakini kazi na shughuli alizozifanya huko kwa siku ...

Read More »

Kortini kwa ‘kula’ fedha za Uchaguzi Mkuu

Maofisa wa halmashauri za wilaya nchini waliosimamia Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015 wameanza kuchunguzwa kwa matumizi mabaya ya fedha. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema baadhi yao wamekwisha kufunguliwa mashitaka wakituhumiwa kuandaa nyaraka za uongo kuficha upotevu wa mamilioni ya shilingi. Miongoni mwao ni aliyekuwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Mwanga, mkoani ...

Read More »

Mtoto wa miaka miwili afariki baada ya kujipiga risasi Texas, Marekani

MAREKANI : Mtoto wa umri wa miaka miwili nchini Marekani amefariki baada ya kujipiga risasi kichwani kwa bunduki ambayo imekuwa ikihifadhiwa na wazazi wake nyumbani kwao. Polisi wa Houston, Texas wanasema wazazi wa mtoto huyo – Christopher Williams Jr – walikuwa nyumbani wakati wa kutokea kwa kisa hicho. Polisi wanasema bunduki hiyo ambayo hutumia risasi za ukubwa wa 9mm ilipatikana ...

Read More »

Tume anayoitaka Mke wa Bilionea Erasto Msuya iundwe

Upande wa Mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (41), umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa jalada la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) analifanyia kazi. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa. Wakili Mwita amedai kuwa ...

Read More »

Maharamia watamba Rorya

Wizara ya Fedha imeombwa ipeleke boti wilayani Rorya, Mara ili kukabiliana na maharamia katika Ziwa Victoria. Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Simon Chacha, amesema matukio ya uvuvi haramu na biashara ya magendo vinashamiri Ziwa Victoria upande wa Rorya kutokana na kukosekana kwa boti ya doria. Amesema maharamia wakiwamo wanaotoka nchi jirani, hupora nyavu, samaki, mafuta na hata boti za wavuvi ...

Read More »

Sunny Safaris waishi kwa bahshishi

Wafanyakazi 23 wa Kampuni ya Utalii ya Sunny Safaris ya jijini Arusha, wamelalamikia uongozi wa kampuni hiyo kwa kufanya kazi bila mikataba na kunyimwa mishahara kwa miaka miwili. Wanadai kuwa uongozi wa kampuni hiyo umekuwa ukiwafanyisha kazi kwa saa nyingi bila malipo ya ziada, huku wakiendelea kukosa mishahara kwa madai kuwa kampuni haina fedha. Wafanyakazi hao ni madereva wanaoongoza watalii ...

Read More »

Kilichomponza tajiri Zakaria

Mfanyabiashara Peter Zakaria (58), amerejesha mali zote alizonunua kutoka Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza (NCU), akiamini kwa kufanya hivyo ataondoa ‘nuksi’ ya kuandamwa na Serikali. Tajiri huyo mkazi wa Tarime mkoani Mara, anayemiliki vitegauchumi mbalimbali yakiwamo mabasi ya Zakaria, amekabidhi nyaraka za umiliki wa mali hizo serikalini, wiki iliyopita. Zakaria anashikiliwa rumande akituhumiwa kuwajeruhi kwa risasi maofisa usalama wawili waliomfuata ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons