Daily Archives: August 7, 2018

YANGA YAENDELEA KUJIFUA MOROGORO KWA AJILI YA WARABU

Kikosi cha Yanga kipo mjini Morogoro kikiendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger. Yanga itashuka dimbani Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Agosti 19 2018 kumenyana na Alger kutoka Alger wakiwa na kumbukumbu mbaya katika mechi ya mkondo wa kwanza. Yanga iliruhusu mabao manne kwa sufuri huko Algiers, Algeria na mpaka ...

Read More »

KATIBU WA ZAMANI WA TFF ANUSURIKA AJALI YA GARI DAR

Mwanahabari mwandamizi na katibu mkuu wa zamani wa TFF, Angetile Osiah amenusurika kifo katika ajali mbaya ya gari, jana. Osiah alipata ajali mbaya baada ya gari lake kugonga roli akiwa njiani kwenda nyumbani kwake Chanika jijini Dar es Salaam. Akizungumza na SALEHJEMBE, Angetile ambaye mmoja wa waandishi na wahariri bora wa habari za michezo nchini alisema alikuwa njiani kurejea nyumbani. ...

Read More »

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wataalamu wa afya wilayani humo kutoa elimu ya njia sahihi za kunyonyesha watoto.

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wataalamu wa afya wilayani humo kutoa elimu ya njia sahihi za kunyonyesha watoto. Amesema elimu hiyo itawawezesha kinamama kupata kizazi chenye afya bora na kushiriki vyema masuala ya uchumi na kijamii kwa siku zijazo. Ameyasema hayo leo Agosti 7 muda mfupi mara baada ya kufunga maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji watoto duniani ...

Read More »

TCRA yawaburuza 13 kortini

Mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imewafikisha mahakamani watu 13 wakikabiliwa na mashtaka matano ikiwamo ya kusambaza taarifa za uongo, uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha wa zaidi ya Sh154 milioni. Wakili wa Serikali Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Tumain Kweka amewasomea kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 58 ya 2018 leo Agosti 7mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin ...

Read More »

JULIUS KALANGA AWAVULUGA CCM MONDULI

Wanachama wa CCM wilaya ya Monduli wameandamana kwenye ofisi za chama hicho wakitaka Mbunge wa CHADEMA Julius Kalanga aliyejiunga na chama hicho kufuata utaratibu ikiwemo hatua za uteuzi wa nafasi ya kugombania ubunge. Wakizungumza katika ofisi hizo wamesema wamesikia taarifa za kuteuliwa kwake bila kufuata utaratibu ikiwemo kukaa vikao na wazee wa kimila Malaigwanani ili waweze kumpitisha. Mwenyekiti wa CCM ...

Read More »

BASATA LAKANUSHA KUUFUNGIA WIMBOA WA PARAPANDA YA ROSTAM

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limesema halijaufungia wimbo wa Parapanda ulioimbwa na wasanii wa kundi la Rostam, Roma Mkatoliki na Stamina na kusema kuwa labda wameamua kujifungia wenyewe kwa lengo la kutafuta ‘kiki’. Kauli hiyo inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Roma kupitia ukurasa wake wa Instagram kuandika maneno ya kuilaumu Basata kwamba inaua vipaji na ubunifu wa ...

Read More »

SALUM MWALIMU : MILANGO IPO WAZI KWA WABUNGE NA MADIWANI WANAOHAMA CHADEMA

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu, amesema milango ipo wazi kwa wabunge na madiwani wa chama hicho wanaokubali kurubuniwa na kukikimbia chama. Alisema wabunge na madiwani hao hawana dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi, hivyo wanaweza kwenda wanakorubuniwa. Alisema hayo mwishoni mwa wiki mjini hapa wakati akiwahutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani ...

Read More »

SIMBA YAANZISHA GAZETI LAKE

Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kuanzisha gazeti lake ambalo litatambulishwa kesho katika tamasha la Simba Day. Hatua hiyo imekuja mara baada ya uongozi huo kueleza kumekuwa na magazeti baadhi mtaani yamekuwa yakitumia jina la Simba na kujipatia faida ambayo ilipaswa kuwa inaenda klabuni. Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema gazeti hilo litakuwa linaitwa SIMBA NGUVU ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons