Serikali Yaondoa zuio la Kuuza Mazao Nje ya Nchi
Serikali imeondoa zuio la kuuza mazao nje ya nchi ili kutoa fursa soko na mapato kwa wakulima. Hata hivyo, wanaotaka kuuza mazao nje ya nchi watalazimika kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo. Uamuzi huo umetangazwa leo Agosti 8 na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alipokuwa akiyafunga rasmi maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi…