Mahakama yamuachia huru mbunge Haonga
Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, Songwe imemuachia huru mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga na wenzake wawili baada ya kukutwa hawana hatia katika kesi iliyokuwa ikiwakabili. Haonga na wenzake, Wilfredy Mwalusamba (katibu wake) na Mashaka Mwampashi wameachiwa huru leo mchana Ijumaa Agosti 10, 2018. Walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matatu ya kufanya fujo na kuvuruga mkutano…