Daily Archives: September 1, 2018

MIAKA 54 YA JWTZ: JENERALI MABEYO, MAKONDA WAFANYA USAFI

MKUU wa Majeshi yaUlinzi nchini (JWT), Venance Salvatory Mabeyo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wameongoza maadhimisho ya mwaka wa 54 tangu kuundwa kwa jeshi hilo, kwa kufanya usafi jijini Dar es Salaam. Mabeyo na Makonda mapema leo wamefanya usafi katika eneo la Kambi ya JWTZ eno la Lugalo jijini Dar es Salam sambamba na viongozi ...

Read More »

LIVERPOOL YAZIDI KUFANYA MAAJABU EPL, YAITWANGA LEICESTER 2-1

Kikosi cha Liverpool kimeendelea kuonesha dhamira ya kukirejesha kikombe cha Ligi Kuu England kwa kuicharaza Leicester City mabao 2-1 ikiwa kwao. Mabao ya Liverpool yamepachikwa kimiani na Sadio Mane mnamo dakika ya 10 pamoja na Robert Firmino katika dakika ya 45. Bao pekee la Leicester limewekwa nyavuni na Rachid Gezzal kwenye dakika ya 63 na likiwa la kwanza kwa kipia ...

Read More »

Bobi Wine: Aruhusiwa kuelekea Marekani kwa matibabu

Mbunge wa Uganda anayedaiwa kupigwa na wanajeshi ameruhusiwa kuondoka nchini humo , kulingana na maafisa wa polisi Hatua hiyo inajiri kufuatia madai kwamba mbunge huyo alipigwa mara kadhaa akiwa katika kizuizi cha jeshi, madai ambayo yamekataliwa na jeshi. Yeye na wanasiasa 32 wa upinzani walishtakiwa na shtaka la uhaini wiki iliopita kufautia madai ya kuupiga mawe msafara wa rais Yoweri ...

Read More »

Mwanafunzi aliyezirai kwa kipigo, aruhusiwa kutoka hospitali

Mwanafunzi wa sekondari ya Kalangalala mkoani Geita, Jonathan Mkono anayedaiwa kupigwa na mwalimu wake na kulazwa hospitalini, ameruhusiwa leo mchana Septemba Mosi, 2018. Mkono alikuwa amelazwa hospitali tangu Agosti 30 baada ya kuchapwa na kupoteza fahamu na mwalimu wa nidhamu, Lawson Lechipya kwa kosa la kukutwa bwenini wakati wa vipindi jambo lililosababisha maumivu makali mwilini. Akizungumza na waandishi wa habari ...

Read More »

  Serikali imesema iko tayari kutangaza katika Gazeti la Serikali msitu wa Mwalimu Nyerere uliopo Butiama Mkoani Mara kama eneo lindwa kimazingira, kufuatia ahadi iliyotolewa mwaka jana wakati wa kilele cha Siku ya Mazingira Duniani iliyofanyika Butiama Mkoani Mara. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba mara baada ya kutembelea ...

Read More »

Meya mwita ataka Kiswahili kufundishia sekondari, vyuo

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita ameishauri serikali kuanza kutumia lugha ya Kiswahili katika kufundisha masomo ya shule za msingi, sekondari na vyuo ili kuwawezesha wanafunzi kupata uelewa. Kauli hiyo ameitoa jana jijini Dar es salaam alipokuwa akizindua mashindano ya ya mashaiiri ya Meya wa jiji yaliyodhaminiwa na kampuni ya mabati ya Alaf. Alisema ni vyema kama ...

Read More »

Mkenya Kipruto ashinda mbio za mita 3000 baada ya kupoteza kiatu

Mwanariadha wa Kenyan Conseslus Kipruto alikaidi pigo la kupoiteza kiatu mapema ili kuibuka mshindi wa mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji katika ligi ya almasi ya IAAF Diamond League mjini Zurich, nchini Switzerland. Baada ya kupiga kona moja ya uwanja kiatu chake cha kushoto kilitoka lakini hilo halikumzuia . ” Ilikuwa kisirani .Lakini nilipata motisha ya kupigana zaidi ...

Read More »

Watanzania 27 wasio na vibali wakamatwa Mombasa nchini Kenya

Watanzania 27 wamekamatwa mjini Mombasa Kenya baada ya kuingia nchini humo bila vibali maalum. Mamlaka ya usalama huko Mombasa inaendelea na mipango ya kuwarejesha nchini kwao. Baadhi ya watu hao wameshikiliwa na polisi katika kituo cha Likoni wakati wakisubiri kurejeshwa nyumbani. Kamanda wa polisi wa Mombasa Johston Ipara ameeleza kwamba Watanzania hao ni miongoni mwa wahamiaji wengine kutoka Congo, Somalia, ...

Read More »

16 WANAODAIWA KUKWAPUA FEDHA ZA USHIRIKA WILAYANI HAI ,WAWEKWA NDANI KWA AMRI YA DC SABAYA

WATU 16 wakiwemo viongozi wa Bodi ya Ushirika wa Umoja wa watumia maji katika kijiji cha Mijongweni (UWAMI) wanashikiliwa na Jeshi la  Polisi kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya  wakituhumiwa kuhusika na ubadhilifu wa fedha za mradi zaidi ya Sh Mil 200. Mbali na Viongozi wa Bodi ya ushirika huo wakiongozwa na Mwenyekiti wake ,Nuru Ndoma ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons