Monthly Archives: November 2018

Bomu la mafao

Kuna dalili za kukwama kwa kanuni mpya za ukokotoaji wa mafao ya wastaafu zilizotangazwa na serikali. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo imewatoa hofu wananchi kuhusu kanuni hizo ikisema inazisubiri zipelekwe bungeni hata kama zimekwisha kuanza kutumika. Kanuni zilizotangazwa hivi karibuni zinamfanya mstaafu kulipwa asilimia 25 ya mafao yake baada ya ukomo wa ajira. Kiasi kinachobaki cha asilimia ...

Read More »

GMO yafyekelewa mbali

Wananchi wadau wa kilimo wameupokea kwa shangwe na nderemo uamuzi wa serikali wa kupiga marufuku majaribio ya uhandisijeni yanayofanyika kwenye vituo vya utafiti nchini. Novemba 21, mwaka huu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe, aliiagiza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kusitisha mara moja utafiti huo nchini kote.  Uhandisijeni, yaani Genetic Modified Organism (GMO), ni utafiti ...

Read More »

Watua nchini Uingereza kupinga uhifadhi Loliondo

Ujumbe wa watu watano kutoka Loliondo, Tanzania na nchini Kenya, upo nchini Uingereza kuchangisha fedha za kuendesha harakati za kupinga mpango wa serikali wa kutenga eneo la hifadhi ndani ya Pori Tengefu la Lolindo. Hivi karibuni Gazeti la JAMHURI liliandika kuhusu safari ya Watanzania kadhaa nchini Uingereza wakilenga kupata fedha za kuendeshea harakati za kupinga mpango huo wa uhifadhi. Watu ...

Read More »

Wakili wa Serikali adaiwa ni Mkenya

Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Wakili Mfawidhi Kanda ya Moshi, Omari Kibwana, anadaiwa kuwa si raia wa Tanzania kwa kuzaliwa. Kwa tuhuma hizo, Idara ya Uhamiaji mkoani Kilimanjaro imefungua jalada la uchunguzi ili kubaini ukweli. Kibwana ambaye amekuwa wakili wa serikali kwa muda mrefu, anatuhumiwa kuwa ni Mkenya kwa kuzaliwa na hajawahi kuukana uraia wa nchi hiyo. Mkuu wa ...

Read More »

Hongera Wizara ya Kilimo, hongereni wapambanaji

Wizara ya Kilimo imezuia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) iliyopo Makutupora, Dodoma kuendelea na utafiti wa mbegu za GMO. Uamuzi huo ni majibu kwa kilio cha wazalendo waliojitokeza kupaza sauti kuhoji uhalali wa chepuo linalopigwa ili kuruhusu mbegu hizo kuanza kutumika nchini. Wasomi, wakulima na watu wa kada mbalimbali wamejitokeza kueleza kisayansi madhara ya mbegu za GMO yakiwamo magonjwa ...

Read More »

Watu watanifikiriaje, inakuchelewesha

Kama kuna neno ambalo limewafanya watu wabaki palepale walipo miaka nenda – rudi ni neno: “Watu watanifikiriaje au watu watasemaje.” Watu wengi wana ndoto kubwa, maono makubwa, mawazo makubwa ya kuibadili dunia na vipaji vingi, lakini wanafikiria watu wengine watawafikiriaje na watasemaje kwa wanachokifanya. Hakuna mtu yeyote aliyefanikiwa na kufikia hatua kubwa kwa kufikiria watu wengine watamfikiriaje au watasemaje kwa ...

Read More »

Miundombinu, umeme uko njia sahihi

Leo nimeamua kusitisha makala ya Raila Odinga na urais wa Kenya ili nami kidogo nishiriki kujadili na kuichambua miaka mitatu ya Rais John Magufuli. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli iingie madarakani, yametokea mambo mazuri kadhaa. Binafsi nitajikita katika machache, ambayo yote yanaangukia katika ujenzi wa miundombinu. Naanza na umeme. Umeme ndio msingi wa maendeleo kwa ...

Read More »

Sababu zinazochangia tumbo kujaa

Ni hali ambayo mara nyingi mtu huhisi tumbo lake limejaa wakati wote. Kila mmoja amewahi kupata hali hii mara kadhaa kwa nyakati tofauti. Japo ni hali ambayo kwa kawaida hutokana na ulaji kupita kiasi, lakini kuna baadhi pia hawana tabia ya kula kupita kiasi lakini bado wanakutana na hali hii ya kuhisi matumbo yao yamejaa wakati wote. Hivyo, ni vema ...

Read More »

Bravo: Rais Magufuli (1)

Alhamis, Novemba mosi, 2018 inastahili kuwa siku ya kukumbukwa kutokana na lile tukio la Rais John Magufuli kushiriki kikamilifu mdahalo muhimu pale Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Mlimani), katika ukumbi wa Nkrumah. Nafikiri, mkuu wa nchi alijisikia yuko nyumbani kabisa, maana alitulia tulii na kuwasikiliza wasomi, maprofesa na watu wengine mashuhuri wakitoa “materials” zao pale. Kwa maneno yake mwenyewe ...

Read More »

Ndugu Rais tuonyeshe njia ya kwenda Canaan

Ndugu Rais, imeandikwa; wacha tukuchezee Bwana kwa matendo yako makuu. Wacha tukutukuze Bwana kwa ukuu wako! Mbingu na nchi zinatangaza ukuu wako Bwana, milima nayo yapendeza yamtukuza Yeye. Alipo Wewe Bwana utukufu unashuka! Canaan mji ule! Mji wa divai iliyo njema. Alitutahadharisha mapema kiongozi wetu kuwa mtakapofika Canaan mtakaribishwa kwa divai aina kwa aina, lakini msionje zote kwa maana mnaweza ...

Read More »

Maisha bila maadui hayana maana (3)

Mhubiri wa Injili, Israel Ayivor, alipata kusema kwamba yule aliyekusaidia kuzungumza mambo mabaya kuhusu mwenzako ndiye atakayemsaidia mtu mwingine kuzungumza uovu juu yako. Wema ni akiba. Tenda wema uende zako, usisubiri malipo. Kumbuka kwamba watu uliowatendea mema wanaweza kukugeuka lakini Mwenyezi Mungu hawezi kukugeuka. Mtu aliyekuwa sababu ya furaha yako anaweza kuwa sababu ya majonzi yako, lakini kumbuka Mungu ndiye ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (5)

Umri wa kati ni mtihani. Huu ni umri kati ya miaka 35 hadi 59. Ni umri kati ya ujana na uzee. Ni umri ambao mtu anaingia katika kipindi cha pili cha mchezo wa maisha. “Katika umri wa kati moyo hauna budi kufunguka kama ua la waridi na si kufunga kama kabeji,” alisema John A. Homes. Kwa wanandoa ni kipindi ambacho ...

Read More »

Pongezi kwa Serikali kupiga ‘stop; GMO

Juma lililopita tumesikia taarifa za kutisha kwamba wabunge wametembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) iliyopo Makutupora, Dodoma na kuridhishwa na matokeo ya utafiti wa mbegu za GMO, mbegu zinazoundwa kwenye maabara. Zilifuatiwa na habari kwamba serikali imesimamisha mara moja utafiti wote unaofanywa na TARI na kuagiza kuteketezwa kwa mazao yote yaliyokuwa yakitumika kwa sababu TARI ilitangaza matokeo ya utafiti ...

Read More »

Namna ya kuzuia ukazaji/utekelezaji wa hukumu

1. Ukazaji wa hukumu ni nini? Ukazaji wa hukumu ni hatua inayochukuliwa na mtu aliyeshinda kesi/shauri kwa kuiomba mahakama kumlazimisha mtu aliyeshindwa katika kesi/shauri kufanya au kutekeleza kile ilichoamua dhidi yake/mshindwa. Kawaida mtu akishindwa kesi/shauri mahakama huwa inatoa maagizo mbalimbali, mathalani agizo la kulipa fedha, agizo la kurudisha nyumba au mali fulani, agizo la kubomoa, agizo la kuondoka katika pango ...

Read More »

Subira ina heri, hila ina shari 

Mwanambuzi alikwenda mtoni kunywa maji. Akiwa anakunywa maji, alitokea mbwamwitu naye alikwenda kunywa maji. Mbwamwitu alisimama hatua chache kutoka aliposimama mwanambuzi.  Mbwamwitu alitamani sana kumla mwanambuzi. Alifikiri mbinu za kumkamata asimkimbie. Wakati anafikiri hivyo, mwanambuzi alikwisha kubaini janja ya mbwamwitu. Alijiweka tayari kumkwepa na kumkimbia.  Mara mbwamwitu akanena: “Wee mtoto mbona hauna adabu? Unatibua maji wakati nakunywa.” Mwanambuzi akajibu: “Mzee ...

Read More »

Yah: Maisha ya leo ndiyo tunayohitaji

Nianze na salamu za makabila ya huku kwetu Kusini kwenye mafanikio ya kununua korosho kwa mkupuo, tena bila mizengwe ya kuzungushana wala kupangiwa bei tofauti. Kuna salamu ambayo nadhani nikiitumia wengi wataielewa kwamba yajayo yanafurahisha, msishangae kutuona mjini kuja kufanya ‘shopingi’ ya vitu vya maana kama magari na mabati mazuri. Sisi ndio wakulima wa korosho ambao tumesemewa mengi na wakubwa ...

Read More »

Tumkumbuke nguli Shakila Binti Said (1)

Ni zaidi ya miaka miwili tangu atutoke Shakila Binti Said aliyekuwa nguli katika miondoko ya muziki wa taarabu humu nchini na Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla. Wakati wa uhai wake, aliweza kuonyesha umahiri wake wa utunzi na uimbaji wa taarabu katika bendi zote alizowahi kuzitumikia. Shakila alifariki dunia ghafla, ambapo binti yake wa mwisho aitwaye Shani, alisikika kupitia vyombo mbalimbali ...

Read More »

Nani kuibuka mchezaji bora Afrika?

Wachezaji watano wamependekezwa kuwania tuzo ya BBC ya Mchezaji Bora wa soka barani Afrika mwaka 2018. Wachezaji wote wanacheza soka la kulipwa barani Ulaya. Wachezaji walioorodheshwa mwaka huu ni Medhi Benatia (Morocco), Kalidou Koulibaly (Senegal), Sadio Mane (Senegal), Thomas Partey (Ghana) na Mohamed Salah (Misri). Upigaji kura ulianza rasmi Novemba 17, saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki na ...

Read More »

‘Balozi’ Alphayo Kidata kufikishwa mahakamani

Kuna kila dalili kuwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, Alphayo Kidata, atafikisha mahakamani Kisutu muda wowote kuanzia sasa kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka wakati akiwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Kidata aliapishwa Mei 10, mwaka huu kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, alikokwenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Balozi ...

Read More »

Mchati: Mti wa thamani unaotoweka Mafia

Licha ya ukweli kuwa uoto wa asili wa Kisiwa cha Mafia unafanana kwa kiasi kikubwa na uoto wa asili wa visiwa jirani vya Pemba na Unguja na maeneo ya Bara yaliyopo jirani kama Kisiju na Rufiji, watafiti Rogers na Greenaway (1988) waliokuwa wakidurusu uoto wa Kisiwa cha Mafia walishangazwa mno na kiwango kikubwa cha upekee (endemism) wa mimea ya kisiwa ...

Read More »

Benki Kuu yaichunguza BOA

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeanza kuichunguza Benki ya BOA ambayo Gazeti la JAMHURI limeandika kwa wiki mbili mfululizo kuelezea jinsi inavyochezea dhamana za wateja, JAMHURI limeelezwa. Wateja wengi wa BOA wamejitokeza na malalamiko ya aina mbalimbali dhidi ya benki hii yenye kuonyesha ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Benki na Maduka ya Fedha ya Mwaka 2006, ikiwamo kuwaongezea wateja riba ...

Read More »

Amri ya DC Moshi yamchefua Askofu, wananchi Vunjo

Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, amepinga amri ya Mkuu wa Wilaya (DC) ya Moshi, Kippi Warioba, kuzuia ujenzi wa barabara vijijini katika Jimbo la Vunjo. Barabara hizo zinajengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo Vunjo (VDF). Askofu Shao ambaye ni Mwenyekiti wa VDF, amewambia waandishi ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons