Daily Archives: November 6, 2018

Benki yaibia wateja

Maofisa wa Bank of Africa (BOA) jijini Dar es Salaam wanadaiwa kughushi hati ya ardhi Na. 55709, Kitalu ‘C’, Ukonga Stakishari ya Jimmy Mwalugelo (68), mkazi wa eneo hilo na kuitumia kumkopesha mtu mwingine Sh milioni 500. Hati hiyo iliyoghushiwa na maofisa wa BOA inajumuisha viwanja namba 660/1, 662/1, 696/1 na 698/1 na viwanja namba 665 na 666 ambavyo havipo ...

Read More »

Polisi aiba, aumbuliwa

Askari Polisi wa Wilaya ya Kinondoni amefanya uporaji kwenye ofisi za kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam. Oktoba 3, mwaka huu saa tatu usiku, askari aliyefahamika kwa jina moja tu la Shuka, akiwa na wenzake wawili walifika kituo cha mabasi Ubungo na kuwakamata wafanyakazi wa kampuni tatu za mabasi kisha kuwaweka chini ya ulinzi katika ...

Read More »

Microchip yageuka gumzo Kenya

Baada ya Gazeti la JAMHURI kuchapisha taarifa kuwa mfanyabiashara, Mohamed Dewji, maarufu kama ‘Mo’ alikuwa na microchip mwilini iliyorekodi taarifa zote za watekaji, matajiri na wafanyabiashara nchini Kenya wameanza juhudi za kuwekewa teknolojia hiyo, JAMHURI limefahamishwa. Wengi wa matajiri wameona teknolojia ya microchip itasaidia kuongeza usalama wa maisha yao, hasa wamevutiwa baada ya kubaini kuwa teknolojia hiyo inatumika mno huko ...

Read More »

Hongera RC Mtaka

Mkuu wa Mkoa (RC) wa Simiyu, Anthony Mtaka, ametoa msimamo wa namna alivyodhamiria kuubadilisha mkoa huo ili uendane na ‘Tanzania ya Viwanda.’ Kabla na baada ya kusifiwa na Rais John Magufuli, aliyemtaja kama RC bora nchini, Mtaka ameendelea kuonyesha maono makubwa ya uongozi. Amezidi kuibua miongozo mbalimbali ya kiuongozi ambayo kwa kweli imekuwa nadra kuipata kutoka kwa viongozi wengi nchini. ...

Read More »

Kamati ya Bunge itimize wajibu

Wiki hii Bunge la 11 linakutana jijini Dodoma kwa ajili ya kuendelea na vikao vyake kama ilivyo ada. Pamoja na changamoto za hapa na pale katika maisha ya Mtanzania, naamini bado Watanzania wanayo imani na Bunge hili. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ni kamati yenye jukumu kubwa nchini. Jukumu lake hasa ni kuhakikisha nchi na watu ...

Read More »

Kiongozi wa upinzani afungwa jela maisha

Kiongozi wa upinzani nchini Bahrain, Sheikh Ali Salman, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya mahakama ya rufaa kumkuta na hatia ya kuipeleleza nchi hiyo kwa niaba ya nchi ya Qatar. Hukumu hiyo inakuja miezi michache baada ya mahakama ya juu nchini Bahrain kumuondolea mashtaka Salman kwa kushirikiana na taifa hasimu. Nchi ya Bahrain ilisitisha uhusiano wake na nchi ya ...

Read More »

Raila Odinga anakuwa Rais Kenya (5)

Wiki iliyopita tuliishia katika eneo linaloonyesha kuwa nchini Tanzania hakuna chama kinachoweza kuunda muungano na kikasimamisha mgombea kama walivyotaka wanasiasa wa upinzani mwaka 2015 kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Kwa Kenya, hili linawezekana. Wamelifanya mara kadhaa na limekuwa na matokeo ya aina yake. Endelea… Wenzetu kule Kenya wana kitu kinaitwa sympathy vote, yaani kura za huruma. Ni huruma ileile ...

Read More »

Je, maumivu ya titi ni saratani?

Nakukumbusha tu msomaji wa safu hii kuwa mwezi Oktoba huadhimishwa kwa kuinua uelewa kuhusu saratani ya titi. Hii ni kutokana na kalenda ya magonjwa ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya afya (WHO) kwa lengo la si tu kuinua uelewa, bali kuongeza mapambano dhidi ya saratani ya titi, saratani ambayo huanzia kwenye tishu za titi. Saratani ya titi imekuwa ...

Read More »

Ndugu Rais tunyooshe kwa upendo, tutanyooka tu

Ndugu Rais, watu wako wamekusikia vema kwa yote uliyoyasema Novemba Mosi, 2018 katika kongamano la siasa na uchumi lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika ukumbi wa Nkrumah. Wamekusikiliza tangu ulivyoanza mpaka ulivyomaliza. Sitaki nikufananishe na mtu yeyote, lakini ulinikumbusha ile hotuba kuu aliyoitoa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika ukumbi wa Simba pale ilipokuwa ikiitwa The ...

Read More »

Wanangu tunahitaji ushindi – Lesotho

“Wanangu nendeni mkashinde, nendeni mkapeperushe vizuri bendera ya Tanzania, lengo letu iwe ni kushinda tu.” Ni nasaha iliyotolewa na Rais Dk. John Magufuli alipokutana na kuzungumza na wachezaji wa Taifa Stars wiki mbili zilizopita Ikulu, jijini Dar es Salaam.  Ni nasaha iliyobeba maneno matatu muhimu; kwenda, lengo na ushindi. Si kwa wachezaji tu, bali pia kwa viongozi wa Shirikisho la ...

Read More »

Yah: Hiki ni kizazi gani na tunaelekea wapi?

Kuna wakati huwa najiuliza, ni wapi ambapo tulikosea hii nchi yetu? Nchi iliyokuwa ya asali na maziwa katika uzalendo, maadili, uaminifu, utamaduni, mapenzi, upendo na mengineyo mengi tu. Najiuliza tuko wapi tulio hai mpaka leo na tunaojua ukweli wa asili ya nchi yetu iliyotukuka? Najiuliza tumefikia hapa kwa sababu gani? Kuna wakati nikiamka asubuhi naona kama dunia inakwenda kasi sana, ...

Read More »

Mkopaji kumfidia mdhamini wake mali ya mdhamini inapouzwa

Ni kawaida mali za wadhamini kuuzwa pale ambapo wale waliowadhamini wanaposhindwa kurejesha mikopo. Huwa inauma kwa sababu wakati mwingine mdhamini hakufaidika na mkopo, ila tu aliamua kumsaidia ndugu, rafiki, jamaa ili akope, asonge mbele, ila baadaye inakuja kuwa hivyo. Suala la msingi huwa ni kujua nini la kufanya hasa kama wewe ni mdhamini na hali hii imekutokea au inaelekea kukutokea. ...

Read More »

Kwenye msafara wa mamba, kenge wamo

Nawasifu sana wanaharakati kote duniani, ambao wanashikilia suala moja na kulipigania bila woga, bila kujali yatakayowakuta. Uanaharakati upo wa aina nyingi. Mtu yeyote anaweza kuwa mwanaharakati. Unaingia kwenye kundi hilo iwapo unajaribu kushawishi mabadiliko ndani ya jamii kwa madhumuni ya kuleta mageuzi kwenye siasa, mazingira, uchumi au masuala ya jamii. Kwa fasili hii, mpiga kura yeyote ni mwanaharakati kwa sababu ...

Read More »

Mkasa wa 2Pac Shakur Malaysia (2)

Tupac alilelewa katika mazingira magumu, jamii yake ilimpatia jina la ‘Black Prince’ kwa kuwa mama yake alimpenda mtoto wake. Tupac alikulia katika mazingira ya ‘kitemi’ kutokana na kushindwa kupata malezi bora, huku mama yake akishindwa kuwa karibu ili kumlea mtoto wake, ingawa alimpenda sana. Alikuwa akimsumbua sana mama yake kuhusu kumjua baba yake na mama huyo hakuwa na jibu la kuweza kumridhisha zaidi ya kumwambia ...

Read More »

Henry aizamisha Monaco?

Nahodha wa zamani wa Klabu ya Arsenal na mchezaji wa klabu za Juventus, Barcelona, Red Bulls ya New York pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry, ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa Klabu ya AS Monaco inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa. Henry ameajiriwa kwa mkataba wa miaka mitatu utakaokwisha mwaka 2021 na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Leonardo Jardim ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons