Monthly Archives: December 2018

Siri zavuja Jiji

Siri nzito za mradi wa ujenzi wa kituo kikubwa cha mabasi ya kwenda mikoani eneo la Mbezi Luis zimevuja, zikavuruga watendaji na Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam, JAMHURI linathibitisha. Baada ya wiki iliyopita gazeti hili kuandika habari za jinsi rushwa ilivyovuruga Baraza la Madiwani, uongozi wa Jiji la Dar es Salaam na watumishi wa umma, sasa ...

Read More »

Jenerali Waitara atafuta mrithi Mlima Kilimanjaro

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, Jenerali George Waitara, ametumia maadhimisho ya miaka 57 ya Uhuru kutangaza rasmi kustaafu kupanda Mlima Kilimanjaro. Waitara amekuwa akipanda mlima huo kwa kipindi cha miaka kumi mfululizo. Waitara ametangaza azima hiyo wakati wa mkutano wake na wanahabari, mkutano huo aliufanya katika kituo cha Mandara muda mfupi kabla ya kuagana na timu ya wapanda mlima ...

Read More »

Asanteni wasomaji wetu

Wiki iliyopita, yaani Desemba 6, 2018 Gazeti la JAMHURI limetimiza miaka saba sokoni. Sasa tumeanza mwaka wa nane. Katika kipindi chote hicho cha miaka saba hatujawahi kushindwa kwenda sokoni. Tumechapisha kwa ukamilifu matoleo yote 52 kila mwaka na ya ziada tulipopata matoleo maalumu. Ndiyo maana toleo la leo ni la 376. Katika maoni yetu ya Desemba 6, 2011 tulipotoa nakala ...

Read More »

Maeneo matatu pesa ilikojificha (1)

Pesa imejificha katika maeneo makuu matatu. Sehemu ya kwanza pesa ilikojificha ni katika uhitaji.Biashara yoyote kubwa yenye mafanikio ni biashara inayotoa suluhu kwa mahitaji yanayohitajika katika jamii. Ukiweza kutatua uhitaji wa watu kwenye jamii yako au kutatua matatizo ya watu kwenye jamii yako pesa itakufuata. Tatizo la watu wengi wanaoanzisha biashara zinazokufa kila kukicha ni kwa sababu hawatoi majibu ya ...

Read More »

Padri Kitunda amenigusa, tujenge uzalendo

Najua baadhi ya wasomaji wangu wanapenda kila wakati tuandike siasa, uchumi na mambo mengine ya kijamii. Leo naomba mniruhusu nichepuke kidogo. Kuna kitu kimenigusa katika ibada niliyohudhuria Jumapili iliyopita katika Parokia yetu ya Roho Mtakatifu ya Kitunda. Paroko Msaidizi, Paul Njoka, alitutaka kanisani tufurahie siku ya Uhuru kwa kuimba nyimbo za uzalendo. Sitanii, amefafanua kwa kina umuhimu wa nyimbo hizi ...

Read More »

Ndugu Rais naiona kesho yangu

Ndugu Rais, naiona kesho yetu iliyopangwa na Baba. Kesho ya heshima iliyopangwa na Baba. Kesho ya neema, kesho yetu ya ushindi liyopangwa na Mungu. Sitaki kuitazama leo yetu. Leo yetu ni ya shida. Kuna majira hufika mambo yakawa magumu. Hata tukisukwasukwa vipi kamwe tusimuache Baba kwa kuwa kasema tuione kesho yetu aliyotuwekea. Hata kwa macho ya nyama tu utaona ni ...

Read More »

Watanzania tusiwe kama Thomaso

Desemba 9, 2018 imeangukia siku ya Dominika, ni siku ya Bwana, sisi Watanganyika tumefanya kumbukumbu ya mwaka wa 57 wa Uhuru wa taifa letu. Ni fahari kubwa sana kwa sisi sote kukumbuka Desemba 9, mwaka ule wa 1961 tuliojikomboa kutoka mikononi mwa wakoloni Waingereza. Kwa wazee kama Mhesheshimiwa Balozi Job Lusinde kule Dodoma, nafikiri inakuwa siku ya kumbukumbu ya namna ...

Read More »

Namna ya kuishinda hasira yako (2)

Hasira hupunguza furaha katika maisha Hasira iko tofauti na upendo, hasira iko tofauti na furaha, hasira iko tofauti na msamaha. Hasira iko tofauti na huruma, hasira iko tofauti na amani. Ndugu wa hasira anajulikana, ndugu huyo ni hasara. Kila mmoja anaifahamu hasira, kila mmoja anafahamu ule msemo wa ‘Hasira ni hasara’. Katika ndoa unaweza kuitwa baba upendo au baba hasira au ...

Read More »

Wanyama wanamalizwa Loliondo

Hadi naandika makala hii, mizogo ya tembo wanane imeonekana katika Kijiji cha Maaloni, Arash, Ngorongoro mkoani Arusha. Miezi miwili, katika Kitongoji cha Karkamoru, Loliondo pekee twiga wanane wameuawa. Watuhumiwa wa ujangili wamekwisha kukamatwa, japo kuna taarifa kuwa wahusika wenyewe bado wamo mitaani. Mauaji hayo ya twiga ni tofauti na haya ya tembo. Tembo wanakufa kwa namna inayotia shaka. Mizoga hii ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (7)

Ujana ni mtihani. Ujana ni kama mtindo unapita haraka. Ujana ni moshi, ukienda haurudi. Hakuna mzee yeyote ambaye ana utajiri wa kununua tena siku zake za ujana. Kipindi cha ujana ni kimoja, ingawa baadhi ya wazee wanaitwa vijana wa zamani. Umri wa uzeeni unategemea ujana. Umri wa kati unategemea ujana. Ukweli huu unabainishwa na methali ya Wahaya: “Mvi anakula vilivyolimwa ...

Read More »

Hali zinabadilika, mabadiliko ni muhimu

Desemba 13, mwaka huu itatimia miaka 27 tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliposema: “Hali zinabadilika. Tuendelee na chama kimoja cha siasa ama tuwe na vyama vingi vya siasa.” Maelezo haya aliyatamka Desemba 13, mwaka 1991 alipozungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, alipotoa maoni na msimamo wake wa kutaka tubadilike kufuatana na hali, tuwe na vyama vya ...

Read More »

Yah: Tuna vituko hadi kichekesho

Uswahili ni uungwana na hata kama jana tumeonana si vibaya leo tukajuliana hali na salamu, ukizingatia maisha ni mafupi na mtu husafiri na kifo chake, hii si busara kujua unahitaji kuangalia uzao wako na sasa mmebaki wangapi mtaani au kijijini kwenu. Usiangalie wamezaliwa wangapi, angalia mliozaliwa wote, mkacheza wote na mkasoma wote, wako wapi sasa, ndipo utakapojua kuwa kifo ni ...

Read More »

CCM, wembe ubaki ule ule

Taarifa kwamba Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, kumtaka aliyekuwa mgombea wa urais wa CCM, Bernard Member kufika ofisini kwake kujibu tuhuma za kuendesha mikakati ya “kukwamisha” juhudi za Rais John Magufuli zimepandisha kidogo joto la kisiasa, zimetawala mijadala. Kisichoelezwa wazi katika tuhuma hizo ni kuwa Membe anafanya mikakati ya kumuengua Rais Magufuli kuwa mgombea wa ...

Read More »

CAF yaiomba Afrika Kusini wenyeji AFCON

Karne ya 21 ina mambo mengi yanayogonga vichwa vya habari duniani, achana na kifo cha Rais wa 41 wa Marekani, George H.W. Bush, ambaye mazishi yake yamefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Achana na habari ya Bernard Membe na CCM yake, sahau kuhusu kipigo cha mbwa koko ambacho Simba SC wamewachapa Mbambane Swallows ya Swaziland na kuwasukuma nje ya mashindano ya ...

Read More »

Rushwa yavuruga Jiji

Rushwa imevuruga safu ya uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi Mbezi Luis, na sasa viongozi wote wanashikana uchawi, JAMHURI limebaini. Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa kiwango cha kuaminiana kati ya wabunge wanaoingia kwenye vikao vya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo ...

Read More »

Sera ya uzazi wa mpango ibadilishwe

Septemba 9, mwaka huu Rais John Magufuli alipokuwa akizungumza na wananchi akiwa Meatu mkoani Simiyu aligusia uzazi wa mpango. Baada ya kuona, kusikia na kusoma mitazamo na maoni ya watu mbalimbali juu ya hoja aliyoitoa Rais Magufuli, nimeona nami nichangie mawazo kidogo juu ya hili; na kwa kweli kukazia maarifa juu ya kile alichokisema na mtazamo wake thabiti kwa masilahi ...

Read More »

Aliyemhonga ofisa TRA ahukumiwa Moshi

Meneja wa Fedha wa kampuni za ujenzi za Dott Services (TZ) Ltd na General Nile Company for Roads and Bridges/Dott Services JV, Suresh Kakolu, amehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni moja, hivyo kukwepa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kutoa rushwa. Kakolu amekiri kumhonga Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoani Kilimanjaro, Msafiri Mbibo, dola 2,000 za Marekani ...

Read More »

Ukatili wa kijinsia waongezeka

Matukio ya ukatili wa kijinsia yanaongezeka. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema mwaka jana kulikuwa na matukio 41,000; kati ya hayo matukio 13,000 yaliwalenga watoto. Wizara inasema asilimia 27 ya wasichana wenye umri wa miaka 15 -19, ama wamejifungua au ni wajawazito. Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Faustine Ndugulile, amesema mikoa ya Mara na ...

Read More »

Hii ni aibu rushwa kukwamisha stendi

Habari tuliyoipa umuhimu wa pekee kwenye toleo hili inahusu mkwamo wa ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi ya mikoani eneo la Mbezi Luis, Dar es Salaam. Tumeeleza namna vitendo vya rushwa vinavyotishia mradi huo mkubwa kwenye sekta ya usafiri wa mabasi nchini na katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. Ni jambo la bahati mbaya kuona kuwa bado tunao baadhi ...

Read More »

Jitofautishe, fanya kitu fulani

“Kama unafikiri wewe ni mdogo kiasi cha kuleta tofauti, haujawahi kukesha usiku kucha ukiwa na mbu,” ni methali ya Kiafrika. Mbu ni viumbe wadogo sana, lakini wakati wa usiku tukiwa tumelala huwa wanafanya maajabu makubwa. Unaweza kuwa umelala na haujashusha chandarua ukafyonzwa damu na mbu mmoja, ukiamka unajikuta umevimba usoni, mikononi, miguuni na hata mwili mzima na unaweza kufikiri kulikuwa ...

Read More »

Magufuli asante kuwatumbua Dk. Tizeba, Mwijage

Nafahamu leo zimepita siku kadhaa tangu Rais John Magufuli afanye uamuzi wa kuwatumbua Waziri mwenye dhamana ya Kilimo, Dk. Charles Tizeba na huyu aliyekuwa na dhamana ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. Sijaandika lolote kuhusu kutumbuliwa kwao. Wasomaji wangu mmekuwa mkiniuliza, nina kauli gani? Nikawambia subirini. Sitanii, nakiri kwamba sina ugomvi binafsi na Dk. Tizeba au Mwijage, ila katika ...

Read More »

Zitambue dalili za sonona

Mwanamke mmoja kati ya watano, na mwanamume mmoja kati ya 10 wamewahi kupata sonona katika jamii zinazotuzunguka na kuleta matokeo hasi katika maisha yao. Takwimu hizi zinadhihirisha kuwa wanawake ndio wahanga wakubwa wa janga hili. ‘Depression’ ni neno la kisayansi ambalo kwa tafsiri ya kawaida ndipo tunapoita sonona. Huu ni ugonjwa wa akili ambao mtu anaupata baada ya kupitia matatizo ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons