Daily Archives: December 4, 2018

Rushwa yavuruga Jiji

Rushwa imevuruga safu ya uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi Mbezi Luis, na sasa viongozi wote wanashikana uchawi, JAMHURI limebaini. Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa kiwango cha kuaminiana kati ya wabunge wanaoingia kwenye vikao vya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo ...

Read More »

Sera ya uzazi wa mpango ibadilishwe

Septemba 9, mwaka huu Rais John Magufuli alipokuwa akizungumza na wananchi akiwa Meatu mkoani Simiyu aligusia uzazi wa mpango. Baada ya kuona, kusikia na kusoma mitazamo na maoni ya watu mbalimbali juu ya hoja aliyoitoa Rais Magufuli, nimeona nami nichangie mawazo kidogo juu ya hili; na kwa kweli kukazia maarifa juu ya kile alichokisema na mtazamo wake thabiti kwa masilahi ...

Read More »

Aliyemhonga ofisa TRA ahukumiwa Moshi

Meneja wa Fedha wa kampuni za ujenzi za Dott Services (TZ) Ltd na General Nile Company for Roads and Bridges/Dott Services JV, Suresh Kakolu, amehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni moja, hivyo kukwepa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kutoa rushwa. Kakolu amekiri kumhonga Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoani Kilimanjaro, Msafiri Mbibo, dola 2,000 za Marekani ...

Read More »

Ukatili wa kijinsia waongezeka

Matukio ya ukatili wa kijinsia yanaongezeka. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema mwaka jana kulikuwa na matukio 41,000; kati ya hayo matukio 13,000 yaliwalenga watoto. Wizara inasema asilimia 27 ya wasichana wenye umri wa miaka 15 -19, ama wamejifungua au ni wajawazito. Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Faustine Ndugulile, amesema mikoa ya Mara na ...

Read More »

Hii ni aibu rushwa kukwamisha stendi

Habari tuliyoipa umuhimu wa pekee kwenye toleo hili inahusu mkwamo wa ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi ya mikoani eneo la Mbezi Luis, Dar es Salaam. Tumeeleza namna vitendo vya rushwa vinavyotishia mradi huo mkubwa kwenye sekta ya usafiri wa mabasi nchini na katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. Ni jambo la bahati mbaya kuona kuwa bado tunao baadhi ...

Read More »

Jitofautishe, fanya kitu fulani

“Kama unafikiri wewe ni mdogo kiasi cha kuleta tofauti, haujawahi kukesha usiku kucha ukiwa na mbu,” ni methali ya Kiafrika. Mbu ni viumbe wadogo sana, lakini wakati wa usiku tukiwa tumelala huwa wanafanya maajabu makubwa. Unaweza kuwa umelala na haujashusha chandarua ukafyonzwa damu na mbu mmoja, ukiamka unajikuta umevimba usoni, mikononi, miguuni na hata mwili mzima na unaweza kufikiri kulikuwa ...

Read More »

Magufuli asante kuwatumbua Dk. Tizeba, Mwijage

Nafahamu leo zimepita siku kadhaa tangu Rais John Magufuli afanye uamuzi wa kuwatumbua Waziri mwenye dhamana ya Kilimo, Dk. Charles Tizeba na huyu aliyekuwa na dhamana ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. Sijaandika lolote kuhusu kutumbuliwa kwao. Wasomaji wangu mmekuwa mkiniuliza, nina kauli gani? Nikawambia subirini. Sitanii, nakiri kwamba sina ugomvi binafsi na Dk. Tizeba au Mwijage, ila katika ...

Read More »

Zitambue dalili za sonona

Mwanamke mmoja kati ya watano, na mwanamume mmoja kati ya 10 wamewahi kupata sonona katika jamii zinazotuzunguka na kuleta matokeo hasi katika maisha yao. Takwimu hizi zinadhihirisha kuwa wanawake ndio wahanga wakubwa wa janga hili. ‘Depression’ ni neno la kisayansi ambalo kwa tafsiri ya kawaida ndipo tunapoita sonona. Huu ni ugonjwa wa akili ambao mtu anaupata baada ya kupitia matatizo ...

Read More »

Bravo: Rais Magufuli (2)

Sehemu ya kwanza, mwandishi wa makala hii alieleza namna wakoloni walivyoleta elimu kwa ajili ya kuwapumbaza Waafrika na kuwafanya wapuuze asili yao. Alieleza namna mkurugenzi wa kwanza wa elimu aliyeitwa Stanley River-Smith alivyokuja mwaka 1920 na kusimamamia utekelezaji wa sera hiyi kwa Waafrika nchini Tanganyika. Endelea… Kuanzia pale Waafrika wasomi walipachikwa kasumba za ubora na uzuri wa mambo ya Wazungu ...

Read More »

ZEBAKI: Sumu hatari inayoua taratibu

Zebaki katika maeneo yenye uchimbaji mdogo wa dhahabu si msamiati unaotaka kamsi ya Kiswahili sanifu kujua ni nini na inafanya kazi gani. Katika migodi midogo iliyopo mkoani Geita, hususan machimbo ya Nyarugusu, Makurugusi, Lwamugasa na Mugusu, wachimbaji wadogo wameizoea zebaki kiasi kwamba wanaitegemea kama zinavyotegemewa kuni au mkaa kupika chakula. JAMHURI limefanya uchunguzi katika migodi hiyo (Nyarugusu, Makurugusi, Lwamugasa na ...

Read More »

Ndugu Rais wosia wa Baba usipotubadilisha ole wetu

Ndugu Rais, kama ilivyo kwa viongozi wetu wa dini wanapofanya ibada hurudia maneno yale yale na kwa msisitizo ule ule, kuwa tuache dhambi na tumrejee Muumba wetu. Maneno haya yamekwishatamkwa mara nyingi mno, lakini kwa umuhimu wake hayajawahi kuchosha wala kukifu. Basi na iwe hivyo kwa wosia aliotuachia Baba Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya, Mhashamu Evarist Marc Chengula. ...

Read More »

Manufaa ya Ngorongoro kwa jamii, taifa

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni miongoni mwa injini za maendeleo katika taifa letu. Dhima kuu ni kuhakikisha uhifadhi unakuwa endelevu, lakini wenye tija kuanzia ngazi ya chini kabisa ya jamii hadi taifa zima. Kwa kulitambua na kulizingatia hilo, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imekuwa ikitekeleza miradi mingi ya uhifadhi na jamii ndani na nje ya hifadhi. Miradi hiyo imegawanyika ...

Read More »

‘Maana ya Chuo Kikuu Huria inapotea’

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Elifas Bisanda, amezungumza na Gazeti la JAMHURI kuhusu historia, mafanikio, changamoto na hatima ya chuo hicho. Sehemu iliyopita alieleza namna OUT ilivyosambaa nchini kote. Sehemu hii anaelezea kuhusu mtandao huo na hatari inayokikabili chuo kutokana na mfumo wa usaili anaosema unaua maana halisi ya ‘Chuo Kikuu Huria’. Mwandishi MANYERERE JACKTON, ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (6)

Kusubiri ni mtihani. Mtihani mgumu sana maishani ni kuwa na subira ya kungoja wakati muafaka. “Ni vigumu kuwa na subira, lakini ni jambo baya mno kukosa zawadi za subira,” alisema Abu Bakr. Subira hata kwa mtu mwema ina mpaka. Mvumilivu hula mbivu akivumilia sana anakula mbovu. “Ufunguo wa kila kitu ni subira. Unapata kifaranga kwa kutotolewa na si kwa kuvunja ...

Read More »

Namna ya kuishinda hasira yako (1)

Unaweza kutumia miaka 20 kujenga haiba yako mbele ya jamii lakini sekunde tano tu zinatosha kukiharibu kile ulichokijenga kwa miaka 20.                                                                                  Mtu mmoja alikuwa akisafiri kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Akiwa njiani kwenda Yeriko aliona kaburi moja limeandikwa: “Njia ya Mungu imepungukiwa watu wa kuipita.” Inawezekana ni kweli, jambo la msingi ni sisi tulio hai kuipita njia ya Mungu bila kujali ...

Read More »

Uongozi Hospitali ya Amana haukumtendea haki marehemu

Kumetokea jambo ambalo nimejitahidi nibaki nalo moyoni lakini nafsi imegoma kabisa. Nafsi imegoma kwa sababu naamini kulinyamazia kutahalalisha matukio mengine mengi ya aina hii yaendelee kufanywa. Wiki iliyopita tulipata taarifa ya msiba wa mtu tunayemfahamu. Hana umaarufu, lakini ni binadamu mwenzetu. Huyu alikuwa mfanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO), Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Jina lake ...

Read More »

Yah: Sheria zetu na namna ya kukabiliana na mazoea

Nianze na salamu. Najua kwamba tumeanza mwezi wa mwisho wa mwaka huu, ni vema tukatumia fursa hii kwanza kumshukuru Mungu kwa kutufikisha hapa tulipo. Pili, kama kampuni ya gazeti, tuna kila sababu ya kuwashukuru wasomaji wetu kwa kutuunga mkono, kwa kuwa nasi kwa kipindi chote hiki. Hata hivyo lazima nikiri kuwa wapo ambao watasema tumewakwaza kwa kutowapa kile ambacho walikitarajia. ...

Read More »

Heshima ya kijana ni kazi 

Kijana na Ajira ni maneno mawili yenye maana tofauti katika istilahi ya lugha ya Kiswahili. Lakini ni maneno yenye uhusiano na ushirikiano mwema katika mazingira ya kufanya kazi ambayo huleta kipato kizuri na maendeleo mema kwa kijana. Kijana anapofanya kazi hupata heshima kwa jamii ya watu.  Nazungumzia kijana – awe ni mtoto wa kiume au wa kike, ni mtu wa ...

Read More »

Si lazima mke kumtolea ushahidi mume wake

Mathalani, mume anatuhumiwa kwa kutenda kosa fulani. Upande wa upelelezi wakiwamo polisi na wengine wanaamini mke ni mtu pekee anayejua tukio, hivyo kuwa shahidi muhimu kwao. Au mke anatuhumiwa kwa kutenda kosa na mume ndiye mtu pekee anayeweza kuwa shahidi. Swali ni je, polisi au mamlaka nyingine inaweza kumshurutisha/kumlazimishi mke au mume huyu kuwa shahidi dhidi ya mwenza wake? Tutaona ...

Read More »

Drogba atundika daruga

Mchezaji nyota kutoka Ivory Coast aliyeng’ara akiwa na Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Didier Drogba, amestaafu kucheza soka baada ya miaka 20 ya hekaheka uwanjani. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 40, ameichezea Chelsea mara mbili tofauti na kufunga jumla ya magoli 164 katika mechi 381. Pia ameshinda mataji manne ya Ligi Kuu ya Uingereza pamoja  na taji la Klabu ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons