Daily Archives: January 8, 2019

Hujuma korosho

Juhudi za Rais John Magufuli kudhibiti magendo katika biashara ya korosho, maarufu kama ‘kangomba’ zinaelekea kuingia doa kutokana na watendaji aliowaamini katika ngazi ya wilaya kushiriki biashara hiyo, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Taarifa kutoka mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi zinaonyesha kuwa baada ya watendaji wa serikali kuwadhibiti wafanyabiashara waliokuwa wananunua kangomba, wao sasa wamebaki na uwanja mpana wa kutengeneza ...

Read More »

Aliyetekwa arejeshwa kwa staili ya Mo

Raymond Mkulo (29) anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana Novemba 18, mwaka jana katika ufukwe wa Coco, Dar es Salaam, naye amerejeshwa kwa mtindo unaoshabihiana na ule uliotumika kumrejesha mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo). Mkulo alipotea kwa siku 47 tangu alipotekwa akiwa kwenye gari lake aina ya Noah lenye namba T 961 DCJ. Gari hilo ndilo linalodaiwa kukodiwa na watu wawili waliotaka ...

Read More »

Kilichong’oa mabosi TAKUKURU

Mchezo wa rushwa aliounusa Rais John Magufuli katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ukabila, ukanda na usiri wenye lengo la kunufaisha watu binafsi na jamaa zao, vimetajwa kumsukuma Mkurugenzi Mkuu mpya wa Takukuru, Diwani Athumani, kufumua mtandao alioukuta, JAMHURI limebaini. “Katika harakati za kuboresha utendaji wa Takukuru, kufumua mtandao wa ukabila, kuwadhibiti wakubwa waliopenyeza ‘vijana’ wao ndani ...

Read More »

Apandishwa kizimbani Moshi kwa udanganyifu

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imemfikisha mahakamani Mhasibu wa Mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, John Bogohe, kwa makosa matatu ikiwamo kutumia nyaraka kwa nia ya kumdanganya mwajiri. Mhasibu huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Hai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Devota Msofe na kusomewa mashtaka na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Suzan ...

Read More »

IGP inusuru Tunduru

Katika toleo la leo tumechapisha taarifa za magendo ya zao la korosho, maarufu kama ‘kangomba’ inayoendelea katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi. Kwa kiasi kikubwa, habari hiyo imejikita katika Mkoa wa Ruvuma, Wilaya ya Tunduru. Watendaji wa umma katika ngazi ya wilaya wametajwa kwa kiasi kikubwa kuhusika katika biashara ya kangomba. Askari PC Mtaki ametajwa kutoa fedha za kununulia ...

Read More »

Nina ndoto

Yusufu alikuwa mtoto wa Yakobo. Akiwa na miaka 17 baba yake alitokea kumpenda sana maana alikuwa ni mwana wa uzee wake, akamtengenezea kanzu ndefu. Ndugu zake walipoona anapendwa zaidi wakaanza kumchukia. Siku moja Yusufu akaota ndoto na kuwaambia ndugu zake, “Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. Tazama, sisi tulikuwa tukifunga maganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama na tazama, miganda yenu ...

Read More »

Binadamu kutoka Afrika walivyozagaa duniani

Watu wa kale walitumia zana za mawe kuchinja mawindo yao. Katika kutekeleza hayo, huacha alama za chale kwenye mifupa. Hizi chale huweza kutambuliwa kutokana na umbo lake. Nyingi huwa na umbo la ‘V’ pamoja na mikwaruzo miembamba upande wa ndani isababishwayo na chembechembe ndogondogo za mawe yaliyotengenezea zana hizo. Chale hizi husongamana maeneo maalumu ya mifupa na kwa mpangilio fulani. ...

Read More »

Rais Magufuli, Dk. Mpango jengeni wafanyabiashara

Wiki hii naandika makala kwa kusukumwa na kauli za viongozi wakuu wawili wa taifa hili. Hawa si wengine, bali ni Rais John Pombe Magufuli na Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango. Rais Magufuli ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuepuka kufunga biashara, badala yake wapokee kidogo wanachopewa kama kodi kinachobaki wakubaliane utaratibu wa kukilipa. Dk. Mpango yeye amekuja na maagizo ...

Read More »

NSSF watekeleza agizo la Rais

Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeanza utekelezaji wa maagizo ya Rais John Magufuli kwa kuhakiki waliokuwa wafanyakazi wa migodi na ajira za muda mfupi.  Akizungumza mwishoni mwa wiki, Meneja Kiongozi wa Matekelezo (Chief Manager Compliance and Data Management), Cosmas Sasi, amesema mbali na NSSF kuendelea kulipa mafao mbalimbali kwa wanachama wake kwa wakati, imeanza kazi ya kuhakiki wafanyakazi waliokuwa ...

Read More »

Waraka wa korosho kwa Rais Magufuli

Natanguliza shukrani kwako Rais wetu mpendwa kwa utendaji kazi wako uliotukuka na ambao watu wa mataifa mengine wanatamani ungekuwa rais wao. Nchi nyingi zinakupigia mfano japo umeiongoza Tanzania kwa miaka mitatu tu! Naamini si wote watakaoukubali utendaji wako hasa waliokatiwa mirija ya kutunyonya sisi wananchi, lakini ingepitishwa kura ya maoni leo ndipo ungeshuhudia watu wanaokukubali. Hivyo kwa msemo wako wa ...

Read More »

Mwendokasi wa magari sasa ujangili mpya Hifadhi ya Taifa Mikumi

Umewahi kuendesha gari katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na ukamgonga mnyama yeyote ndani ya hifadhi? Unakumbuka kama ulilipa faini za kumgonga mnyama? Basi kwa taarifa yako magari ndiyo yamekuwa majangili wapya katika hifadhi hiyo. Wakati Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) wakishusha kiwango cha ujangili katika hifadhi hizo, sasa ujangili mpya ni ule unaohusisha magari. Magari ndani ya Mikumi ...

Read More »

TPA: Tunamjibu mteja ndani ya dakika 3

Bandari ni lango kuu la biashara kwa Tanzania na nchi zote zinazotumia bandari zetu hususan Bandari ya Dar es Salaam ambazo; ni Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Sudan Kusini na Comoro. Tunapoanza mwaka 2019, tumeona ni vema kukufahamisha ukweli huu kwa nia ya kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wetu. Kutokana na umuhimu ...

Read More »

Ndugu Rais ili tupite salama lazima tubadilike kifikra

Ndugu Rais, hivi karibuni wengi wamekuwa na shamrashamra, vifijo na nderemo huku wakiuaga mwaka 2018 na huku wakiushangilia mwaka 2019. Wanasema ni upendeleo wamepewa kuufikia mwaka 2019 kwa sababu wengi walitamani kuufikia, lakini hawakuweza. Tunajiuliza ni wakati gani waliwauliza hao wengine ambao hawakuweza nao wakawajibu kuwa walitamani kuufikia? Mwanadamu ana maneno mengi ya kujifariji na hasa anapoona maisha yake yanaleta ...

Read More »

Kuporomoka maadili nani alaumiwe?

Nimesukumwa kuandika makala hii kwa ukweli kwamba hatuwezi kujenga taifa lenye maadili mema pasipo familia zenye maadili mema. Siku moja nilipita katika mtaa fulani nikakuta majibizano ya ajabu kati ya mtoto na mzazi, nilishangaa sana. Ustawi wa taifa unaanzia nyumbani. Kinyume chake ni kweli. “Kuporomoka kwa taifa kunaanzia nyumbani.’’ Ni methali ya Kiafrika. Uhai wa taifa unategemea uhai wa familia. Tunapaswa kutambua ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (11)

Urafiki ni mtihani. “Katika mafanikio marafiki zetu wanatujua; katika shida tunawajua,” alisema John C. Collins. Mtu akifanikiwa anawakwepa baadhi ya marafiki, lakini akiwa na shida baadhi ya marafiki wanamkwepa. Urafiki ni mtihani. Msemo wa “biashara haina urafiki” unabainisha kuwa urafiki ni mtihani. Methali ya “maskini hana rafiki” inabainisha kuwa urafiki ni mtihani. Methali ya “ukimwamini usimwambie yote” inabainisha kuwa urafiki ...

Read More »

Wavamizi hawa si wa kuchekewa

Nimesoma tamko la serikali linalohusu uamuzi ‘mgumu’ ilioamua kuuchukua dhidi ya wavamizi wa hifadhi mkoani Kigoma. Tathmini iliyofanyika mkoani humo imeonyesha hifadhi za misitu na mapori ya akiba yamevamiwa kwa shughuli za kilimo, ufugaji, ukataji miti na baadhi ya vijiji vimesajiliwa ndani ya maeneo hayo. Uvamizi huu umesababisha athari nyingi zikiwamo za kupotea kwa uoto wa asili na viumbe hai, wakiwamo ...

Read More »

Buriani mwaka 2018, karibu mwaka 2019

Namshukuru Mwenyezi Mungu kunijalia na kuniwezesha kuuona na kuukaribisha mwaka mpya 2019 na kunipa uwezo kutamka buriani mwaka 2018. Mwaka ambao kwangu na kwa nchi yetu Tanzania ulikuwa ni mwaka wa mafanikio. Nina wajibu tena na tena kutoa shukrani kwa Mola wangu kunijalia pumzi, afya njema na nguvu tele hata kushika kalamu na kutuma salamu za upendo na amani kwako ...

Read More »

Yah: Utabiri wangu haukomi, natabiri tena 

Nianze kwa salamu za mwaka mpya kwa wasomaji wetu wote, najua tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kutuvusha mwaka huu, mwaka jana ulikuwa na mambo yake, yapo yaliyokuwa ya heri kwetu na yapo ambayo kwa kweli yalizikera nafsi zetu, lakini pamoja na yote tuna kila sababu ya kushukuru. Nilikuwa sijui kama miaka inakimbia kiasi hiki, mara mwaka jana imekuwa historia, ...

Read More »

Tabuley, Pepe Kalle Wakumbukwa Kongo 

Desemba mwaka jana baadhi ya wapenzi na mashabiki wa wanamuziki Tabu Ley na Pepe Kalle walifanya kumbukizi ya wanamuziki hao.  Ikumbukwe kuwa kifo cha Pepe Kalle kilitokea Novemba, 1998 wakati Tabu Ley alifariki dunia Desemba 2013, kutokana na mshtuko wa moyo kwenye Hospitali ya Ngaliema jijini Kinshasa. Kwakuwa wasifu wa nguli hawa ni mrefu sana, safu hii leo inamzungumzia marehemu ...

Read More »

Zahera asimamia nidhamu Yanga

Ukienda mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam yalipo Makao Makuu ya Klabu ya Yanga utawakuta viongozi, mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo hawana presha yoyote kuhusiana na mwenendo wa timu yao, wanakunywa tu kahawa. Wanaamini Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera,  ameiweka timu hiyo vizuri pamoja  na kushika usukani wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kujikusanyia ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons