Monthly Archives: February 2019

Wafuja mamilioni

Ufisadi wa fedha za kilimo cha miwa na kiwanda cha sukari vilivyobuniwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga, ndio uliomfanya Rais John Magufuli, amng’oe kwenye nafasi hiyo, JAMHURI limebaini. Mradi huo ulibuniwa na Luoga kwa kigezo cha kuongeza kipato cha wananchi wa wilaya hiyo wasiokuwa na zao la biashara, kwani bila mradi wa kuwaingizia pato wanalazimika kulima na ...

Read More »

‘Wapigaji’ ATCL wadakwa

Je, una akaunti ya benki nje ya nchi? Umewahi kujiuliza kuhusu usalama wa kadi yako? Hebu fanya mpango ukague kadi yako na ujiridhishe kama haijadukuliwa na fedha zako kutumika kulipa huduma ambazo hukuzitumia. Mtandao unaojihusisha na matumizi ya kadi za benki za wizi katika ununuzi wa bidhaa na huduma umefikia tamati kwa kudhibitiwa na uongozi wa Shirika la Ndege la ...

Read More »

Waliofuja KNCU hawatapona – Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema serikali inaendelea na uhakiki wa mali zote za Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro (KNCU) na kuonya kuwa hakuna atakayepona kwa wale wote watakaobainika kufuja mali za chama hicho kikongwe nchini. Baadhi ya viongozi wa chama hicho wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria na kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi. “Mwaka jana tulibaini madudu KNCU, nikatuma ...

Read More »

Wananchi waitunishia Serikali msuli

Mvutano umeibuka kati ya serikali na wakazi wa Kata ya Nyatwari, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara baada ya wananchi hao kutakiwa kuhama huku wao wakipinga amri hiyo. Wananchi hao wametakiwa kuondoka kwenye kata hiyo ili kupisha njia ya wanyama wanaotoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwenda kunywa maji Ziwa Victoria. Februari 21, mwaka huu, mamia ya wakazi wa Nyatwari waliapa ...

Read More »

Tuongeze uwekezaji elimu

Kwa muda sasa tunapata taarifa kutoka sehemu mbalimbali za nchi juu ya uhaba wa vyumba vya madarasa kwa watoto walioshinda mtihani wa darasa la saba kwenda kidato cha kwanza mwaka 2018. Malalamiko ya ukosefu wa vyumba vya madarasa yameanza kujitokeza si tu katika ngazi ya sekondari, bali hata ngazi ya shule za msingi. Kwa mfano Shule ya Msingi Kyakailabwa, katika ...

Read More »

NINA NDOTO (8)

‘Tumezaliwa kwa ajili ya wengine’   Hapo zamani za kale kulikuwa na mkulima aliyenunua vibuyu viwili vya kutekea maji. Baadaye alikuja kugundua kwamba kibuyu kimoja kilikuwa kimetoboka sehemu ya chini. Mkulima huyo alizoea kutekea vibuyu hivyo maji kutoka mtoni na kuyapeleka mjini kwake. Kibuyu kilichokuwa kimetoboka kilimwaga maji njia nzima, hivyo kilijiona hakifai. Kibuyu kingine kilijigamba na kujisifu huku kikikitania ...

Read More »

Wananchi walilia fidia mradi wa umeme

Wananchi wa maeneo ya Kinyerezi, Chalinze na Tanga waliohamishwa kupisha mradi wa umeme wa North, East, Grid wa (Kv 400), wameilalamikia serikali kwa kushindwa kuwalipa fidia licha ya zoezi la uhakiki wa maeneo hayo kukamilika tangu mwaka 2015. Wakizungumza na Gazeti la JAMHURI kwa nyakati tofauti, wamesema ukimya wa serikali juu ya jambo hilo tangu mwaka 2015 umekuwa kama msiba kwao kiasi ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (3)

Wiki iliyopita nilieleza sehemu ya pili ya taratibu za kuanzisha biashara kwa mtu yeyote mwenye nia ya kufanya hivyo hapa Tanzania. Nimeandika mwendelezo wa hatua ya kwanza ambayo ni ‘wazo la biashara’ na nikagusia hatua ya pili ambayo ni ‘eneo la kufanyia biashara’. Jambo la tatu katika kuanzisha biashara unapaswa kuamua MFUMO WA KUFANYA BIASHARA yako. Sitanii, mfumo wa kufanya ...

Read More »

Dalili za shambulio la moyo

Kinga ni bora kuliko tiba. Mara nyingi magonjwa mengi yanahatarisha afya zetu kwa kutoziweka maanani dalili zake. Bila shaka makala hii leo itakusaidia katika kuzitambua dalili zinazoashiria shambulio la moyo na kuwahi kuwaona wahudumu wa afya. Uchovu usio wa kawaida Uchovu usio wa kawaida ni moja ya dalili kuu zinazoashiria kuwa mtu yumo hatarini kupata shambulio la moyo. Dalili hii mara ...

Read More »

Serikali yahaha Monduli, Karatu kupata maji

Miradi ya maji lazima itekelezwe kwa wakati kama serikali ilivyopanga ili wananchi wapate huduma ya maji safi na salama, na kujishughulisha na kazi nyingine za maendeleo, ikiwamo kutumia maji hayo kuongeza thamani ya bidhaa mbalimbali na kuleta maendeleo zaidi. Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amesema hayo baada ya kukagua miradi ya maji katika wilaya za Monduli, Karatu,  Bagamoyo na ...

Read More »

Ndugu Rais nitupeni mimi

Ndugu Rais, maandiko yanasema watu walikuwa wanasafiri katika chombo baharini. Chombo kilisheheni mizigo mingi, lakini kilienda bila tatizo. Kilipofika katikati ya bahari chombo kikaonekana kulemewa na mizigo. Kikaanza kuzama. Abiria wakapatwa na mfadhaiko wakaamua kuitupa mizigo baharini, lakini chombo kiliendea kuzama. Nao walipokwisha kata tamaa wakisubiri kuzama pamoja na chombo, walijikusanya pamoja, wakaulizana, “Jamani ni nani kati yetu mwenye shida ...

Read More »

Kiongozi anao wajibu kuelimisha anaowaongoza

Miongoni mwa wajibu wa kiongozi ni kuelimisha anaowaongoza. Anapata fursa nyingi zaidi za kujielimisha na anao wajibu wa kutawanya elimu hiyo kwa wengine. Hiyo elimu inahitajika sana kwenye uanaharakati. Naamini hivi kwa sababu lipo kundi kubwa la watu linaingizwa kwenye harakati mbalimbali bila kufahamu vyema malengo, faida, hasara, ya wanachounga mkono. Uanaharakati una maana pana zaidi ya ule tunaouhusisha na ...

Read More »

Utaratibu wa kusajili day care

Badala ya kuendesha shule za kulea watoto kinyemela huko mitaani, makala hii itakueleza namna ambavyo unaweza kusajili, hivyo ukaendesha shughuli hii kihalali. Ifahamike kuwa ni kosa la jinai kuendesha kituo au shule ya kulea watoto  bila usajili. Kanuni ya 4(1) ya Kanuni za Vituo vya Kulea Watoto Wadogo Mchana na Watoto Wachanga za Mwaka 2012,  zinasema kuwa mtu hataendesha kituo ...

Read More »

Demokrasia Tanzania imetundikwa msalabani (2)

Wiki iliyopita makala hii iliishia pale ambapo ilionyesha kwamba Tanzania ni yetu, wa kuiua ni sisi wenyewe na wa kuijenga ni sisi wenyewe. Maisha yana ladha pale tu tunapotofautiana mitazamo, sasa endelea … Maisha hayawezi kuwa na ladha kama mitazamo yetu itafanana. Tukifanana mitazamo tutakuwa kama wanyamapori wa mwituni wajulikanao kama ‘nyumbu’. Kuna mafanikio makubwa katika kutofautiana kimtazamo. Maana yangu ni ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (18)

Upendo ni mtihani, palipo na husuda, hakuna upendo. Palipo na chuki hakuna upendo. Palipo na umbea hakuna upendo. Maneno kwenye kanga za kina mama yanabainisha upendo ni mtihani. Chokochoko za jirani hazinitoi ndani, mtamaliza visigino kwa safari za umbea. Hunilishi, hunivishi na wala hunibabaishi, vikao kaeni, umbea  acheni, penye udhia penyeza rupia. Usisafirie nyota ya mwenzio, macho yanacheka, moyo unalia. ...

Read More »

Kufungwa Malkia wa Tembo si mwisho wa ujangili

Malkia wa Tembo amefungwa jela miaka 15. Hii ni habari njema kwa wahifadhi. Sijasikia wanaobeza hukumu hiyo, japo wapo wanaoona ni ndogo ikilinganishwa na tembo 430 waliotoweka kutokana na mwongozo wake. Kwenye kesi hii waliofungwa ni wawili. Huu ni “utani”. Haiwezekani tembo 430 wauawe na watu wawili tu. Hatujaambiwa madereva, walenga shabaha, wapagazi, wasafirishaji na wengine wote kwenye mtandao huu ...

Read More »

Tusipoteze lugha mama tukakuza lugha ya mapokeo

Umoja wa Mataifa (UN) umepanga Februari  21, kila mwaka ni ‘Siku ya lugha ya mama duniani.’ Siku hii ina lengo na madhumuni ya kukumbusha na kudumisha utamaduni (historia, mila na desturi) wa kuzungumza lugha mama ambayo ndiyo lugha ya asili kwa mtu yeyote duniani. Katika utafiti uliofanywa na umoja huo, na ripoti yake kutolewa mwaka jana inaeleza kila baada ya ...

Read More »

Yah: Na leo nakumbuka mambo ya zamani tu

S alamu zenu waungwana ambao naamini wengi wenu mnaosoma waraka wangu ni wale wenye umri wangu na kweli mnakumbuka pamoja na mimi. Nawapa salamu kwa sababu naamini kuwepo kwetu mpaka leo ni kwa neema tu na matunzo tuliyopata kutoka kwa wazazi wetu, wazazi ambao hawakupata mafunzo ya malezi kutoka mahali popote zaidi ya kujitegemea na kutumia mbinu za asili. Hawakuwa ...

Read More »

Simba inakula ‘viporo’

Wiki iliyopita timu ya Simba imeendelea kula viporo vyake vema katika mechi zake baada ya kuilaza timu ya Azam kwa magoli 3-1 katika Uwanja wa Taifa. Simba ilipata magoli hayo kupitia kwa Meddie Kagere aliyefunga magoli mawili huku jingine likifungwa na John Bocco, na lile la kufutia machozi la Azam likifungwa na Frank Domayo, hivyo kujiongezea nafasi ya kutwaa ubingwa ...

Read More »

Serikali yalizwa

Kampuni ya Crown Lapidary ya jijini Arusha inayojihusisha na biashara ya madini imekumbwa na kashfa ya kutorosha madini yenye thamani ya dola za Marekani milioni 300 (shilingi zaidi ya bilioni 700), JAMHURI limebaini. Madini hayo aina ya Green Garnet, yanatajwa kuwa na thamani kubwa kuliko aina nyingi za madini ya vito, ikiwamo tanzanite. Tukio hilo ingawa lina muda sasa, limeishitua serikali, ...

Read More »

Fahamu kuhusu ‘mwuaji’ watoto Njombe

Ni baba wa watoto wanne, mganga wa jadi aeleza siri imani ya utajiri wa kichawi Maisha ya mtuhumiwa, Joel Nzuki, katika kesi ya mauaji ya watoto watatu wa familia moja yameelezwa kutokuwa na viashiria vya wazi kwa mhusika kuhusishwa na unyama huo, JAMHURI limeelezwa. Kwa mujibu wa ndugu wa mtuhumiwa huyo, pamoja na wenzake wanaofanya biashara ya kuuza mbao pamoja ...

Read More »

Aibu tupu stendi Makambako, Njombe

Mpita Njia, maarufu kama MN wiki mbili zilizopita alikuwa katika miji ya Njombe na Makambako kwa nyakati tofauti, ndani ya Mkoa wa Njombe kwa Wabena, Wahehehe, Wakinga na makabila mengine mchanganyiko ya Tanzania na hata watu wa mataifa mengine, ikizingatiwa kuwa Afrika ni moja, chambilecho Mwalimu Julius Nyerere na Azimio la Arusha. Naam, Njombe na Makambako kuna mengi hasa! Ndiyo, ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons