Daily Archives: February 5, 2019

Magufuli achukua mkondo mpya

Ugumu wa upatikanaji wa fedha ulioibua msemo maarufu wa “vyuma vimekeza”, umebadilika kwa serikali kuanza ‘kulegeza’ baadhi ya mambo. Manung’uniko yameanza kupungua mitaani ambako fedha ziliadimika kwa kiwango kikubwa kuanzia mwaka 2016, lakini Rais John Magufuli akisema waliokuwa wakilalamika ni mafisadi waliozoea kujipatia fedha kwa njia haramu. Desemba 14, 2017 alipozungumza na walimu, alisema: “Watu wanaosema vyuma vimekaza, kama vimekaza ...

Read More »

Mjomba amtia mimba mpwawe 

Ukishangaa ya Musa…hivyo ndivyo naweza kusema kuhusu binti (jina limehifadhiwa kwa sababu za kisheria) mwenye umri wa miaka 16, ambaye anatakiwa kuwa shuleni, lakini haiko hivyo kwake, yupo nyumbani analea mtoto wake mwenye umri wa miezi minne. Anatamani kupata nafasi ya kusoma tena lakini anashindwa kuwatumikia ‘mabwana wawili’, yaani mtoto na shule, yeye amechagua kumlea mtoto. Mtoto wake amepewa jina ...

Read More »

MPITA NJIA

Bunge na madereva wa wabunge…!   Umri wa Mpita Njia (MN) unatosha kumfanya awe na kumbukumbu ya mengi – kuanzia zama za ukoloni hadi uongozi wa Awamu hii ya Tano. Anakumbuka zama zile za ubaguzi ambapo Mzungu alikuwa mtu wa daraja la kwanza; Mhindi, Mwarabu na Machotara wakiwa watu wa daraja la pili; na daraja la tatu na lililodhoofu lilikuwa ...

Read More »

Wawekezaji waanza na elimu Ulanga

Kampuni ya uchimbaji madini ya kinywe – Mahenge Resources imejitolea kuboresha sekta ya elimu katika Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro. Kampuni hiyo kwa kushirikiana na serikali ya wilaya imechangia Sh milioni 16 kwenye harambee maalumu iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, lengo likiwa ni kuboresha majengo na miundombinu ya shule wilayani humo. Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi fedha ...

Read More »

Mlungula wadaiwa kuvuruga vigogo TFDA, Jiji Mwanza

Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Kanda ya Ziwa imeingia ‘vitani’ na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikizuia maofisa wa jiji hilo kufanya ukaguzi kwenye maduka ya vipodozi, dawa na maeneo mengine ya kibiashara. Haya yanafanyika huku Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ikiwa imekwisha kumwandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa TFDA ikimuomba kufanya kazi ...

Read More »

WHO: Ajali 16,000 zasababisha vifo nchini

Takwimu za Jeshi la Polisi na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusiana na  vifo vinavyosababishwa na matukio ya ajali za  barabarani Tanzania zimezua hofu ya mwenendo halisi wa usalama barabarani nchini. Desemba mwaka jana, shirika hilo limetoa ripoti yake ijulikanayo kama ‘Global status report on road safety 2018’, imebainisha kwamba matukio yaliyosababisha vifo kutokana na ajali za barabarani na kuripotiwa na ...

Read More »

Rais Magufuli, Dk. Mpango jengeni wafanyabiashara (5)

Katika makala zilizopita nimeshauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanzisha Kitengo cha Kuanzisha na Kukuza Biashara. Ni wiki ya tano sasa nikiwa naandika makala hii kuunga mkono uamuzi wa Rais John Magufuli na Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, kupiga marufuku TRA kufunga biashara ya mtu yeyote hapa nchini, isipokuwa kwa wakwepa kodi sugu, ila hiyo nayo ni lazima iwe ...

Read More »

ATCL imefufuka, imesimama, inapaa

1. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani na kuliboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua ndege mpya, je, idadi ya  abiria imeongezeka kiasi gani tofauti na ilivyokuwa awali? JIBU: Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani Novemba 5, 2015. Kati ya ahadi zilizotolewa na Mhe. Rais wakati wa kampeni za uchaguzi ni pamoja na kuifufua Kampuni ya ...

Read More »

Rais amethubutu, tumuunge mkono

Awali ya yote nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kumpata kiongozi shupavu. Mungu ni mwema, akamuinua Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli awe Rais wa Tanzania baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015. Kabla ya uchaguzi huo, Watanzania wengi walitarajia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kingeporomoka. Kusema kweli haikuwa kazi rahisi, bali ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu kumpata rais shupavu ...

Read More »

Ndugu Rais tunajenga huku tunabomoa nyumba haitakwisha

Ndugu Rais, Mungu ni mwema. Ni mwema siku zote. Alikuwapo mwanamwema mmoja akiitwa Beni Kiko. Huyu alikuwa mtangazaji ambaye aliwavutia wasikilizaji wengi kwa namna alivyokuwa akiziwasilisha ripoti zake. Siku ya kwanza akiwa Dodoma mnyama mkali alimshambulia mtu hadi kumuua. Beni Kiko akaripoti. Haukupita muda tembo alimuua mtu kwa kumkanyagakanyaga huko huko Dodoma. Beni Kiko akaripoti. Wakati watu wanatafakari namna ya ...

Read More »

Vikao vya wazi vya Rais Magufuli vinafaa

Vikao vya wazi na rais vinafaa, pamoja na kwamba Rais Magufuli ‘anatisha’. Mmoja wa waalikwa wa kikao kilichoitishwa Ikulu na Rais John Magufuli ametamka kuwa Rais “anatisha”. Yapo mazingira yanayohitaji rais kutisha, kama kutisha kunaleta pia uadilifu na uwajibikaji ndani ya utumishi wa umma. Lakini kutisha kunaweza pia kuzuia taarifa muhimu kumfikia rais. Aliyetishika kasema kuwa si rahisi kuongea yote ...

Read More »

Ushahidi wa daktari kuhusu sababu za kifo

Unaweza kuwa wewe, ndugu yako, rafiki au  jamaa yako ameunganishwa katika kesi ya mauaji. Aghalabu, daktari anasubiriwa kutoa ushahidi mahakamani kuhusu sababu za kifo cha marehemu. Na ni ushahidi huo wa daktari utakaokuondoa katika kesi hiyo ya mauaji au utakuingiza katika kesi hiyo, hivyo kutiwa hatiani na kuadhibiwa. Lakini si daktari tu, bali wenye kesi wote ambao ushahidi wake unahitaji ...

Read More »

Historia ya Sikukuu ya Valentine’s Day (2)

Wiki iliyopita makala hii inayomhusu Mtakatifu Valentino iliishia pale ambapo aliweza kuhamasisha upendo na taratibu watu walianza kujirekebisha na upendo ukaanza kurudi ndani ya ndoa.  Hata hivyo Mfalme Claudio alimchukia Valentino na kumfunga gerezani. Endelea… Wachumba walifundishwa na Valentino kwamba upendo wa kweli wa wapendanao hujidhihirisha katika kufunga ndoa mbele ya Mwenyezi Mungu.  Hivyo, aliwakemea bila woga vijana wengi waliokuwa ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (15)

Mawazo ni mtihani. “Mawazo yana nguvu kuliko bunduki,” alisema Joseph Stalin. Mawazo yakisongana yanaleta msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo unadhoofisha mwili. Mawazo ni mtihani. Chunga mawazo yako yanazaa maneno. Chunga maneno yako yanazaa matendo. Chunga matendo yako yanazaa tabia. Chunga tabia yako inazaa desturi. Chunga desturi yako inazaa hatima yako. Yote yanatokana na mawazo. Kuna upande mzuri wa mawazo. ...

Read More »

Tusiwe taifa la kuwaza mapumziko

Rais John Magufuli alipozungumza na viongozi wa dini, kwa chini chini kulionekana tofauti za hapa na pale. Tofauti hizo hazikuzungumzwa kwa mwangwi, na kwa maana hiyo ilisaidia kutoibua hisia za utengano. Kiongozi mmoja wa Kikristo alitoa maombi yaliyonikumbusha maneno niliyopata kuyaandika miaka kenda iliyopita na kuyarejea mwaka 2013. Katika safu hii niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari: ‘Wakati mwingine Wakristo ...

Read More »

Hekima na busara zitawale wasanii

Walimwengu wanatambua wasanii wa muziki ni kundi ambalo linatoa mafunzo yenye maarifa mbalimbali kwa jamii. Tungo zao hutazamwa kwa shauku kubwa, kwa matarajio ya kuelimisha na kuburudisha jamii. Aidha, ndimi zao zinatawaliwa na adabu. Katika fasihi hii namtazama mwana mama Siti bint Saad, aliyekuwa mwimbaji maarufu wa nyimbo za taarabu katika Kisiwa cha Unguja. Alitumia hekima na busara zipi kuvuta ...

Read More »

Yah: Njombe nini kimetusibu, ni ukarimu wetu?

Kabla sijaanza na salamu ni vema nikatumia fursa hii kutoa pole nyingi sana kwa wafiwa na watoto wote waliopoteza marafiki zao wa utotoni. Wapo watoto ambao kwa kitendo hiki huenda ndoto zao pia zikawa zimekufa kutokana na wenzao kutendewa matukio ya kutisha. Najua ninazo salamu lakini kule Njombe katika kipindi hiki naamini hawahitaji salamu, bali wanahitaji pole ya matatizo yaliyowasibu. Katika ...

Read More »

Kipanya: Nilikotoka

Mchora katuni maarufu, Ally Masoud (Masoud Kipanya), amesema hataogopa kumchora rais wa nchi kwa kuwa havunji sheria na kwamba uchoraji wa katuni umedumu kwa muda mrefu duniani kote. Kipanya licha ya kuwa ni mchoraji wa katuni, pia ni mtangazaji wa kituo cha redio na televisheni, amewahi kuwa mhariri msanifu wa magazeti ya katuni. Pia alikuwa mhariri na mchoraji wa Gazeti la ...

Read More »

Ambokile amefungua njia

Mchezaji wa zamani wa Mbeya City, Eliud Ambokile (pichani), wiki iliyopita alisafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujiunga na timu ya Black Leopards inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo kwa mkopo wa miezi mitatu. Katika maisha ya soka Ambokile amepiga hatua kubwa, amefanikiwa kupata nafasi ya kucheza kwenye ligi bora licha ya kuwa na umri mdogo.   Usajili ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons