Daily Archives: February 12, 2019

Aeleza alivyoua watoto Njombe

Kabrasha linaanza kufunguka juu ya nani anahusika na mauaji ya watoto mkoani Njombe huku ikithibitika kuwa ndumba, uchawi, ukimwi na ujinga vimekuwa nguzo ya mauaji hayo, JAMHURI limebaini. Ni wiki mbili sasa tangu matukio ya mauaji ya watoto wasiopungua saba katika mazingira ya kutatanisha na kutikisa taifa yaanze kutokea mkoani Njombe na JAMHURI limebaini namna baadhi ya matukio hayo yalivyotekelezwa. ...

Read More »

Ubabe wa wachuuzi

Mpita Njia (MN) yapo mambo anamkosoa Rais Magufuli, lakini yapo mengine – tena mengi – anayokubaliana naye. Waswahili walisema mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. Kazi inayofanywa sasa katika maeneo mbalimbali nchini inatia fora. Kumjaza sifa zilizopitiliza kunaweza kumfanya abweteke, lakini itoshe kusema yapo mazuri yanayopaswa kusemwa na kwa kweli Watanzania wana kila sababu ya kujidai. Ujenzi wa barabara umeshika ...

Read More »

Mjomba amtia mimba mpwawe (2)

Wiki iliyopita Gazeti la JAMHURI liliandika habari kuhusu binti wa shule anayedaiwa kutiwa mimba na mjomba wake. Hapa chini ni mwendelezo wa mahojiano ya wahusika wa tukio hilo. Endelea… Saimoni anasema kisa hicho kimetengenezwa na mama yake mzazi ili kukwamisha suala la mirathi, anasema familia yake wameamua ‘kumbambikia’ tuhuma hiyo kama njia ya kumficha mtuhumiwa halisi aliyetajwa kwa mara ya ...

Read More »

Wanafunzi Moshi wajisaidia vichakani

Ukosefu wa vyoo katika baadhi ya shule za msingi na sekondari Wilaya ya Moshi umechangia kwa baadhi ya wanafunzi kujisaidia vichakani na wengine kwenye vyoo vya wananchi wanaoishi karibu na shule hizo. Hatua hiyo imetokana na baadhi ya miundombinu ya vyoo kwenye shule hizo kuwa chakavu na kutishia usalama wa wanafunzi kutokana na vyoo hivyo kuwa katika mazingira hatarishi. JAMHURI ...

Read More »

Waziri Mkuu anena

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema serikali imejiandaa kumjibu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kwa ushahidi; na sasa inachofanya ni kumsubiri arejee nchini. Amesema serikali inatambua kuwa Lissu anatibiwa, na kwa maana hiyo si jambo la busara kujibizana na mgonjwa. Waziri Mkuu ametoa msimamo huo katika mahojiano maalumu na JAMHURI yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dodoma muda mfupi kabla ya ...

Read More »

Mauaji Njombe hayakubaliki

Habari kubwa katika gazeti letu la leo inahusiana na mauaji ya watoto yanayoendelea mkoani Njombe. Serikali kupitia vyombo vya dola imeimarisha ulinzi na usalama Njombe. Bunge limeombwa kuunda kamati ya kuchunguza mauaji haya. Uchunguzi wa Gazeti hili la JAMHURI umebaini kuwa mauaji haya yanatokana na imani za kishirikina. Mmoja wa watu wanaoshikiliwa na vyombo vya dola atakayefikishwa mahakamani muda wowote ...

Read More »

Nina ndoto (6)

Watu ni nguvu. Ukikaa na watu bora utakuwa mtu bora. Ukikaa na watu wa kawaida utakuwa mtu wa kawaida. Ukikaa na watu wanaowaza mambo hasi utaanza kuwaza mambo hasi, ukikaa na watu wanaowaza mambo chanya utakuwa mtu chanya. Ukiwa na ndoto unahitaji kuambatana na watu wenye ndoto. Ukiwa na maono makubwa unahitaji kuambatana na watu wenye maono makubwa. Tai siku ...

Read More »

Zakaria amkaanga Luoga

Siku kadhaa baada ya Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga, mfanyabiashara maarufu, Peter Zakaria, ambaye yuko mahabusu ameibua mambo mapya yanayomhusu Luoga. Zakaria ambaye amezungumza na Gazeti la JAMHURI kupitia kwa msemaji wa familia hiyo, Samuel Chomete, amesema amefurahishwa na uamuzi wa Rais Magufuli wa kumfuta kazi Luoga. Januari 27, mwaka huu, ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (1)

Wiki iliyopita nimehitimisha makala iliyokuwa ikiwasihi Rais John Magufuli na Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, kujenga wafanyabiashara nchini. Nimeandika makala hii katika matoleo matano yaliyopita, na nashukuru tayari maandishi yangu yamezaa matunda. Nilianza kuandika makala hizi baada ya Rais Magufuli kuwazuia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wasiwakadirie kodi kubwa isiyolipika wafanyabiashara. Dk. Mpango naye amewazuia TRA kufunga biashara ya ...

Read More »

Ukiona dalili hizi za saratani muone daktari

Saratani ni muunganiko wa magonjwa ambayo mara zote husababishwa na uzalishwaji wa seli za mwili kupita kiasi kinachohitajika mwilini, na seli hizo huendelea kujigawa kupita kiasi na kutengeneza kiasi kikubwa kuliko mwili unavyoweza kuhimili. Ukuaji huu wa seli hizi unaweza kusababisha vimbe mbalimbali katika mwili na uvimbe unavyokuwa mkubwa unasababisha kubanwa kwa baadhi ya viungo muhimu mwilini kama vile neva, mishipa ya ...

Read More »

Mkaa unaotunza misitu, kuleta neema Kilosa

Hifadhi ya Taifa ya Mikumi imepakana na vijiji 19, Kijiji cha Ihombwe kilichoko Kata ya Mikumi, wilayani Kilosa kinajivunia mradi wa mkaa endelevu uliopo kijijini hapo. Ni kupitia mradi huo kijiji kimefanikiwa kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 40 wanaofanya kazi ya doria ya kulinda misitu iliyopo kijijini hapo huku kikitajwa kujipatia maendeleo makubwa kutokana na kuuza mkaa. Mkaa endelevu ...

Read More »

Uwekezaji Sao Hill ni tija kwa taifa

Namshukuru Mwenyezi Mungu kupata fursa hii kufafanua juu ya uwekezaji kwenye mashamba ya miti. Kama tunavyofahamu, misitu ni rasilimali muhimu kwa uhai wetu na viumbe wengine. Hata hivyo, wengi wanaiona misitu kama chanzo cha kupata mbao, magogo, nguzo, mkaa na kuni. Isitoshe, wapo wanaonufaika kwa kufanya biashara ya mazao ya misitu kama kuuza asali na nta. Kwenye mada hii naeleza ...

Read More »

Ndugu Rais tulee katika njia ifaayo nasi hatutaiacha

Ndugu Rais, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa mimi si mwanasiasa. Sijawahi kujiunga na chama chochote cha kisiasa tangu kuzaliwa kwangu. Na nitabaki hivi nilivyo. Nitaisema kweli kwa ajili ya amani ya nchi yangu na kwa ajili ya ustawi wa Watanzania wenzangu huku nikimwombea afya njema Rais wangu. Muumba wangu anijalie mwisho mkamilifu! Siasa ni kazi njema. Lengo la chama chochote ...

Read More »

Siasa ni uwanja wa maajabu

Mwaka juzi mwanasiasa wa siku nyingi wa nchini Malaysia, Dk. Mahathir Mohamad, alishinda uchaguzi kwa kumuondoa madarakani Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Najib Razak. Kilichotokea kinashangaza. Inakuwaje babu wa miaka 92 afanye kampeni kwa mafanikio na kuweza kumuengua waziri mkuu aliyekuwa madarakani? Na afanye hivyo baada ya kustaafu siasa kwa miaka 15, akijipatia sifa ya kuwa kiongozi wa nchi mzee ...

Read More »

Kuendesha gari spidi ndogo, kosa kisheria

Wapo watu wanaojua kuwa kuendesha gari kwa mwendo mdogo ndio ustaarabu na ndilo jambo zuri linalopendwa sana na sheria.  Yeyote mwenye mawazo ya aina hii amekosea sana. Kifungu cha 56 cha Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 kinakataa dhana hii. Kifungu hicho kinasema kuwa: “Dereva wa gari au trela ambaye bila sababu za msingi ataendesha kwa mwendo mdogo (low speed) ambao ...

Read More »

Historia ya Sikukuu ya Valentine’s Day (3)

Wiki iliyopita katika makala hii inayomhusu mwasisi wa Siku ya Wapendanao, Mtakatifu Valentino, iliishia pale ambapo katika kila barua aliyokuwa anaandika aliweka maneno  “Ndimi Valentino wako.” Maneno hayo yakawa ni kielelezo cha upendo wa Mtakatifu Valentino kwa watu wote kuwa yeye aliishi na kufa kwa ajili ya kuwapenda watu wote kama Kristo alivyosema: “Amri yangu ndiyo hii: Mpendane kama nilivyowapenda ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (16)

Mwanzo ni mtihani, mwanzo mgumu, lakini lisilowezekana linawezekana. Mwanzo wa ngoma ni lele, mambo yote makubwa huanzia madogo. Mwandishi wa vitabu vya hadithi wa Uingereza, John Creasy, alipata barua 753 za kukataa kuchapisha vitabu vyake na wachapishaji wa vitabu kabla ya vitabu vyake 564 kuchapishwa. Methali ya Kiswahili inasema ukweli wote: “Mwanzo huwa na usiri, ikawa mkaragazo.” Kila mwanzo wa ...

Read More »

Nani katuloga?

Wiki iliyopita Kampuni ya Mwananchi ilifanya jambo la maana sana. Iliandaa mjadala muhimu sana uliohusu athari za biashara na matumizi ya mkaa nchini. Nasikitika kutoshiriki mjadala huo. Hizi picha zinazoonekana hapa nilizipata wiki mbili zilizopita bila kujua kungekuwapo mjadala wa aina hiyo. Laiti kama ningejua, nina hakika ningepata nzuri zaidi. Picha hizi ni tone ndani ya bahari. Wote hawa wanaoonekana ...

Read More »

Hekima na busara zitawale wasanii (2)

Siti alikuwa maskini wa sura lakini tajiri wa sauti. Alikuwa kinanda Afrika Mashariki na watu wakampenda. Alikuwa na kinywa cha mbubujiko mkubwa wa muziki. Alighani katika taarabu kwa miaka thelathini. Alitumia ulimi wake kuvuta walio mbali kumsikiliza na wa karibu kumzungumza. Majivuno na makeke yalikuwa haramu kwake. Maneno na sauti yake murua yalikuwa kama ua la waridi katika umbo la ...

Read More »

Yah: Tanzania ilikuwa nyumba ya amani Afrika

Nimekumbuka kuna siku nilisikia kwamba vita ya uchumi sasa hivi ni kubwa na inapiganwa sana duniani baina ya nchi na nchi, vita hii ina lengo la kumiliki njia za uchumi kwa mataifa mbalimbali ili kuweza kuendelea kwa mataifa machache na mengine kubaki maskini, dhana hiyo haikumaanisha vita dhidi ya uhai wa watoto ambayo taifa letu limejikita. Nimeshawishika kuandika waraka huu hivi sasa ...

Read More »

Yanga yaweka ubingwa rehani

Na Khalif Mwenyeheri Yanga imeshindwa kupata matokeo mazuri katika mechi zake za hivi karibuni na kuifanya timu hiyo kupunguza nafasi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), hali hiyo inawafanya Yanga kuwa na kazi kubwa ya kufukuzia ubingwa. Katika msimamo wa ligi, Yanga inaongoza ligi baada ya kujikusanyia alama 55, katika mechi 22, huku Azam ikishika nafasi ya pili baada ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons