Monthly Archives: March 2019

Most Noticeable Dating Online

Dating Online Secrets That Nobody Else Knows About Teaming up with a person on the world wide web is alright but you have to be truthful regarding the reason. As talking on the web is the principal sort of communication it is perfectly alright to send an email to this person who has the copy motives. When you talk to ...

Read More »

the Brand New Angle On Fun Just Released

Afternoon snacks will be furnished throughout the week. Simply speaking, it felt the same as being a recipe for a amazing party full of fun wedding thoughts. Sure, some folks just have lousy taste. In order have the ability to inspire individuals who create stuff, HBS students will require to understand to empathize with people who do it now. Making ...

Read More »

Polisi ‘yamtimua’ askari aliyekamata mihadarati

Jeshi la Polisi limemtimua kazi askari wake, Manga Msalaba Kumbi, mwenye namba F. 5421, kwa kile kinachodaiwa ni mwenendo mbaya kazini. Askari huyo alikuwa anafanya kazi mkoani Mwanza. Uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini kwamba askari huyo alikumbwa na masahibu hayo baada ya kukamata mihadarati inayohusishwa na ‘wakubwa’ ndani ya Jeshi la Polisi. Akizungumza na Gazeti la JAMHURI, askari huyo ...

Read More »

Maji ya visima hatari Songea

Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa Songea, Mkoa wa Ruvuma wamo hatarini kupata ugumba na saratani kutokana na kutumia maji yenye kinyesi cha binadamu kwa miaka 16 baada ya kuchimba visima karibu na vyoo, JAMHURI limebaini. Uchunguzi wa gazeti hili uliohusisha, pamoja na mambo mengine, kuwahoji wananchi 123 wa kata mbili, Ruvuma, yenye wakazi 15,706 ambako Mamlaka ya Maji Safi na ...

Read More »

Aliyepigwa risasi Ikulu Ndogo kuburuzwa kortini

Mtu mmoja aliyepigwa risasi na polisi akiwa maeneo ya Ikulu Ndogo inayotumiwa na Makamu wa Rais jijini Mwanza atafikishwa mahakamani baada ya matibabu. Raia huyo amelazwa Hospitali ya Rufaa mkoani hapa ya Sekou Toure akiendelea kuuguza jeraha la risasi mwilini mwake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro, amelithibitishia Gazeti la JAMHURI akisema tukio hilo limetokea Machi 11, 2019 ...

Read More »

Utulivu uendelee vyama vya siasa

Katika siku za karibuni uwanja wa siasa nchini umeshuhudia matukio makubwa. Ni matukio yenye kuzua mjadala na kimsingi, unaweza kusema ni matukio ambayo kwa sehemu kubwa yamevuruga mikakati ya vyama vya siasa kwa ujumla wake, mikakati kati ya chama kimoja dhidi ya kingine na hata mikakati kati ya mwanasiasa mmoja hadi mwingine. Matukio haya yanahusu baadhi ya wanasiasa wenye majina ...

Read More »

NINA NDOTO (12)

Ongeza thamani kwa ukifanyacho Mchezaji bora katika timu si yule mwenye umri mkubwa zaidi ya wachezaji wengine au aliyeitumikia timu kwa muda mrefu, bali ni yule mwenye thamani.  Ndiye hulipwa zaidi ya wote. Thamani ni gharama au ubora wa kitu kutokana na hali na kuhitajika kwake kwenye jamii.  Kila  unachokifanya kitakulipa kuendana na thamani unayoitoa. Ukiwa kazini usifikiri kwamba unalipwa ...

Read More »

Hofu ya Chadema sheria mpya ya vyama vya siasa

Katika taarifa kwa umma, Machi 22, 2019, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefanya uchambuzi wa sheria mpya ya vyama vya siasa iliyotiwa saini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni kama ifuatavyo: Tumeiona Sheria mpya ya Vyama vya Siasa ambayo imesainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, Februari 13, 2019 na kuchapwa ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (7)

Leo naandika makala hii nikiwa hapa Bukoba. Nimesafiri kutoka Dar es Salaam hadi Bukoba kwa kutumia usafiri wa gari dogo (IST). Kauli aliyopata kuitoa Rais John Pombe Magufuli kuwa ipo siku mtu atasafiri kwa teksi kutoka Mtwara hadi Bukoba, hakika ni ya kweli. Waswahili wanasema: “Baniani mbaya, kiatu chake dawa.” Sitanii, hakika Rais Magufuli anajenga miundombinu. Mikoa yote niliyopita, Pwani, ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (22)

Hatuoni ingawa tunatazama Kuona ni mtihani. Si kila jicho lililofunguka linaona. Na si kila jicho lililofumbwa limelala. Kila mtu anatazama lakini si kila mtu anaona. Kuona ni mtihani. Je, unapotazama unaona? “Hatuoni vitu kama vilivyo, tunaviona kama tulivyo.” (Anais Nin). Kwa msingi huo, kuona ni mtihani. Mfinyanzi atauona udongo kama kitu cha kumsaidia kutengeneza vyungu, kutegemea fani yake. Mkulima atauona ...

Read More »

Ndugu Rais, Jaji Mkuu Samatta ametoa tamko

Ndugu Rais, ndivyo alivyo Mwenyezi Mungu; huwatuma watu wake wema walio kati ya watu wake kuwafikishia ujumbe watu wake walio kati yao. Wenye masikio ya kusikia husikia, bali wenye viburi Bwana huwaadhibu kwa mwisho wao wa aibu. Nukuu katika kitabu cha Mwalimu Mkuu wa Watu inasomeka kuwa Bwana Mageuzi alisema madhara yangekuwa makubwa zaidi kama si kwa ubunifu na busara ...

Read More »

Rais Magufuli wasaidie wanyonge hawa

Jumamosi iliyopita nilikuwa jijini Arusha. Nikiwa nimeegesha gari kwa ajili ya kupokea simu, nikamwona mama aliyeonekana mwenye mawazo mengi. Hakuwa na furaha usoni. Hapa ni jirani na Uwanja wa Ndege wa Kisongo. Sikuhitaji kumuuliza maswali mengi. Nilichofanya baada ya kumtazama, nilimwita. Akasogea akionekana mwenye shaka nyingi. Nilimuuliza anakokwenda. Akajibu kuwa anakwenda Soko la Kilombero ambako anauza mbogamboga. Kwa namna nilivyomwona ...

Read More »

Mgeni mpe mchele na panza

Mgeni ni mtu aliyetembelea eneo fulani kwa mara ya kwanza. Ni mtu anayepewa dhamana ya kuwa mtu muhimu, na aghalabu hupewa jukumu la kutekeleza shughuli rasmi inayofanyika. Mgeni ni mtu asiye na uelewa wa kutosha au ueledi katika fani fulani. Tunaweza kusema ni mwanagenzi. Mimi na wewe tunamfahamu mgeni anavyopewa heshima, thamani na huba wakati wa mapokezi na mwenyeji wake. ...

Read More »

Yah: Tunabadilika kwa kasi

Nianze na salamu kama mtu muungwana, maana itakuwa si busara kukurupuka na mawazo yangu kichwani bila kuwajulia hali. Najua kuwa si kila mtu yuko sawa kichwani, hasa katika kipindi hiki cha mpito wa mabadiliko ya mambo mengi, hasa yale yahusuyo mifuko yenu, natoa pole. Salamu zangu zingine, tena za kipekee kabisa nazituma kwa wale ambao hawajatetereka katika kipindi hiki cha ...

Read More »

Diamond Plutnumz shujaa asiyechoka

Msanii wa kizazi kipya, Diamond Platnumz (pichani), ambaye ‘nyota’ yake inaendelea kung’aa kwa kuingiza pesa lukuki kutoka katika maonyesho yake amekuwa akipata mialiko mingi ndani na nje ya nchi, ambako hulipwa ‘kitita’ kizuri cha pesa. Mara baada ya kuzaliwa Oktoba 2, 1989 katika Hospitali ya Amana, jijini Dar es Salaam, alipewa majina ya Nasibu Abdul Juma. Kwa bahati mbaya hakupata ...

Read More »

Babu Miura bado anakiwasha

Ng’ombe hazeeki maini, Waswahili ndivyo wanavyosema. Kazuyoshi Miura, ndiye anayetajwa kuwa mchezaji wa soka mwenye umri mkubwa zaidi duniani. Inaelezwa kuwa licha ya kuwa na umri wa miaka 52, bado anasakata kabumbu katika timu ya Yokohama inayoshiriki Ligi Kuu nchini Japan. Miura pia anafahamika kwa jina la ‘King Kazu’, kutokana na kucheza miondoko ya ‘kazu’ pindi anapofunga magoli. Miura ni ...

Read More »

Wagombea msikiti aliojenga Nyerere

Waumini wa Kiislamu katika Kijiji cha Butiama na uongozi wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mara wamo kwenye mgogoro kuhusu umiliki na uendeshaji wa msikiti uliojengwa kwa msaada wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kijijini hapo. Msikiti huo ulianza kujengwa wakati Mwalimu akingali hai, na ulifunguliwa rasmi na aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk. Omar Ali Juma, ...

Read More »

Mapya sakata la korosho

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mikoa ya Lindi na Mtwara, Zuberi Ally Maulid, amefichua kinachoendelea kuhusu wakulima kurudishiwa korosho zinazodaiwa ni mbovu. Kwa mujibu wa kiongozi huyo ambaye amewahi kuwa mbunge ndani ya Bunge la Tanzania, hali si shwari katika mchakato wa ununuzi na malipo ya korosho. Katika mazungumzo yake ...

Read More »

Gari la Polisi ladaiwa kuua bodaboda Segerea

Gari la Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linadaiwa kuua dereva wa pikipiki, Cosmas Swai (42), kwa kumkanyaga kichwani akiwa amembeba mkewe, Anna Swai (39) pamoja na mwanawe, David Swai (11). Ajali hiyo imetokea Machi 12, mwaka huu, eneo la Segerea Mbuyuni, baada ya mashuhuda wa ajali hiyo kudai kuwa gari hilo ...

Read More »

Namna ya kukomesha ubambikaji kesi Polisi

Wiki iliyopita katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa miaka mingi, Jeshi la Polisi Tanzania limekuwa miongoni mwa taasisi za kitaifa zilizothibitisha kuwa chombo hicho kimewahi kuhusika kubambikia baadhi ya wananchi kesi. Baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kudai kuwa Jeshi la Polisi kupitia kwa baadhi ya askari wake walimbambikia kesi mmoja wa wafanyabiashara mkoani Tabora, Jeshi la Polisi kupitia kwa ...

Read More »

NINA NDOTO (11)

Ukiamua kufanya, fanya kweli   Fanya mambo kwa ubora. Chochote unachokifanya hakikisha unakifanya vizuri  na kwa ubora wa hali ya juu; kiasi kwamba watu wakikiona wawe tayari kuwaambia wengine kuhusu wewe. Hata mimi nikiona kazi yako unaifanya kwa ubora nitakuwa tayari kuwaambia wengine na kutoa sifa bora juu yako wewe, hii imekuwa tabia yangu. Watu wanapenda ubora, watu wanapenda vitu ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (6)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii kwa aya hii: “Kumbuka kuna biashara zina leseni zaidi ya moja, hivyo kama nilivyosema kabla ya kuanzisha biashara, unapaswa ufanye utafiti kufahamu aina ya biashara unayotaka kuifanya, eneo unalopaswa kufanyia, aina ya wateja, aina za kodi, leseni na mengine mengi. Ikumbukwe hapa nazungumzia mtu aliyechagua kuanzisha biashara kama mtu binafsi, hapa sijazungumzia jina la biashara ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons