Daily Archives: March 12, 2019

Magufuli kutua China

Rais Dk. John Magufuli kwa mara ya kwanza anatarajiwa kuvuka mipaka ya Bara la Afrika, kwa kuitembelea China kwa ziara ya kiserikali, Gazeti la JAMHURI limebaini. China imekuwa mdau muhimu wa maendeleo wa Tanzania, kupitia mkakati mahususi wa Tanzania ya viwanda, wawekezaji kadhaa kutoka nchi hiyo ya barani Asia wameitikia wito kwa kuanzisha viwanda kadhaa hapa nchini. Vyanzo vyetu vinasema ...

Read More »

Katavi, Tabora vipi?

Mpita Njia ameshitushwa na taarifa za hivi karibuni kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshika nafasi ya tatu barani Afrika katika ndoa na mimba za utotoni. Hizi si tu ni taarifa za kushitua, bali ni taarifa za aibu katika wakati huu ambao Serikali ya Awamu ya Tano inajielekeza katika kuhimiza elimu kwa wote, kiasi cha kuondoa malipo ya ada. Hili ...

Read More »

Ajali ya ndege yaua abiria wote

Watu wote 157 waliokuwa safarini katika ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia,  Boeing 737, wamepoteza maisha baada ya ndege hiyo kuanguka. Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa kuelekea mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Jumapili iliyopita. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ethiopia, abiria waliokuwamo kwenye ndege hiyo ni 149 na watu wengine wanane ...

Read More »

Mjamzito afanya Mtihani wa Taifa, afaulu

Shule ya Filbert Bayi iliyopo Kibaha, mkoani Pwani, mwaka jana iliruhusu mwanafunzi mjamzito kufanya mtihani wa taifa wa kuhitimu Kidato cha Nne. Mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) alifanya mtihani huo kwa namba S 1437/0002 katika matokeo ya mtihani yaliyotangazwa Januari mwaka huu, alifaulu kwa kupata daraja la pili lenye alama 20 (Division II, 20). JAMHURI limeelezwa wakati anakutwa na mimba hiyo ...

Read More »

Wawekezaji wamchongea DC kwa Rais

Uamuzi wa wawekezaji wilayani Hai, Kilimanjaro kumshtaki mkuu wa wilaya (DC) hiyo kwa Rais John Magufuli umepongezwa na baadhi ya wafanyabiashara na kuonekana kuwa ni mwanzo wa kumaliza vitendo vya kunyanyaswa. DC wa Hai, Lengai ole Sabaya, anatuhumiwa na wawekezaji hao kuwa anawanyanyasa kwa kuwakamata, kuwaweka ndani na kuwaomba rushwa. Kilio chao kilichowekwa kwenye maandishi, kimewasilishwa kwa Rais Magufuli, ambaye ...

Read More »

Maji ni kichocheo cha maendeleo

Wiki ya Maji ni fursa maalumu ya sekta ya maji nchini kujitathmini kwa kujilinganisha na nchi nyingine duniani katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya maji. Maji ni kichocheo muhimu cha maendeleo katika sekta mbalimbali za uchumi hapa nchini, ikiwemo kilimo, biashara, utalii na viwanda. Katika kutambua umuhimu na thamani ya maji katika maisha ya binadamu na uchumi wa dunia ...

Read More »

Tanzania tunao wajibu wa kuziokoa Rwanda, Uganda

Fukuto la kutokea mfarakano na hata umwagaji damu linaendelea kati ya Uganda na Rwanda. Lakini pia kuna msuguano mkubwa wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Burundi. Mataifa haya matatu ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hii ina maana kwamba jambo lolote baya katika mataifa hayo lina athari kwa nchi wanachama, hasa Tanzania. Tanzania ni mwathirika mkuu kwa sababu tunapakana ...

Read More »

NINA NDOTO (10)

Maono humfanya dhaifu awe imara   Maono hubebwa katika vitu vitatu muhimu. Mosi, uwezo wa kuona mbele. Pili, uwezo wa  kuona kwa undani. Tatu, uwezo wa kuona nyuma. Uwezo wa kuona mbele ni sawa na kuona kwa kutumia darubini. Darubini ni chombo  kinachofanya vitu vilivyo mbali vionekane karibu. Kila mtu na uwezo wa kuona mbali, lakini ni wachache tu wameamua ...

Read More »

Wizara ya Maji yataka wahandisi wazalendo

Serikali inaweka nguvu katika sekta ya maji ili kuhakikisha wananchi katika maeneo yote ya nchi wanapata huduma ya maji safi, salama, ya uhakika na yenye kutosheleza. Wajibu huu wa serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kwa Watanzania wote, bila kubagua itikadi au eneo. Aidha, sera ya maji ya mwaka 2002 inaelekeza wananchi kupata huduma ya maji safi na ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (5)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala yangu kwa kuzungumzia ukadiriaji wa mapato/mauzo/mzunguko, kiwango ambacho hutumika kumkadiria kodi ya mapato mfanyabiashara. Kabla sijaendelea, yametukuta tena. Mtangazaji maarufu nchini, Ephraim Kibonde, amefariki dunia. Kibonde, ndiye alikuwa mwendesha shughuli ya maziko ya Ruge Mutahaba huko Bukoba, sasa naye amefariki dunia. Naipa tena pole familia ya Clouds na wanahabari wote hapa nchini. Ni habari mbaya, niko ...

Read More »

Kupata hedhi isiyokoma inaashiria tatizo

Ni kawaida kwa mwanamke aliyepevuka kupata hedhi ya kila mwezi katika mzunguko wake kutokana na mabadiliko ya homoni, ambapo mfuko wa uzazi unatengeneza ukuta mpya kwa ajili ya mapokezi ya utungishwaji wa mimba. Kwa kipindi hicho mwanamke anapitia siku kadhaa za utokwaji wa damu kupitia uke. Idadi ya siku hizi imetofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine, kulingana na mfumo ...

Read More »

Sao Hill: Mgodi wa miti

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuandika makala hii kuhusu Kiwanda cha Sao Hill cha kuchakata magogo ili kupata mbao na bidhaa nyingine zitokanazo na miti au rasilimali misitu. Kiwanda cha misitu – Sao Hill Industries Ltd – ni miongoni mwa viwanda vya mazao ya misitu vilivyokuwa vinamilikiwa na serikali kupitia Shirika la Viwanda vya Misitu lililokuwa likijulikana kama ‘Tanzania Wood ...

Read More »

Rais Magufuli: Tunawapenda, tuwahitaji wawekezaji na wafanyabiashara

Hotuba ya Rais John Magufuli kwenye hafla aliyoindaa kwa ajili ya mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa kukaribisha mwaka mpya 2019 Ikulu, Dar es salaam; Machi 8, 2019   Mheshimiwa Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki;   Mheshimiwa Ahamada Fakih, Balozi wa Muungano wa Visiwa Vya Comoro na Kiongozi wa Mabalozi nchini; ...

Read More »

Mikasa ya maisha ya Kingunge

Kwa mara ya kwanza, Kavazi la Mwalimu Nyerere limechapisha kitabu kuhusu maisha ya mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale – Mwiru. Kitabu hicho kimezinduliwa Machi 6, wiki iliyopita, kikiitwa ‘Kutoka Kavazini – Mazungumzo na Kingunge wa Itikadi ya Ujamaa. Kingunge Ngombale – Mwiru 1930 – 2018.’ Kitabu hicho kimetokana na mazungumzo kati ya Kingunge enzi za uhai wake na Profesa Issa ...

Read More »

Ndugu Rais umesema wanao tumekusikia

Ndugu Rais, ukifanya vema lazima tukuambie umefanya vema. Ukiwaapisha makamishna wa Polisi, Ikulu jijini Dar es Salaam, baba ulisikika ukisema, “…Lakini kuna mambo mengine tu ambayo ni ya kawaida ambayo Jeshi letu la Polisi mnatakiwa myaelewe kwamba Watanzania siyo wajinga sana. Wanafahamu na wanajua ‘kuanalaizi’ mambo.’’ Kwa kulitambua hili baba, Mwenyezi Mungu akutangulie katika kutuongoza. Ukaendelea, “Niwatolee mfano tu alipotekwa ...

Read More »

Jumuiya ya Afrika Mashariki inayumba

Hali ya kutoelewana iliyopo kati ya Rwanda na Uganda, nchi mbili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, inatishia utangamano wa jumuiya hiyo. Uhasama kati ya nchi hizi mbili ni wa muda mrefu na umewahi kusababisha mapambano ya silaha kati ya majeshi yao ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Zipo tuhuma kutoka kila upande kwamba kuna njama za kushawishi ...

Read More »

Huwezi kubadili hatimiliki kama una mkataba serikali za mitaa

Hapo awali niliandika  namna  sheria isivyowaruhusu viongozi  wa  serikali  za mitaa  (watendaji kata, wenyeviti wa mitaa, wajumbe, na ule uongozi wote wa huko chini) kuandaa  na  kusimamia  mauzo  na manunuzi  ya nyumba au viwanja, kwa ujumla ardhi. Nikasema kuwa kitu hicho  hakiruhusiwi  katika  sheria  na wanaofanya  hivyo wako  katika  makosa  makubwa. Asilimia kumi wanayowatoza ni makosa na ndiyo maana hailipwi ...

Read More »

Tuyapende mazingira

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anasema: “Dunia ni makazi yetu ya pamoja.” Mwalimu na gwiji wa theolojia wa Kanisa Katoliki, Yohane Krisostom, naye anasema: “Dunia imeumbwa na Mungu ili kumtunza mwanadamu.” Jamii yoyote ile inayopuuza mustakabali mwema wa mazingira na uumbaji wake, ni jamii isiyojijali na isiyojali hatima ya vizazi vyake. Uharibifu wa mazingira ni aina mpya ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (20)

Kujikosoa ni mtihani, unapowanyoshea wengine kidole, vitatu vinakuelekea wewe na  kidole gumba kinasema Mungu ni shahidi. Kwa msingi huu kujikosoa ni mtihani. “Si namna tunavyofanya makosa kunakotutambulisha bali namna tunavyoyasahihisha,” alisema Rachel Wolchin. Kuna kitendawili kisemacho: “Kipo lakini hukioni.” Jibu ni ‘kisogo’. Kama kisogo kipo lakini hatukioni, kuna makosa yetu yapo lakini hatuyaoni. “Macho yangu nitazame na mimi pia.” Ni methali ya ...

Read More »

Siasa zisiwagawe mama zetu

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake yalifikia kilele wiki iliyopita. Shamrashamra zilikuwa nyingi karibu maeneo yote ndani na nje ya nchi. Wanaotambua na kuthamini utu wa mwanamke, kwao hadhi ya mwanamke iko palepale muda wote. Hawasubiri siku maalumu kulitambua au kulionyesha hilo. Mkoani Geita kuna tukio lililonishawishi kuandika haya ninayoandika leo. Si jambo zuri kwa umoja na mustakabali wa mama zetu. ...

Read More »

AINA TATU ZA SWALI Elekevu, jinga na pumbavu 

Mimi naamini mazungumzo yoyote kati ya mtu na mtu (au watu) yana maana na madhumuni yake. Yanapata uimara na thamani ya maana yanapojengewa maswali yenye nguvu ya hoja na kupata majibu yaliyosheheni ukweli na usahihi. Mazungumzo, maswali na majibu hayana budi kulandana kukidhi hoja husika kati ya mtu na mtu (au watu). Mazungumzo yasipopatiwa ustahamilivu na ukweli hayawezi kutimiza lengo na ...

Read More »

Yah: Kwanini viongozi wengi hawakufanana na Ruge?

Naandika waraka huu nikiwa najua fika kwamba kuna majonzi juu ya majonzi kwa watu wengi, hasa tasnia ya habari hapa nchi. Wengi wamesikia misiba na ambao hawajasikia ni vema wakajua sasa hata kwa kuuliza. Naandika waraka huu nikiwa na maswali mengi sana kichwani mwangu, najiuliza nimuulize nani lakini simuoni, nafikiri ni vema nikajiuliza mimi mwenyewe, Ruge ni nani? Nani alikuwa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons