Ngorongoro inavyotafunwa
Wakati Rais Dk. John Magufuli akihimiza kubana matumizi ya idara na taasisi za serikali, hali ni tofauti kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Shilingi bilioni 1.1 zimetumika kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 kuhudumia vikao vya bodi hiyo. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, bodi imekaa vikao 20 tofauti na utaratibu…