Monthly Archives: April 2019

Hatua kubwa miaka 55 ya Muungano

Aprili 26, mwaka huu taifa litaadhimisha miaka 55 tangu kuasisiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Umri huo wa miaka 55 ya Muungano si haba, changamoto na mafanikio kadhaa yamekwisha kujidhihirisha na kubwa zaidi kwa upande wa mafanikio kuimarika kwa mshikamano baina ya raia wa pande hizo mbili za Muungano. Serikali zote mbili, yaani ...

Read More »

Funzo miaka 25 mauaji ya Rwanda

Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yametimiza miaka 25. Huu ni umri wa mtu mzima na hili linajionyesha wazi kule Rwanda, asilimia 60 ya watu wa Rwanda ni vijana na wengi wao ni miaka 25 na kwenda chini. Wengi wamezaliwa baada ya mauaji haya ya kinyama. Aprili 7, 2019 Rwanda ilifungua siku mia moja za maombolezo ya kumbukumbu ya miaka 25 ...

Read More »

UJENZI GATI JIPYA LA MAGARI BANDARI YA DAR WAFIKIA ASILIMIA 50

Kazi ya utekelezaji wa ujenzi wa Gati mpya kwa ajili ya kuhudumia Meli za magari (RoRo Berth) kwenye Bandari ya Dar es Salaam imefikia asilimia 50 na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2019. Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema mbali na kukamilika kwa ujenzi wa Gati hiyo unaotarajiwa kukamilika katikati ya 2019, kazi ya kuboresha Gati namba ...

Read More »

Watanzania tunaepushwa mengi

Matukio ya hivi karibuni ya nchini Sudan yanatukumbusha umuhimu mkubwa wa dhana ya kung’atuka, neno la Kizanaki lililoingia kwenye msamiati wa lugha ya Kiswahili na ambalo husikika pia kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Raia wa Sudan wamekuwa kwenye kipindi cha miezi kadhaa ya maandamano ya kushinikiza serikali yao kuachia madaraka na kuanzisha mchakato wa kurudisha utawala wa kiraia. Maandamano ...

Read More »

Haki za mtuhumiwa mbele ya polisi

Mtuhumiwa ni nani? Ni mtu yeyote anayewekwa chini ya ulinzi na polisi au chombo cha usalama kwa kutuhumiwa kufanya kosa la jinai. Makosa ya jinai ni yapi? Ni makosa ambayo mtu akipatikana na hatia hupewa adhabu. Ni makosa kama wizi, ubakaji, mauaji, kufanya makosa ya kuhatarisha amani na mengine ya namna hiyo. Haki za mtuhumiwa Mtuhumiwa anapowekwa chini ya ulinzi ...

Read More »

Ndugu Rais maneno makali ni maneno gani hayo?

Ndugu Rais, wapo wanaosema kuna maneno ambayo ni makali. Ni yapi hayo maneno makali? Ukali wake upo kwa namna yanavyotamkwa kwa ukali au ukali wake uko katika maneno yenyewe kuwa hata ukiyatamka kwa upole yanabaki kuwa makali? Kwamba, hata yakiwa yenyewe kama ni kitabuni au wapi yanakuwa makali. Maneno makali ni yapi? Ukimwambia timamu ambaye si dhaifu kuwa ni dhaifu, ...

Read More »

Epuka kuishi maisha ya majivuno (3)

Fumbua macho yako utazame. Tazama upya uhusiano wako na Mungu wako. Tazama upya uhusiano wako na mke/mume wako. Tazama upya uhusiano wako na watoto wako. Tazama upya uhusiano wako na majirani zako. Tazama upya uhusiano wako na kazi yako. Tazama upya uhusiano wako na wafanyakazi wenzako. Baada ya kutazama umebaini nini? Je, umebaini kasoro za kiuhusiano? Jifunze kumwomba msamaha aliyekukosea ...

Read More »

Kupenda si kazi, kazi ni kumpata akupendaye

Kupendwa ni mtihani.  Kupenda ni kujiweka katika hatari ya kutopendwa. Lakini hatari kubwa ni kutojiweka katika hatari. Kupenda si kazi, kazi ni kumpata akupendaye. Kuna methali ya Wahaya isemayo: “Mwereka wa mzazi unaomwangukia mtoto, si mwereka wa mtoto unaomwangukia mzazi.” Mzazi anajitaabisha kukidhi mahitaji ya mtoto, lakini baadaye mtoto hajitaabishi kukidhi mahitaji ya mzazi. Kwa msingi huu kupendwa ni mtihani. ...

Read More »

Uhuru una kanuni na taratibu zake

Uhuru ni uwezo au haki aliyonayo mtu binafsi, jumuiya au taifa ya kujiamulia mambo yake kwa hiari yake bila kuingiliwa na mtu au taifa jingine. Kuna uhuru wa mtu binafsi, ambao humpa haki ya kuishi akiheshimika sawa na watu wengine. Mtu binafsi huwa na haki ya kutoa mawazo yake, kufuata dini anayoipenda na kushiriki katika uamuzi wa mambo yote yanayohusu ...

Read More »

Yah: Mkuu, huku mbwa atamla mbwa

Kama siku zote ninavyosema salamu ni ada, na ni uungwana kujuliana hali, nawashukuru sana wote wanaonitumia ujumbe wa simu kunieleza yale ambayo yamewakuna. Hata kama litakuwa si jema kwako, naomba unijulishe ili nijue kuwa nimekukera, sisi ni binadamu, hiyo ni hatua ya maisha na lazima niipitie ili niweze kukiri, hakuna binadamu mkamilifu, karibu wote ni dhaifu. Kuimaliza wiki ukiwa salama ...

Read More »

Bodi ya Ligi gumzo

Hali ya soka nchini hususan mwenendo wa michezo ya ligi kuu si ya kuridhisha. Kumekuwa na lawama kutoka kwa wadau wa soka zinazoelekezwa kwa waamuzi wa mechi mbalimbali, lakini kwa upande mwingine, vilevile kumekuwa na malalamiko dhidi ya Bodi ya Ligi Tanzania Bara. Wakati waamuzi wakilalamikiwa  kutokuwa imara na makini katika baadhi ya mechi wanazosimamia, Bodi ya Ligi imekuwa ikishutumiwa ...

Read More »

Ngorongoro inavyotafunwa

Wakati Rais Dk. John Magufuli akihimiza kubana matumizi ya idara na taasisi za serikali, hali ni tofauti kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Shilingi bilioni 1.1 zimetumika kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 kuhudumia vikao vya bodi hiyo. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, bodi imekaa vikao 20 tofauti na utaratibu unaoagiza vikao viwe vinne kwa ...

Read More »

Aibu Mkwakwani

Mpita Njia (MN) anatanguliza salamu zake za Sikukuu ya Pasaka kwa Wakristo wote nchini ambao bila shaka wataungana na wenzao wa maeneo mengine duniani kwa ajili ya siku hiyo ya kiimani kwao. Tukiachana na hayo, kama ilivyo kawaida yake, MN wiki hii alikuwa mkoani Tanga kwa ajili ya shughuli zake za ujenzi wa taifa. Loh! Tanga kuna mengi yaliyo mazuri, ...

Read More »

Mnyukano wa Spika, CAG wapamba moto

Mvutano kati ya Bunge na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, umepamba moto. Kauli iliyotolewa wiki iliyopita na bingwa huyo wa masuala ya ukaguzi wakati akiwasilisha muhtasari wa ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka 2017/2018, imemwibua tena Spika Job Ndugai. Akionekana kukasirika, Spika Ndugai amesema endapo Profesa Assad anaendelea kurudia rudia kauli ya ‘udhaifu’, ...

Read More »

Jiji waomba fursa mabasi 100 ‘mwendokasi’

Uongozi wa Jiji la Dar es Salaam umeiomba Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwapa kibali cha kuongeza mabasi ya usafiri wa haraka (mwendokasi) katika Jiji la Dar es Salaam. Lengo la kuomba kibali hicho ni kutaka kushirikiana na mkandarasi aliyepewa dhamana ya kuendesha mradi huo ili kuboresha huduma ya usafiri ya ...

Read More »

Nondo feki zazua balaa Siha

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) imeanza uchunguzi kuhusu tuhuma zinazoikabili kampuni moja ya uuzaji wa vifaa vya ujenzi mkoani Kilimanjaro, inayodaiwa kuiuzia serikali nondo feki zisizo na ubora. Kampuni hiyo ambayo kwa sasa jina lake tunalihifadhi baada ya mkurugenzi wake kutopatikana, ilishinda zabuni ya kuuza nondo kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Siha ...

Read More »

Tukio la Papa Francis Vatican latikisa dunia

Baba Mtakatifu, Papa Francis, katika hali isiyotarajiwa amebusu miguu ya Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, akimsihi pamoja na wenzake kuhakikisha nchi hiyo hairudi kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe. Papa Francis amemwomba Rais Kiir na makamu wake wa awali, Riek Machar, ambaye ameasi kwa sasa, pamoja na makamu wengine wa rais waliofika Vatican kuheshimu makubaliano waliyotia saini ya kusitisha ...

Read More »

Kauli ya Dk. Bashiru ni mwanga kwa nchi yetu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amezungumza maneno mazito ambayo kwa yeyote anayeitakia heri nchi yetu yamemgusa. Maneno aliyoyasema yanaweza yasiwafurahishe wengi, hasa ndani ya chama chake, lakini huo ndio ukweli wenyewe. Ameonya juu ya mmomonyoko wa haki miongoni mwa wananchi na vyombo vya utoaji haki, na kuonya kuwa mataifa kama Sudan ambayo utawala wake umeangushwa ...

Read More »

NINA NDOTO (15)

Mambo ni mengi muda mchache   “Muda ni kitu tunachokihitaji sana, lakini ndicho kitu tuna  chokitumia vibaya,” anasema William Penn. Siku hizi ukipita mitaani utasikia watu wakisema, “Mambo ni mengi, muda mchache.” Ukweli ni kwamba mambo si mengi wala muda si mchache. “Tatizo la muda linaanzia kwenye matumizi yetu ya muda. Linaanzia kwenye vipaumbele vyetu na jinsi tunavyoutumia. Kila dakika ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (10)

Wiki iliyopita nilieleza kuwa leo nitaeleza wakati wa kuwasilisha maombi ya leseni chini ya kifungu cha 14 unapaswa kuipitisha hatua zipi. Katika sehemu hii ya 10, naomba kufafanua hili. Fomu yako ya kuomba leseni ni lazima ianzie ngazi ya chini kabisa. Sitanii, ngazi hizi ndizo za kufanya uamuzi wa awali wenye madhara makubwa mbele ya safari. Unaanzia ngazi ya kijiji ...

Read More »

Katika kushindwa kuna mbegu za ushindi

Ushindi ni mtihani. Si kila anayepata ‘A’ darasani atapata ‘A’ katika maisha. Si kila anayepata daraja la kwanza kwenye mitihani atapata daraja la kwanza kwenye maisha. Ushindi ni mtihani. Katika kila kushindwa kuna mbegu za ushindi, na katika kila ushindi kuna mbegu za kushindwa. Kauli hii iliwahi kutolewa na mwanadiplomasia na makamu wa 42 wa Rais wa Marekani, Walter Mondale. ...

Read More »

Ndugu Rais wanashangilia tu lakini mioyo yao haiko ‘clear’

Ndugu Rais, serikali ni sawa na mwanadamu. Haiwezekani kila kinachofanywa na serikali kikawa ni kibaya. Yako mazuri yanayofanywa na serikali. Na kuna maovu yanayofanywa na serikali. Hii ni kwa serikali zote – siyo hapa kwetu tu. Timamu hasifii kila jambo linalofanywa na serikali, na wala timamu hakosoi kila jambo linalofanywa na serikali. Timamu hushauri katika kweli na kwa nia njema ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons