Daily Archives: May 7, 2019

Mazito ya Mengi

Mfanyabiashara maarufu nchini na kimataifa, Reginald Mengi, amekuwa na maisha yenye mengi, kuanzia mwenendo wake binafsi na mwenendo wake ndani ya jamii alimoishi. Undani wa maisha yake umejibainisha katika kitabu chake cha hivi karibuni kinachoitwa “I Can, I Must, I Will” chenye kaulimbiu ya “The spirit of success”. Mengi, katika kitabu hicho amepata kukizungumzia kifo, hasa baada ya kufariki dunia ...

Read More »

Lo! Misafara ya wakubwa

Mpita Njia (MN) wiki iliyopita akiwa mdau muhimu wa masuala ya habari nchini aliungana na waandishi wa habari katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. MN amesikia mengi katika maadhimisho hayo. Amesikia vilio vya wanahabari wanaoendelea kujiuliza, mwenzao Azory Gwanda aliyepotea atapatikana lini? Lakini amesikia jambo jingine la aina yake, kwamba serikali iko tayari kushirikiana na ...

Read More »

Mateso magerezani…

Mahabusu 200 waachiwa huru   Mahabusu 201 waliokuwa katika magereza ya wilaya za Musoma, Tarime na Serengeti mkoani Mara wamefutiwa kesi zilizowakabili. Hatua hiyo imekuja baada ya ziara ya ukaguzi ndani ya magereza hayo iliyofanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju; na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, hivi karibuni. Viongozi hao na ...

Read More »

Avamia ardhi ya mwenzake kibabe

Kumeibuka mgogoro wa ardhi katika Kisiwa cha Juma Kisiwani, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, unahusu ekari 26 zinazomilikiwa na mfanyabiashara wa madini, Baraka Chilu; lakini mfanyabiashara wa samaki, Joseph Njiwapori, anadaiwa kulivamia eneo hilo. Serikali ya Kijiji cha Juma Kisiwani imelifikisha suala hilo Polisi Wilaya ya Sengerema. Mwenyekiti wa Kijiji cha Juma Kisiwani, Tibahikana Maharage, ameliambia Gazeti la JAMHURI kuwa Njiwapori ameingia isivyo ...

Read More »

Matajiri wengine waige mfano wa Dk. Mengi

Reginald Mengi, mmoja wa wafanyabiashara wachache wanaotajwa kuwa na moyo wa kuwasaidia binadamu wenzao, hatunaye tena duniani. Tangu taarifa za kifo chake zianze kusambaa wiki iliyopita, mamia kwa maelfu ya waombolezaji – ndani na nje ya nchi – wamejitokeza kutoa ushuhuda wa mema waliyotendewa na mzee Mengi. Kifo chake kimeleta mzizimo mkubwa nchini kiasi cha kuwafanya watu wa kada mbalimbali ...

Read More »

NINA NDOTO (17)

Msamaha si kwa ajili yako bali kwa wengine   Unapokosewa kuwa tayari kutoa msamaha kwa anayekukosea, unapokosa omba msamaha pia. Kusamehe ni jambo lililowashinda watu wengi, ukijenga tabia ya kusamehe wanaokukosea utakuwa umejiondoa katika kundi la wengi. Usiposamehe siku zote utabaki kuishi maisha ya siku za nyuma na si maisha ya sasa. Watu wanaoishi maisha ya siku za nyuma hawawezi ...

Read More »

Sheria ni kama silaha, itumike kwa uangalifu

Katika sifa nyingi zinazohitajika kuwa polisi, sifa moja ambayo haitajwi ni imani ya polisi kuwa kila binadamu ana uwezo wa kuvunja sheria na iwapo bado hajavunja sheria kuna siku atafanya hivyo. Ni sifa inayofanya polisi kuamini kuwa kila raia anayekutana naye anaficha uhalifu ambao polisi anapaswa kuufichua. Ni sifa ambayo inasaidia kudhibiti uhalifu na uvunjifu wa sheria, lakini ni sifa ...

Read More »

Utaratibu wa kuajiri watoto wadogo

Mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 ni mtoto. Kisheria si kosa kumwajiri mtoto. Nataka tuelewane vizuri katika hili. Tunatakiwa kuifahamu sheria. Wengi wanadhani ni kosa kumwajiri mtoto. Wanaposikia kampeni za ajira kwa watoto wanadhani ni kosa na haramu kabisa  kumwajiri mtoto. Ndiyo maana nikasema inabidi tuelewane na tuijue sheria ili siku nyingine tunaposikia kampeni hizi tujue zinamaanisha nini. ...

Read More »

Dk. Mengi kwaheri ya kuonana

Najua yameandikwa mengi kuhusu Dk. Reginald Mengi. Dk. Mengi, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni za IPP na Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), amefariki dunia wiki iliyopita. Ni kutokana na kifo cha Dk. Mengi, leo nimeahirisha sehehemu ya 13 ya makala yangu ya ‘Jinsi ya Kuanzisha Biashara Tanzania’. Nilifanya hivyo walipofariki dunia Ruge Mutahaba na Ephraim Kibonde, kama ...

Read More »

Mwalimu Nyerere angekuwepo angesemaje?

Namshukuru Mungu nimeweza kuketi kuandika kumkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kipindi hiki cha kumbukizi ya kuzaliwa kwake na kujiuliza swali ambalo bila shaka Watanzania wengine nao wamekuwa wakijiuliza: Mwalimu angekuwapo akaona utendaji wa Rais John Pombe Joseph Magufuli kwenye Awamu hii ya Tano, angesemaje? Watanzania tuliokuwapo Awamu ya Kwanza tulishuhudia uongozi uliotukuka wa Mwalimu Nyerere. Mwalimu ...

Read More »

Kutokujiandaa ni kujiandaa kushindwa

Kujiandaa ni kujiandaa kushinda na kutokujiandaa ni kujiandaa kushindwa. Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln (1809 – 1865) anasema: “Ukinipa saa sita ili niukate mti, nitatumia saa nne za awali kuliona shoka langu.” Hii ni busara inayoonyesha umuhimu wa kujiandaa. Dunia inamilikiwa na watu waliojiandaa kuimiliki. Huwezi kuimiliki dunia bila kujiandaa kuimiliki. Eleanor Roosevelt anasema: “Wakati ujao unamilikiwa na ...

Read More »

Unaitambua nguvu ya moja?

Moja ni mtihani. Kuna nguvu ya moja. Anayefunga goli ni mtu mmoja lakini timu nzima inafurahi. Lakini kwa upande mwingine kosa la mtu mmoja linachafua picha ya kundi zima, samaki mmoja akioza wote wameoza. Kuna nguvu ya moja. Kuna uwezekano mkubwa mtu kuidharau moja. Kumbuka mdharau mwiba mguu huota tende. Kuna nguvu ya moja. Okoa shilingi moja, shilingi moja itakuokoa. ...

Read More »

Nawapongeza Mpanju, DPP Biswalo

Miongoni mwa habari zilizopewa umuhimu katika toleo hili inahusu kuachiwa huru kwa mahabusu 201 waliokuwa katika magereza ya wilaya za Musoma, Tarime na Serengeti mkoani Mara. Kuachiwa kwao ni matokeo ya ziara ya ukaguzi ndani ya magereza hayo uliofanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju; Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga na wadau ...

Read More »

Buriani Dk. Mengi

Kifo kimeumbwa, kifo ni faradhi. Kifo ni ufunguo wa kufunga uhai wa binadamu duniani na kufungua maisha ya milele ya binadamu huko ahera (mbinguni). Faradhi na ufunguo umemshukia ndugu yetu mpendwa, Dk. Reginald Abraham Mengi.  Reginald Mengi amefariki dunia. Ni usiku wa kuamkia Alhamisi wiki iliyopita katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu, Reginald alifariki dunia baada ya kuugua kwa ...

Read More »

Yah: Malipo ni hapa hapa duniani

Salamu ndugu zangu wote mliopata baraka ya kuishuhudia Pasaka. Sina hakika, lakini ni kweli kwamba wengi walipenda kufurahia ufufuko wake Yesu Kristo mwaka huu lakini haikuwa hivyo. Wapo ambao waliweka malengo ya miezi sita na mwaka, lakini mipango yao haikuwa na mkataba wa maisha au siha njema na mipango hiyo imevurugika. Vilevile nawatakia mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ...

Read More »

Ndugu Rais tupandishe madaraja

Ndugu Rais, Mei ‘Dei’ ya Mbeya imepita. Wanaotaka kujifunza wataisoma. Lo! Maandamano yalikuwa marefu! Lo, mabango yalikuwa mengi yale, lakini yote yalibeba ujumbe mmoja unaofanana. Ulisomeka: “Tanzania ya uchumi wa kati inawezekana. Wakati wa mishahara na masilahi bora kwa wafanyakazi ni sasa.” Wafanyakazi walisisitiza nyongeza ya mishahara kwa nguvu zao zote kistaarabu. Tunasema kistaarabu kwa sababu katika nchi nyingine hali ...

Read More »

Hapatoshi Wydad vs Esperance

Hatimaye timu ya Esperance de Tunis ya Tunisia na Wydad Casablanca ya Morocco zimefanikiwa kufuzu katika hatua ya fainali ya Klabu Bingwa barani Afrika (CAF Champions League). Esperance wameingia fainali baada ya kuwafunga TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo goli 1-0 katika mechi ya raundi ya kwanza wakiwa uwanja wa nyumbani. Katika mchezo wa raundi ya pili wakiwa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons