CWT kwawaka
Fukuto limezidi kuwa kubwa ndani ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) baada ya gazeti hili kuchapisha taarifa za kuwapo ufujaji wa mali za walimu wiki iliyopita, JAMHURI linathibitisha. Wiki iliyopita JAMHURI lilichapisha orodha ya wafanyakazi waliopewa ajira kwa njia ya upendeleo ndani ya CWT, hali inayotajwa kuwa imefungua ‘kabrasha la madudu’ yanayofanyika ndani ya CWT….