Monthly Archives: July 2019

Simu ‘yamuua’ Naomi

Siku chache baada ya polisi kutangaza kumkamata Hamis Said Luwongo (38), kwa tuhuma za kumuua na kumchoma moto mke wake, Naomi Marijani, taarifa za kina zimeanza kuvuja na inaonekana simu ya mkononi ilichangia kutokea kwa mauaji hayo. Uchunguzi unaonyesha kuwa miaka mitatu iliyopita, familia ya Hamis na Naomi, iliingia katika majaribu ya hali ya juu baada ya wanandoa hao kutiliana ...

Read More »

Tuhuma za rushwa zamtikisa DC Sabaya

Mzimu wa tuhuma za kudai na kupokea rushwa kutoka kwa wawekezaji mbalimbali Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro umezidi kumwandama Mkuu wa Wilaya hiyo, Lengai ole Sabaya. Safari hii DC huyo anatajwa kudai na kupokea rushwa ya Sh milioni 10 kutoka kwa mfanyabiashara Cuthbert Swai ambaye ni mkurugenzi wa hoteli ya kitalii, Weruweru River Lodge. Tuhuma hizi ni mwendelezo wa tuhuma ambazo ...

Read More »

Machungu mgogoro wa ardhi Kwimba

Mgogoro wa ardhi uliodumu miaka mitatu sasa baina ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mahiga na familia ya Dionis Mashiba, Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza, unaonekana kupuuzwa na mamlaka wilayani hapa. Mtanziko huo ulioanza mwaka 2016, unatokana na kile kinachodaiwa kuwa familia ya Mashiba kuingia kwenye eneo la Mwalimu Majenga huku Idara ya Ardhi ikishutumiwa kushindwa kuutatua. Kutokana ...

Read More »

Mradi wa umeme Rufiji rasilimali mpya nchini

Mwishoni mwa wiki iliyopita Rais Dk. John Magufuli alizindua ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa maji wa Mto Rufiji. Mradi huo wa kufua umeme wa Mto Rufiji, mkoani Pwani unatarajiwa kuzalisha megawatt 2,115, kiwango ambacho ni kikubwa zaidi katika historia ya uzalishaji umeme nchini.  Mradi huu wa kufua umeme unatajwa kuweza kudumu kwa miaka 60 na utasaidia kuzalisha umeme ...

Read More »

NINA NDOTO (28)

Tumia kichwa chako vizuri   Kila mtu amezaliwa na kichwa chenye ubongo  kinachoweza kufanya mambo makubwa. Akili aliyopewa mwanadamu ikitumika vizuri inaweza kufanya mambo makubwa na pia kusaidia kutimiza ndoto nyingi. Mtu asiyeweza kutumia akili tunasema amerukwa  akili au ni mwendawazimu. Ni mwendawazimu tu ambaye hawezi kutumia kichwa chake vyema. Ipo wazi kuwa kama wewe hujarukwa akili, basi unawezakufanya mambo ...

Read More »

Nyaraka muhimu unapokabidhiwa gari kutoka bandarini

Hivi karibuni tumeeleza njia rahisi ya kutoa gari bandarini katika makala iliyopita. Njia hizi ni zile ambazo  mteja anatakiwa kuzifuata ili aweze kutoa gari lake bandarini kwa haraka na bila usumbufu. Leo katika makala hii tutaelezea umuhimu wa fomu za Vehicle Discharge Inspection Transfer Tally (VDITT) na ile ya makabidhiano ya gari (Vehicle Hand Over Form) wakati mteja anapopokea gari lake kutoka kwa wakala wa forodha aliyempatia kazi ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (24)

Wiki iliyopita nilihitimisha mada yangu kwa kuhoji iwapo msomaji unafahamu viwango vinavyotozwa kwenye Kodi ya Zuio. Nirudie kukiri kuwa hadi sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inacho kituo kimoja tu cha Elimu kwa Mlipakodi kilichopo Dar es Salaam. Baada ya kuandika makala hii nashawishika kusema TRA wanapaswa kufungua vituo vya aina hii kila wilaya nchini haraka inavyowezekana. Wafanyabiashara wanaonipgia simu ...

Read More »

MIAKA 20 BILA MWALIMU NYERERE

Tunamuenzi vipi?   Kwanza, naomba niwapongeze sana vijana hawa; Mhariri Mtendaji wa Gazeti la JAMHURI Ndugu Deodatus Balile na Naibu Mhariri Mtendaji, Ndugu Manyerere Jackton, kwa tuzo za uandishi bora walizopata mwaka huu kwa kazi zao nzuri sana. Walistahili kabisa tuzo hizo. Naipongeza timu yote ya gazeti hili kwa kazi nzuri wanayoifanya. Kwenye makala zangu ninazoandika kwenye gazeti hili maarufu ...

Read More »

Ndugu Rais umetukumbusha ya Mei Dei Mbeya

Ndugu Rais, kukumbuka tuliyoyaona na kuyasikia Mbeya wakati wa sherehe za Mei Mosi au Sikukuu ya Wafanyakazi ni kujirejeshea huzuni na simanzi mioyoni! Lo! Maandamano yalikuwa marefu yale! Du! Mabango yalikuwa mengi yale, lakini yote yalibeba ujumbe uliofanana. “Tanzania ya Uchumi wa Kati Inawezekana. Wakati wa Mishahara na Masilahi Bora kwa Wafanyakazi ni Sasa’’. Du! Wafanyakazi walitema nyongo. Walisisitiza nyongeza ...

Read More »

Fursa ya kipekee kiuchumi kwako na familia (3)

‘Tuchangie tupate mtaji wa Sh milioni 100’   Mwaka 2004 hadi Mei 2006 nilikuwa nimetumia uwezo wangu wa masoko kusajili dawa ya kiasili ya Dental Formula Power (DFP), ambayo inasaidia kutibu na kukinga meno yasipate magonjwa na kuzuia wazee wabaki na meno yao kinywani yakiwa imara hadi wanaingia kaburini. Basi nikatumia ushawishi kwenye mamlaka za nchi nyingine na Dental Formula ...

Read More »

SADC imepiga hatua kubwa

Mwezi ujao Tanzania itakuwa mwenyeji wa kikao cha kilele cha wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (The Southern African Development Community – SADC) jijini Dar es Salaam. Ni kikao cha 39 kinachofanyika kila mwaka. Historia ya SADC ni sehemu ya historia ya harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, historia iliyoanza na jitihada ...

Read More »

Je, kesi haiendelei kwa kukataa kupokea ‘summons’?

Summons ni wito maalumu wa mahakama. Mara zote unapofunguliwa mashitaka (unaposhitakiwa) hasa mashitaka ya  madai, basi ili uweze kufika mahakamani na kujua mashitaka yanayokukabili yaipasa mahakama kutuma wito maalumu  ambao kwa jina la kitaalamu huitwa ‘summons’. Mara nyingi wito huu unapotumwa baadhi ya watu hukataa kabisa kuupokea na wengine huupokea lakini hukataa  kuusaini.  Zipo sababu tatu ambazo huwafanya watu wasipokee ...

Read More »

Palipo na upendo kuna maisha (2)

Ulimwengu wa leo unahitaji kuhubiriwa namna mpya ya kuishi maisha ya upendo. Ni hatari watu wa ulimwengu kuishi bila upendo. Bila kuishi maisha ya upendo, dunia yetu itageuka kuwa jehanamu. Mungu hutabasamu pale anapoona mwanadamu anaishi maisha ya upendo. Nafsi yako haiwezi kuwa na amani kama haipendi wala kupendwa. Njia bora ya kuishi ni kuishi maisha ya upendo. Namna bora ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (39)

Ukitumia dakika 60 kulalamika, umepoteza saa 1 Kulalamika ni mtihani. Unaweza kulalamika kuwa maua aina ya waridi yana miiba au kusifu kuwa miiba ina maua. Ukitumia dakika sitini ukilalamika, umepoteza saa moja. Kama una muda wa kulalamikia jambo, una muda wa kulitatua. Chukua hatua, ukiua muda ukilalamika muda unaishia kukuua. Chukua hatua, yashughulikie mambo unayoyalalamikia. Tafuta suluhisho. “Usilalamike bali chapa ...

Read More »

Rais Magufuli aandika historia Rufiji

Rais Dk. John Magufuli amezindua rasmi ujenzi wa mradi wa umeme wa maji Mto Rufiji. Mradi huo utakapokamilika utazalisha megawatt 2,115 za umeme. Akizungumza katika uzinduzi huo uliohusisha uwekaji wa jiwe la msingi, Rais Magufuli amesema kufanikishwa  kwa mradi huo ni ukombozi wa Tanzania kiuchumi. Ujenzi wa mradi huo utatekelezwa ndani ya miezi 36 na Sh trilioni 6.5 zote zikiwa ni ...

Read More »

Manabii wa viberenge vya Mlima Kilimanjaro…

Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa miongoni mwa waalikwa kwenye mkutano wa mwaka unaoandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kuwakutanisha wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka pande zote nchini. Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TANAPA wameweka utaratibu huu kwa kutambua kuwa wanahabari wana nafasi ya kipekee kwenye uhifadhi. Kwa kutumia magazeti, majarida, redio, televisheni na mitandao ya ...

Read More »

Istilahi za kisiasa zitumike vema – (2)

Usiku  na  mchana, usalama na utulivu wa nchi unatoweka kwa sababu milio ya risasi na mabomu inarindima. Makazi salama yanavunjwa na miundombinu inabomolewa. Zahanati na vituo vya afya vinapokea majeruhi na wagonjwa wengi kuliko kawaida. Maiti wanazagaa barabarani na hospitalini, maji na vyakula vinapatikana kwa shida, sababu vita ya wananchi wenyewe kwa wenyewe. Baadhi ya nchi duniani zimepata kutumbukia katika madhira ...

Read More »

Yah: Huyu Julius wa Burigi anatafakarisha

Nimelala nikaota njozi mbaya sana kwa kuonyeshwa mtu ambaye namfahamu lakini siye, kuna mtu kasema amka umuangalie Julius yuko mbele yako, nami kwa haraka nikaamka ili nimsimulie tumefikia wapi katika kuenzi yale ambayo alituusia kama taifa. La kwanza kabisa ni kumwambia ile hifadhi ambayo ilikuwa bado haijapandishwa hadhi ndiyo hii tumeipandisha hadhi na leo tunaizindua. Nilipoamka na kukutana na mwalimu ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (8)

Wiki iliyopita katika sehemu ya 7 hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Je! Kutabasamu walijifunza wapi? Au unadhani kuna jamii fulani ilitoka huko ilikotoka na kuwafundisha ishara hizi? Jamii zote walijifunza ishara hizo kabla ya lile gharika la zimwi na walipokimbia wakatoka na ishara hizo ambazo zinaendelea hadi leo miongoni mwa jamii zote duniani. Akaniangalia tena kisha akaendelea:” Endelea…  “Masalakulangwa ...

Read More »

Wasanii wa Tanzania mnakwama wapi?

Maneno ya Kiswahili yaliyotumika kwenye wimbo wa ‘Spirit’ wa Beyonce Knowles uliotoka hivi karibuni yamegusa hisia za Watanzania wengi. Si jambo geni kuyasikia maneno ya Kiswahili yakitumiwa na wasanii maarufu katika nyimbo zao, alikwishawahi kuyatumia Michael Jackson katika wimbo wake wa ‘Liberian Girl’. Hata Nas katika wimbo wa ‘Distant Relatives’ alioshirikiana na Damian Marley, mtoto wa Bob Marley wameyatumia maneno ...

Read More »

Ligi dhaifu, Taifa Stars pia dhaifu!

Emmanuel Amunike! Alipata sifa sana wakati akiwa mchezaji lakini amejikuta akiwa garasa katika kazi ya ukocha. Sitaki kuzungumzia huko alikotoka, lakini ndani ya Taifa Stars ameshindwa kufikia malengo ya waajiri wake, nao wamemtoa kafara. Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, akaamua kuitisha mkutano, lakini ‘wababe’ wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakatuma wawakilishi. Nao walikuwa na ...

Read More »

Alivyouawa

Siku chache baada ya Polisi kuthibitisha kwamba Naomi Marijani ameuawa, uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini kwamba maandalizi ya mauaji yake yalifanyika wiki moja kabla, huku akiishi na mtuhumiwa wa mauaji katika nyumba moja. Uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini kwamba kulikuwepo na misuguano baina ya Saidi (Meshack) Hamis Luwongo na mkewe, marehemu Naomi Marijani. JAMHURI limethibitishiwa pasi na shaka ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons