Daily Archives: July 16, 2019

Ameuawa?

Naomi Marijani (36), mama wa mtoto mmoja, mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam ametoweka katika mazingira yenye utata kiasi cha kujengeka hisia kuwa ameuawa, JAMHURI linaripoti. Hadi leo zimetimia siku 63 tangu Naomi ametoweka katika mazingira yenye kuacha maswali mengi huku polisi wa Kigamboni wakionekana kutolipa kipaumbele suala la kupotea kwake, japo ushahidi wa mazingira unabainisha wazi mtuhumiwa wa ...

Read More »

Busara katika kodi ya ardhi

Hivi karibuni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula, ameonyesha ujasiri zaidi katika kuzibana taasisi na kampuni zenye madeni makubwa ya kodi ya pango la ardhi. Mpita Njia ama MN anatambua ukubwa wa tatizo hilo. Kwa mfano, Mwanza tu, kampuni na taasisi nane zinadaiwa zaidi ya Sh milioni 900. Na katika ziara yake, Naibu Waziri ...

Read More »

HALI YA UCHUMI KWA WATANZANIA

TEC, Bakwata, CCT wafichua mkwamo   Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) wamefichua mambo manane yanayoifanya nchi ishindwe kuwahakikishia wananchi uchumi imara na maendeleo endelevu. Mbali na kufichua aina hizo nane za udhaifu katika uchumi wa taifa, taasisi hizo zimebainisha fursa nane kuu, changamoto tano na aina nyingine nane ...

Read More »

Nchi yapiga hatua zaidi sekta ya afya

Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa kuwa na mashine bora 24 zinazopima makundi ya damu. Mitambo hiyo ya kisasa zaidi ulimwenguni inahusika pia kupima maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwamo homa ya ini na virusi vya ukimwi. Afrika Kusini ndilo taifa la kwanza Afrika kuwa na mashine hizo bora. Aidha, imethibitishwa kuwa, Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika kwa kuwa ...

Read More »

Diaspora wa kwanza duniani walitoka Ngorongoro

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabulla na Meneja Idara ya Urithi wa Utamadani katika Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) katika Bonde la Olduvai, Mhandisi Joshua Mwanduka; wanazungumzia ugunduzi wa Zinj miaka 60 iliyopita na faida zake kwa Tanzania na ulimwengu. Mhandisi Mwankunda Kuadhimisha miaka 60 tangu alipopatikana Zinj ni nafasi muhimu na adhimu katika ...

Read More »

Tumewasikia viongozi wa dini

Mwishoni mwa wiki iliyopita Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) walizindua kitabu chao kinachoelezea namna ya taifa kuendesha uchumi wa soko jamii. Maudhui ya kitabu hicho yamegusa mambo mengi. Kwa mfano, kuhusu mfumo wa uchumi wa soko jamii nchini, wameainisha dhamira ya mfumo huo wa soko jamii kwamba ni ...

Read More »

NINA NDOTO (26)

Nyuma ya pazia   Nyuma ya makala za nina ndoto kuna makala nyingi zilizowahi kuandikwa na hazijawahi kusomwa na mtu yeyote isipokuwa mimi mwandishi. Nyuma ya nyimbo wanazoimba wasanii wengi na tunazisikia zikichezwa redioni na nyingine tumepakua na kuweka katika simu zetu, kuna nyimbo nyingi ambazo ziliimbwa miaka ya nyuma na hatujawahi kuzisikia. Nyuma ya video nyingi za kuchekesha za ...

Read More »

Jinamizi wizi wa magari laibuka

Utata umegubika kuhusu umiliki wa gari la mfanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Moshi, Haika Mawala, lenye namba za usajili T 991 DMS aina ya Toyota Vangurd, baada ya taarifa mpya kuibuka zikidai gari hilo ni la wizi na liliingizwa nchini kwa njia za panya. Gari hilo ni miongoni mwa magari matatu yaliyokamatwa na polisi mkoani Kilimanjaro Septemba 14, ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (22)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii kwa kuuliza maswali haya: “Je, mfanyabiashara unaufahamu mwaka wa kodi wa taasisi au kampuni yako? Unafahamu makisio na taarifa ya mapato ya biashara au shughuli zako yanafanywaje? Usikose sehemu ya 22 kupitia Gazeti la JAMHURI kila Jumanne kupata majibu haya.” Sitanii, niwashukuru tena wasomaji wangu kwa mrejesho mkubwa mnaonipa. Nikiri tena sikufahamu kuwa sekta ya ...

Read More »

Fursa ya kipekee kiuchumi kwako na familia

Naitwa Dk.  Joseph Kankola Buberwa au Dk. JK Buberwa. Ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 50. Ni  Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya JKBRS International Co Ltd yenye ofisi zake jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam. Hivi karibuni nimependekezwa kuwa Mwenyekiti wa Muunganikano wa Wana Maono (Visionaries) duniani, tukiwa ni waanzilishi wa chama hiki. Nimekuwa mtu mwenye maono makubwa kuhusu ...

Read More »

Chuo cha Bandari chemchemi ya wataalamu

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na kumiliki bandari nchini, pia inamiliki Chuo cha Bandari (Bandari College) kilichopo katika Wilaya ya Temeke. Chuo hiki ndicho chemchemi au hazina ya kutoa utaalamu au maarifa ya kuwa na uwezo au umahiri wa kuhudumia meli na mizigo, usimamizi wake na utoaji wa huduma zinazohusiana na shughuli za bandari. Historia ya chuo ...

Read More »

Ndugu Rais, Bashiru Ally ni wa fungu lipi?

Ndugu Rais, fikra za walio timamu hazijadili watu. Hujadili fikra pevu za watu walio timamu. Kwa walio wengi mpaka leo hawajaelewa ilikuwaje mpaka ndugu Bashiru Ally akateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Namfahamu tu kwa mawazo yake ya kufikirisha hasa tulipokuwa tukichangia pamoja hoja mbalimbali katika vyombo vya habari vya kimataifa kama DW, BBC, VOA, Radio France ...

Read More »

Tunaishi maisha halisi au vivuli vya maisha?

Inawezekana leo ninaelekea kujadili mada inayochanganya kidogo. Ili kuijadili vizuri mada hii nitamtumia mwanafalsafa Plato, aliyeona kwa mara ya kwanza ukweli juu ya vivuli na vitu halisi. Na ili kupambana na ulemavu wa fikra, ni muhimu kubungua bongo mara kwa mara. Plato ndiye mwanafalsafa aliyeanzisha Astria ya Pango. Astria hii ndiyo iliyoendelea hadi kuonyesha ukweli kwamba kuna vitu vinavyodumu na ...

Read More »

Jaguar amechemsha, lakini asipuuzwe

Mbunge wa Kenya, Charles Njagua Kanyi, maarufu pia kama mwanamuziki ‘Jaguar’, ametukumbusha ugumu wa kujenga utangamano wa Wana Afrika Mashariki. Jaguar ameamsha zogo hivi karibuni baada ya kutishia kuwavamia wafanyabiashara wa nchi kadhaa ikiwamo Tanzania na Uganda wanaofanya kazi Nairobi na ndani ya Jimbo lake la Starehe na kuwatimua warudi makwao. Tatizo ni kuonekana kwa wafanyabiashara hao kudhibiti baadhi ya ...

Read More »

Palipo na upendo kuna maisha

Palipo na upendo kuna maisha. Somo la kwanza katika maisha ni upendo. Somo la kwanza la kiroho ni upendo. Somo la kwanza la familia ni upendo. Somo la kwanza la uongozi ni upendo. Somo la kwanza la mafanikio ni upendo. Somo la kwanza la ujirani mwema ni upendo. Somo la kwanza la upendo ni upendo. Somo la kwanza la msamaha ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (37)

Wivu unaona tabasamu lako hauoni machozi yako   Wivu ni mtihani. Mwenye wivu haonekani mzuri anapokufanya uonekane mbaya. “Baadhi ya watu watakukataa, kwa sababu tu unameremeta sana kuwazidi. Hiyo ni sawa, endelea kumeremeta,” alisema Nandy Hale. Wivu unaona tabasamu lako, hauoni machozi yako. Wivu unaona kicheko chako, hauoni huzuni yako. Wivu unaona pesa yako, hauoni matumizi yako. Wivu unaona baraka ...

Read More »

Istilahi za kisiasa zitumike vema

Mapinduzi, mageuzi na mabadiliko ni baadhi ya istilahi za kisiasa ambazo kiongozi wa siasa anazitumia katika kushawishi na kuhamasisha wanasiasa wenzake na wananchi kufanya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika nchi yao. Bayana iliyoko ni kwamba istilahi zote hizi zina maana moja ya mabadiliko kisiasa. Ni aina gani ya mabadiliko ambayo kiongozi anataka yawepo kwa kupitia katika chama chake cha ...

Read More »

Yah: Nguvu ya hoja kuwa nguvu ya haja

Nianze na salamu japo si lazima sana kwa kizazi hiki chenye akili nyingi zisizokuwa na matokeo chanya kwa maendeleo ya taifa lao, najua nitalaumiwa sana kwa kauli yangu lakini ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili, nimeamua kusema ili nisemwe lakini ujumbe ufike. Taifa letu limekumbwa na wimbi kubwa la vijana wenye misimamo ya kisiasa bila kujua hatima ya ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (6)

Wiki iliyopita katika sehemu ya tano hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Lile limama lilinichukua likaniangalia kwa makini, likawa linasema: “Kanafanana nasi, umekapata wapi?” Lile litoto likasema: “Nimekaokota huko porini karibu na mpaka wa himaya yetu.” “Sasa unasemaje?” Lile limama likauliza tena litoto nalo likajibu: “Kaache tu mama kaende.” “Nenda ukakaweke kule kwenye mpaka wanakoishi watu wadogo kama yeye.” Haya niliyaelewa ...

Read More »

SKIIBII kafufuka baada ya kujiua kimuziki 

‘Hivi ndivyo mtu mashuhuri hufanya’. Ni jina la wimbo wa msanii wa Nigeria, Abbey Elias, maarufu kama Skiibii Mayana ama Swaggerlee, unaomtambulisha katika soko la muziki nchini humo na pande za dunia kwa sasa. Pamoja na umaarufu ambao umeanza kumvaa kijana huyu kwa sasa, mwaka 2015 hatasahaulika kwa mbinu yake ya kuusaka umaarufu kimuziki kwa kujitengenezea kifo na kutangazwa kwa ...

Read More »

Watanzania wapewa somo

Wadau mbalimbali nchini wametoa maoni yao mara baada ya wiki iliyopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumtangaza Ettiene Ndayiragije kuwa kocha mkuu wa muda wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars. Kocha huyo anachukua mikoba iliyoachwa na raia wa Nigeria, Emmanuel Amunike, ambaye mkataba wake wa kuifundisha timu hiyo ulisitishwa baada ya Stars kutofanya vizuri katika mashindano ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons