Monthly Archives: July 2019

Fuvu la Zinj ni zaidi ya tanzanite

Mhadhiri wa Utalii na Mambo Kale katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Noel Lwoga; na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabulla, wanazungumzia ugunduzi wa Zinj miaka 60 iliyopita na faida zake kwa Tanzania, Afrika na ulimwengu. Endelea… Dk. Lwoga: Zinj ni kama tanzanite Zinj ana faida katika makundi matatu ya kiuchumi, kijamii na kimazingira. Zinj ...

Read More »

Mtazamo wa Jaji Mkuu usipuuzwe

Wiki iliyopita Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, alipendekeza kufanyika mabadiliko ya sheria ili kuruhusu watuhumiwa wa makosa yote, yakiwamo ya mauaji na uhujumu uchumi kupewa dhamana. Lengo la pendekezo hilo ni kupunguza msongamano kwenye magereza nchini. Jaji Mkuu alitoa ushauri huo alipotembelea Gereza la Butimba katika Jiji la Mwanza. Amesema Mahakama imekuwa na mapendekezo ...

Read More »

NINA NDOTO (27)

Weka malengo Ndoto inahitaji malengo. “Ndoto bila malengo ni ndoto tu, vinginevyo utaishia kupata mambo usiyoyategemea, hivyo kuwa na ndoto na kuwa na malengo,” anashauri Denzel Washington. “Malengo ni maono na ndoto vikiwa katika nguo za kazi,” anasema Dave Ramsey. Malengo ndiyo humfanya mtu aweke jitihada ya kutimiza ndoto zake, hivyo kuwa na malengo katika maisha ni jambo la msingi ...

Read More »

Fursa ya kipekee kiuchumi kwako na familia (2)

Mifano ya ujasiriamali yenye uthubutu lakini ikakwamishwa   Mwaka 2004 hadi Mei 2006 nilikuwa nimetumia uwezo wangu wa masoko kusajili dawa ya kiasili ya Dental Formula Power (DFP), ambayo inasaidia kutibu na kukinga meno yasipate magonjwa na kuzuia wazee wabaki na meno yao kinywani yakiwa imara hadi wanaingia kaburini. Basi nikatumia ushawishi kwenye mamlaka za nchi nyingine na Dental Formula ...

Read More »

TPA: Mizigo ya wateja iko salama bandarini

Bandari ya Dar es Salaam ni lango kuu la biashara kwa nchi yetu na nchi zote zinazotumia bandari hiyo. Kutokana na umuhimu wake, bandari inahitaji ulinzi madhubuti na wa kiwango cha hali ya juu.  Kutokana na umuhimu katika nyanja za kiuchumi na kibiashara, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeimarisha na inaendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa bandari ikiwemo ...

Read More »

Ndugu Rais waliotutangulia walisema ukimtuma mpumbavu…

Ndugu Rais, yawezekana katika maisha yetu tulishawatuma wapumbavu wengi tu. Kwa maisha yetu ya hapa duniani hao sasa ndio wanaozishikilia funguo za milango ya magereza yetu. Kama kuna pepo na moto baada ya sisi kupita, hao ndio wanaotusafishia njia yetu iendayo Jehanamu. Kuingia katika mji ule itakuwa ni vigumu, sawa na ngamia kupita katika tundu la sindano. Mpaka Mwenyezi Mungu ...

Read More »

Dawasa: Tunawaletea maji Dar na Pwani

Wakati wizara na taasisi za serikali zikiendelea kupambana kukamilisha matarajio ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020, katika kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa, Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) inatekeleza miradi mitano mikubwa ambayo imelenga kuwaondolea kero ya maji wakazi wa Jiji la Dar es Salaam pamoja ...

Read More »

Yapo madhara ya kuiga kila kitu

Binadamu anajiendeleza kwa kujifunza au kuiga kutoka kwa vizazi vilivyotangulia. Haipo jamii itakayojihakikishia maendeleo ya uhakika bila kujifunza kutoka jamii nyingine ilimradi wanajamii wanaafikiana juu ya maana ya maendeleo na yapi yawe ya kuiga ili kujiletea maendeleo. Teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) imeleta mabadiliko na maendeleo makubwa kwa binadamu duniani kote. Sababu moja ya maendeleo haya ni kuunganisha matumizi ...

Read More »

Namna ya kugawa mali za marehemu

Tanzania kuna sheria nne ambazo hutumika kugawa mirathi. Kwanza,  sheria za  kimila; pili,  sheria  za Kiislamu;  tatu, sheria ya urithi ya India ( Indian Succession Act) na nne, sheria ya mirathi ya watu wenye asili ya Asia. Swali la sheria gani kati ya hizo itumike katika kugawa mirathi hutegemea na mambo yafuatayo:  Kwanza, maisha aliyoishi marehemu. Marehemu kama aliishi maisha ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (38)

Malezi ya mama ni mtaji wa watu mashuhuri Umama ni mtihani. Kila nyuma ya mtu mashuhuri kuna mama makini. Mama ni mzaa chema, lakini kila nyuma ya mshika mkia kuna mama mzembe au hakuna mama. “Mungu asingeweza kuwa kila mahali, hivyo aliumba kina mama.” Ni methali ya Wayahudi ikisisitiza umuhimu wa mama. Kina mama ni watengenezaji wa historia, cha kusikitisha ...

Read More »

Asante sana Rais Magufuli

Kwenye safu hii, toleo Na. 391, niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari: “Rais Magufuli wasaidie wanyonge hawa”. Nilichoandika kilihusu mateso yanayowafika maelfu ya Watanzania katika magereza nchini mwetu. Nilianza na kisa cha kweli cha mama mmoja niliyemkuta akitoka kumwangalia mwanae katika mahabusu ya Gereza la Kisongo, Arusha. Mwanae, Gerald Silvanus Sambayuka (23) ni dereva wa bodaboda. Inadaiwa kuwa alikamatwa ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (7)

Wiki iliyopita katika sehemu ya 6 hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Sina kitu nitakachopoteza lile dubwasha likinishinda mama yangu. Sana sana nitapoteza roho yangu tu. Sasa roho yangu ikipotea kutakuwa na hasara gani? Je, ni nani ajuaye kwa dhati roho huenda wapi baada ya kifo? “Aliyeiweka roho ndani yangu atajua pa kuipeleka.” Kijana wangu huyu alikuwa anasema kila mara. ...

Read More »

Tutakwama, tusiendelee kujidanganya

Wakati Madagascar ikifanya maajabu katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika iliyomalizika hivi karibuni nchini Misri, wengine tulijidanganya kuwa tupo kundi gumu. Si kujidanganya tu, bali pia tulijipa matumaini kwamba lazima tupate uzoefu ili tuweze kufikia malengo halisi tunayoyataka. Tukaitolea mfano Uganda. Eti katika michuano ya mwaka huu walifika raundi ya pili, baada ya ‘kufanya vibaya’ katika michuano iliyopita, ambapo ...

Read More »

Ameuawa?

Naomi Marijani (36), mama wa mtoto mmoja, mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam ametoweka katika mazingira yenye utata kiasi cha kujengeka hisia kuwa ameuawa, JAMHURI linaripoti. Hadi leo zimetimia siku 63 tangu Naomi ametoweka katika mazingira yenye kuacha maswali mengi huku polisi wa Kigamboni wakionekana kutolipa kipaumbele suala la kupotea kwake, japo ushahidi wa mazingira unabainisha wazi mtuhumiwa wa ...

Read More »

Busara katika kodi ya ardhi

Hivi karibuni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula, ameonyesha ujasiri zaidi katika kuzibana taasisi na kampuni zenye madeni makubwa ya kodi ya pango la ardhi. Mpita Njia ama MN anatambua ukubwa wa tatizo hilo. Kwa mfano, Mwanza tu, kampuni na taasisi nane zinadaiwa zaidi ya Sh milioni 900. Na katika ziara yake, Naibu Waziri ...

Read More »

HALI YA UCHUMI KWA WATANZANIA

TEC, Bakwata, CCT wafichua mkwamo   Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) wamefichua mambo manane yanayoifanya nchi ishindwe kuwahakikishia wananchi uchumi imara na maendeleo endelevu. Mbali na kufichua aina hizo nane za udhaifu katika uchumi wa taifa, taasisi hizo zimebainisha fursa nane kuu, changamoto tano na aina nyingine nane ...

Read More »

Nchi yapiga hatua zaidi sekta ya afya

Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa kuwa na mashine bora 24 zinazopima makundi ya damu. Mitambo hiyo ya kisasa zaidi ulimwenguni inahusika pia kupima maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwamo homa ya ini na virusi vya ukimwi. Afrika Kusini ndilo taifa la kwanza Afrika kuwa na mashine hizo bora. Aidha, imethibitishwa kuwa, Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika kwa kuwa ...

Read More »

Diaspora wa kwanza duniani walitoka Ngorongoro

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabulla na Meneja Idara ya Urithi wa Utamadani katika Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) katika Bonde la Olduvai, Mhandisi Joshua Mwanduka; wanazungumzia ugunduzi wa Zinj miaka 60 iliyopita na faida zake kwa Tanzania na ulimwengu. Mhandisi Mwankunda Kuadhimisha miaka 60 tangu alipopatikana Zinj ni nafasi muhimu na adhimu katika ...

Read More »

Tumewasikia viongozi wa dini

Mwishoni mwa wiki iliyopita Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) walizindua kitabu chao kinachoelezea namna ya taifa kuendesha uchumi wa soko jamii. Maudhui ya kitabu hicho yamegusa mambo mengi. Kwa mfano, kuhusu mfumo wa uchumi wa soko jamii nchini, wameainisha dhamira ya mfumo huo wa soko jamii kwamba ni ...

Read More »

NINA NDOTO (26)

Nyuma ya pazia   Nyuma ya makala za nina ndoto kuna makala nyingi zilizowahi kuandikwa na hazijawahi kusomwa na mtu yeyote isipokuwa mimi mwandishi. Nyuma ya nyimbo wanazoimba wasanii wengi na tunazisikia zikichezwa redioni na nyingine tumepakua na kuweka katika simu zetu, kuna nyimbo nyingi ambazo ziliimbwa miaka ya nyuma na hatujawahi kuzisikia. Nyuma ya video nyingi za kuchekesha za ...

Read More »

Jinamizi wizi wa magari laibuka

Utata umegubika kuhusu umiliki wa gari la mfanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Moshi, Haika Mawala, lenye namba za usajili T 991 DMS aina ya Toyota Vangurd, baada ya taarifa mpya kuibuka zikidai gari hilo ni la wizi na liliingizwa nchini kwa njia za panya. Gari hilo ni miongoni mwa magari matatu yaliyokamatwa na polisi mkoani Kilimanjaro Septemba 14, ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (22)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii kwa kuuliza maswali haya: “Je, mfanyabiashara unaufahamu mwaka wa kodi wa taasisi au kampuni yako? Unafahamu makisio na taarifa ya mapato ya biashara au shughuli zako yanafanywaje? Usikose sehemu ya 22 kupitia Gazeti la JAMHURI kila Jumanne kupata majibu haya.” Sitanii, niwashukuru tena wasomaji wangu kwa mrejesho mkubwa mnaonipa. Nikiri tena sikufahamu kuwa sekta ya ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons