Monthly Archives: July 2019

Fursa ya kipekee kiuchumi kwako na familia

Naitwa Dk.  Joseph Kankola Buberwa au Dk. JK Buberwa. Ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 50. Ni  Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya JKBRS International Co Ltd yenye ofisi zake jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam. Hivi karibuni nimependekezwa kuwa Mwenyekiti wa Muunganikano wa Wana Maono (Visionaries) duniani, tukiwa ni waanzilishi wa chama hiki. Nimekuwa mtu mwenye maono makubwa kuhusu ...

Read More »

Chuo cha Bandari chemchemi ya wataalamu

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na kumiliki bandari nchini, pia inamiliki Chuo cha Bandari (Bandari College) kilichopo katika Wilaya ya Temeke. Chuo hiki ndicho chemchemi au hazina ya kutoa utaalamu au maarifa ya kuwa na uwezo au umahiri wa kuhudumia meli na mizigo, usimamizi wake na utoaji wa huduma zinazohusiana na shughuli za bandari. Historia ya chuo ...

Read More »

Ndugu Rais, Bashiru Ally ni wa fungu lipi?

Ndugu Rais, fikra za walio timamu hazijadili watu. Hujadili fikra pevu za watu walio timamu. Kwa walio wengi mpaka leo hawajaelewa ilikuwaje mpaka ndugu Bashiru Ally akateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Namfahamu tu kwa mawazo yake ya kufikirisha hasa tulipokuwa tukichangia pamoja hoja mbalimbali katika vyombo vya habari vya kimataifa kama DW, BBC, VOA, Radio France ...

Read More »

Tunaishi maisha halisi au vivuli vya maisha?

Inawezekana leo ninaelekea kujadili mada inayochanganya kidogo. Ili kuijadili vizuri mada hii nitamtumia mwanafalsafa Plato, aliyeona kwa mara ya kwanza ukweli juu ya vivuli na vitu halisi. Na ili kupambana na ulemavu wa fikra, ni muhimu kubungua bongo mara kwa mara. Plato ndiye mwanafalsafa aliyeanzisha Astria ya Pango. Astria hii ndiyo iliyoendelea hadi kuonyesha ukweli kwamba kuna vitu vinavyodumu na ...

Read More »

Jaguar amechemsha, lakini asipuuzwe

Mbunge wa Kenya, Charles Njagua Kanyi, maarufu pia kama mwanamuziki ‘Jaguar’, ametukumbusha ugumu wa kujenga utangamano wa Wana Afrika Mashariki. Jaguar ameamsha zogo hivi karibuni baada ya kutishia kuwavamia wafanyabiashara wa nchi kadhaa ikiwamo Tanzania na Uganda wanaofanya kazi Nairobi na ndani ya Jimbo lake la Starehe na kuwatimua warudi makwao. Tatizo ni kuonekana kwa wafanyabiashara hao kudhibiti baadhi ya ...

Read More »

Palipo na upendo kuna maisha

Palipo na upendo kuna maisha. Somo la kwanza katika maisha ni upendo. Somo la kwanza la kiroho ni upendo. Somo la kwanza la familia ni upendo. Somo la kwanza la uongozi ni upendo. Somo la kwanza la mafanikio ni upendo. Somo la kwanza la ujirani mwema ni upendo. Somo la kwanza la upendo ni upendo. Somo la kwanza la msamaha ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (37)

Wivu unaona tabasamu lako hauoni machozi yako   Wivu ni mtihani. Mwenye wivu haonekani mzuri anapokufanya uonekane mbaya. “Baadhi ya watu watakukataa, kwa sababu tu unameremeta sana kuwazidi. Hiyo ni sawa, endelea kumeremeta,” alisema Nandy Hale. Wivu unaona tabasamu lako, hauoni machozi yako. Wivu unaona kicheko chako, hauoni huzuni yako. Wivu unaona pesa yako, hauoni matumizi yako. Wivu unaona baraka ...

Read More »

Istilahi za kisiasa zitumike vema

Mapinduzi, mageuzi na mabadiliko ni baadhi ya istilahi za kisiasa ambazo kiongozi wa siasa anazitumia katika kushawishi na kuhamasisha wanasiasa wenzake na wananchi kufanya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika nchi yao. Bayana iliyoko ni kwamba istilahi zote hizi zina maana moja ya mabadiliko kisiasa. Ni aina gani ya mabadiliko ambayo kiongozi anataka yawepo kwa kupitia katika chama chake cha ...

Read More »

Yah: Nguvu ya hoja kuwa nguvu ya haja

Nianze na salamu japo si lazima sana kwa kizazi hiki chenye akili nyingi zisizokuwa na matokeo chanya kwa maendeleo ya taifa lao, najua nitalaumiwa sana kwa kauli yangu lakini ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili, nimeamua kusema ili nisemwe lakini ujumbe ufike. Taifa letu limekumbwa na wimbi kubwa la vijana wenye misimamo ya kisiasa bila kujua hatima ya ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (6)

Wiki iliyopita katika sehemu ya tano hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Lile limama lilinichukua likaniangalia kwa makini, likawa linasema: “Kanafanana nasi, umekapata wapi?” Lile litoto likasema: “Nimekaokota huko porini karibu na mpaka wa himaya yetu.” “Sasa unasemaje?” Lile limama likauliza tena litoto nalo likajibu: “Kaache tu mama kaende.” “Nenda ukakaweke kule kwenye mpaka wanakoishi watu wadogo kama yeye.” Haya niliyaelewa ...

Read More »

SKIIBII kafufuka baada ya kujiua kimuziki 

‘Hivi ndivyo mtu mashuhuri hufanya’. Ni jina la wimbo wa msanii wa Nigeria, Abbey Elias, maarufu kama Skiibii Mayana ama Swaggerlee, unaomtambulisha katika soko la muziki nchini humo na pande za dunia kwa sasa. Pamoja na umaarufu ambao umeanza kumvaa kijana huyu kwa sasa, mwaka 2015 hatasahaulika kwa mbinu yake ya kuusaka umaarufu kimuziki kwa kujitengenezea kifo na kutangazwa kwa ...

Read More »

Watanzania wapewa somo

Wadau mbalimbali nchini wametoa maoni yao mara baada ya wiki iliyopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumtangaza Ettiene Ndayiragije kuwa kocha mkuu wa muda wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars. Kocha huyo anachukua mikoba iliyoachwa na raia wa Nigeria, Emmanuel Amunike, ambaye mkataba wake wa kuifundisha timu hiyo ulisitishwa baada ya Stars kutofanya vizuri katika mashindano ...

Read More »

Waliomdanganya JPM kibao chageuka rasmi

Miezi miwili tangu aliyestahili tuzo ya mfanyakazi bora wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), James Kunena, kupokwa fursa hiyo saa chache kabla ya kutunukiwa na Rais Dk. John Magufuli katika kilele cha mwaka huu cha Mei Mosi, hali si shwari ndani ya Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU). Uchunguzi wa JAMHURI umebaini hali ya ‘hasira’ miongoni mwa wafanyakazi wa ...

Read More »

Dizeli yabainika ndani ya visima vya maji

Baadhi ya visima vya maji safi katika Kitongoji cha Buseresere wilayani Chato, mkoani Geita vimebainika kuwa na mchanganyiko wa maji na dizeli. Kutokana na hali hiyo, wananchi hao wanaelekeza lawama zao kwa mmiliki wa Kituo cha Mafuta cha Buseresere, Samwel Magazi. Kituo hicho cha mafuta kipo katika Mtaa wa Kabaherere, Kitongoji cha Buseresere, Kata ya Buseresere. Wananchi hao wamechukua hatua ...

Read More »

Vigogo KCBL watelekeza mali za mabilioni

Wafanyakazi wawili miongoni mwa watano waliofukuzwa kazi na Bodi ya Uongozi ya Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) wametoweka na kutelekeza mali za mabilioni ya fedha. Mali hizo ni pamoja na nyumba za kifahari, magari pamoja na viwanja. Ni mali ambazo kwa sasa zipo chini ya ulinzi wa vyombo vya dola kwa ajili ya uchunguzi. Wafanyakazi hao ni aliyekuwa Meneja Mkuu ...

Read More »

Je, wajua Wazungu, Wahindi, Wachina wote ni weusi?

Sehemu hii ya pili ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kugunduliwa kwa fuvu la binadamu wa kale la Zinjanthropus (Zinj) katika Bonde la Olduvai mkoani Arusha, wataalamu wawili wa mambokale – PROFESA CHARLES MUSIBA kutoka Chuo Kikuu cha Colorado, Marekani; na DK. AGNESS GIDNA wa Makumbusho ya Taifa, wanaeleza fahari hiyo ya Tanzania na Bara zima la Afrika. Profesa Musiba ...

Read More »

Penye nia pana njia

Wiki iliyopita serikali ilitoa taarifa kuhusu uamuzi wake wa kuanza  mchakato wa ununuzi wa vichwa 22 vya treni, mabehewa 1,430 ya mizigo na mabehewa 60 ya abiria, vitakavyotumika kwenye uendeshaji wa reli ya kisasa, maarufu kama SGR, ambayo ujenzi wake unaendelea chini ya Kampuni ya Yapi Merkez. Kampuni hiyo (Yapi Merkez) inajenga reli hiyo ya SGR awamu ya kwanza kutoka ...

Read More »

NINA NDOTO (25)

Fanya kazi kwa bidii   Nyuma ya ndoto nyingi zilizofanikiwa kuna kufanya kazi kwa bidii. Kama haupo tayari kufanya kazi kwa juhudi sahau kabisa ndoto zako kutimia. Ukimuuliza kila mtu aliyefanya makubwa katika dunia hii, sentesi “fanya kazi kwa bidii” huwa haikosi kinywani mwake. Uvivu siku zote huchochea umaskini. Mvivu hapendwi. Jambo jema na la kufurahisha kuhusu bidii ni kwamba ...

Read More »

‘Wenye ualbino wako salama nchini’

Tanzania imetajwa kufanya vizuri katika kukomesha mauaji dhidi ya watu wenye ualbino. Mwaka 2006 Tanzania iliingia kwenye historia mbaya baada ya watu hao kuanza kuuawa kwa imani za kishirikina. Takwimu zilizotolewa Septemba 21, 2014 na Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) zilibainisha kuwa mwaka 2006 hadi 2014, watu 74 walipoteza maisha kwa mikasa hiyo. Kwa mujibu wa takwimu hizo, ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (21)

Wiki iliyopita sikuzama sana katika mada hii ya kodi. Nawashukuru wasomaji wangu kwa kuendelea kuniletea mrejesho mkubwa katika eneo hili la kodi. Hakika sikufahamu kuwa kumbe watu wengi wana matatizo ya jinsi ya kuanzisha biashara kiasi hiki hadi nilipoanza kuandika makala hii. Nimeahidi kuwa makala hii nitaichapisha kama kitabu, lakini pia nikiri kuwa kuna baadhi ya maeneo nitapaswa kuyarekebisha maana ...

Read More »

Serikali, kampuni za simu kusaidia watoto, wanawake

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na kampuni za simu ili kuwasaidia wananchi katika huduma mbalimbali za kijamii zikiwamo za afya, elimu na miundombinu. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Vodacom Tanzania Foundation hivi karibuni, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kandege, amesema serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ili kuwawezesha Vodacom kuwafikia Watanzania wote wenye mahitaji.  Waziri Kandege amesema ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons