Monthly Archives: July 2019

Pongezi Tumaini Media, eneeni nchi nzima

Ni jambo la kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa hatua iliyofikiwa na Tumaini Media kuanzisha matangazo katika Jiji na Mkoa wa Dodoma. Kupitia Tumaini Media tunapata huduma nyingi za kiroho, kimwili na kijamii, ikiwa ni pamoja na uinjilishaji, kuelimisha umma kuhusu masuala mbalimbali ya kimwili ikiwemo maadili yetu ili tuishi vizuri kwa upendo, furaha na amani. Kwa uwezo na nguvu ya ...

Read More »

TPA inavyohudumia shehena ya mafuta, gesi

Katika mfululizo wa makala za bandari, wiki hii tunakuletea makala ya uhudumiaji wa shehena za mafuta na gesi katika bandari za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), hususan katika Bandari ya Dar es Salaam. Shehena za mafuata huagizwa na Petroleum Bulk Procurement Agency (PBPA), ambao ni wakala wa serikali. Wakala huu uliundwa kuepuka msongamano wa meli bandarini, hivyo kupunguza ...

Read More »

Ndugu Rais tukiwachekea waliokosa maarifa nchi itaangamia!

Ndugu Rais sitakusahau kwa ‘kiki’ (msemo wa vijana wakimaanisha kukwezwa) uliyonitunuku ukiwa waziri mwenye dhamana ya barabara. Huku kwetu Mbagala-Kokoto wa zamani wanajua kuwa ni mimi niliyesababisha ujenzi wa barabara mbili kutoka Mbagala-Terminal zilipoishia hadi hapa kwetu Mbagala-Kokoto. Ukiwa msomaji mahiri wa makala zangu, uliposoma tu nilipoandika kuwa gari la mkaa limeiangukia Hiace yenye abiria baada ya kuingia katika shimo ...

Read More »

Fikra inasaidia kuchochea maendeleo

Watanzania tuna kitu kinachotusumbua. Tunataka kujenga jamii iliyo bora. Tunataka kujenga jamii yenye mshikamano na uzalendo. Tunataka kujenga jamii yenye maadili mema na kuwarithisha watoto wetu maadili hayo. Tunataka kujenga jamii ambayo itarithisha vizazi vijavyo Tanzania yenye neema. Tutaijenga vipi jamii hii? Tuanze kutafakari na kufikiri. Tunahitaji wanafalsafa wa Kitanzania ambao watakaa chini na kukuna bongo zao kama walivyofanya wanafalsafa ...

Read More »

Historia ya ukombozi inatoweka polepole

Juma liliopita nimeongozana na ugeni kutoka baadhi ya nchi za Kusini mwa Afrika – Namibia, Zimbabwe, Msumbiji, na Zambia –sehemu ya wajumbe wa bodi ya Southern African Research and Documentation Centre (SARDC), kituo cha utafiti kilichopo Harare kinachofanya kazi kwa karibu sana na Sekretariati ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye ziara yao nchini. Mimi ni mjumbe ...

Read More »

Lissu kupoteza sifa urais, ubunge 2020

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amesema moja kati ya makosa mawili yaliyosababisha Tundu Lissu kufutwa ubunge ni kutojaza taarifa za mali na madeni. Kosa hili kwa mujibu wa Ibara ya 67(2)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kosa la kuvunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Ibara hiyo imeeleza kuwa mbunge yeyote anakosa sifa ...

Read More »

Uponyaji wa majeraha katika maisha (3)

Nakusihi wewe ambaye umeumizwa na mzazi wako, ‘msamehe’. Umeumizwa na mtoto wako wa kuzaa, ‘msamehe’. Umeumizwa na mume wako, ‘msamehe’. Umeumizwa na mke wako, ‘msamehe’. Umeumizwa na kaka yako, au dada yako, ‘msamehe’. Umeumizwa na jirani yako, ‘msamehe’. Umeumizwa na rafiki yako, ‘msamehe’. Umeumizwa na mwajiri wako, ‘msamehe’. Kusamehe ni bure. Yawezekana kwa wakati huu mambo yako hayaendi sawa. Una ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (36)

Neno ‘haliwezekani’ tafsiri yake hujafikiria sana   Suluhisho ni mtihani. Kila tatizo lina suluhisho, tatizo ni wapi upate hilo suluhisho. Kuna maoni tofauti juu ya suluhisho. Uri Levine anapendekeza: “Lipende tatizo, na si suluhisho.” Kuna ambao wanaona kuwa usijikite kwenye tatizo, jikite kwenye suluhisho. Mitazamo hii inafanya suluhisho kuwa mtihani. Kila tatizo limebeba suluhisho. Suluhisho ni njia ya kutatua tatizo. Katika ...

Read More »

Marekebisho vitambulisho vya wamachinga yanahitajika

Rais John Magufuli amejipambanua kama kiongozi mpenda wanyonge. Mara zote amesikika na hata ameonekana akiwatetea watu wa kada hiyo ambao kwa muda mrefu wametaabika. Hili ni jambo jema linalostahili kutendwa na kiongozi mkuu wa nchi. Katika kutekeleza dhana hiyo ya kuwa “Rais wa Wanyonge”, amehakikisha kodi nyingi zilizokuwa kero kwao zinaondoshwa. Akaona hiyo haitoshi. Akaandaa vitambulisho vya wachuuzi kwa kuwatoza ...

Read More »

Wananchi tunataka mabadiliko

Siasa ni sayansi, ni taaluma pia. Sayansi ina ukweli na uhakika, na taaluma ina maadili, kanuni na taratibu zake. Siasa ni mfumo, mtindo, utaratibu au mwelekeo wa jamii katika fani zake zote za maisha. Ni utaratibu uliowekwa au unaokusudiwa kuwekwa na chama kinachoongoza nchi, au kinachokusudia hivyo ili kukiwezesha chama hicho kunyakua au kudumisha uongozi wake. Mtu aliyomo katika taaluma ...

Read More »

Yah: Tumemaliza AFCON tujipange

Nianze kwa kuwapongeza vijana ambao kwa mara ya kwanza wametambua kwamba ni wawakilishi kwa maana ya mabalozi wetu waliokuwa wakipigania mafanikio ya taifa. Nawapongeza sana na tumeona ni jinsi gani ambavyo pamoja na jitihada zote kubwa walizokuwa nazo tumeshindwa kufanikiwa kuendelea kupeperusha bendera yetu kimataifa. Si jambo baya kwa sasa kwa kuwa bado tu wachanga katika vita ambayo wengine wameizoea ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (5)

Wiki iliyopita katika sehemu ya nne hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Akina mwewe pia walikuwepo wananyakua matambara kwa fujo kisha wanalia Zwi! Zululu! Ndege wengine wadogo walikuwa wanaruka juu juu na baadhi yao walikuwa wanaruka chini chini. Bata mzinga nao pia walikuwa wanahimiza wakisema mrudisheni mtoto wetu jamani, mrudisheni kwani amepotea na tunamtafuta.” Je, unafahamu nini kinafuata? Endelea… Bulongo, ndoto ...

Read More »

V.MONEY unakua kimuziki na kuikuza sanaa yako

Sikio halilali njaa, wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva baada ya kukanyaga na kutimua vumbi mitaani kwa nyimbo za vijana wa kundi la Wasafi (WCB) sasa ni muda wa Vanessa Mdee, maarufu kama Cash Madame na wimbo wake wa ‘Moyo’. Vanessa Mdee ambaye kwa mashabiki wake anafahamika zaidi kama V. Money, ameachia wimbo wa ‘Moyo’ wiki iliyopita ukiwa ni sehemu ...

Read More »

Lampard kuanza kipimo na vigogo

Wiki iliyopita mchezaji wa zamani wa timu ya Chelsea na West Ham United, Frank Lampard, alitangazwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Chelsea (The Blues). Timu hiyo inayopatikana katika Jiji la London, Uingereza, imeingia mkataba wa miaka mitatu na Lampard ambaye kabla ya mkataba wake huo wa kuinoa Chelsea alikuwa kocha wa Derby Country, klabu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza England. Lampard ...

Read More »

Bomu la ardhi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amepata jaribio kubwa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. “Siku moja baada ya kuingia ofisini, alijifungia ofisini kwake akasema ana shughuli nyingi hivyo asingeweza kumwona mtu yeyote. Ghafla, akaja mzee mmoja. Akamweleza msaidizi wake tukio la kusikitisha. Tukio lenyewe lilikuwa kama sinema vile. ...

Read More »

Bibi mjane Dar amlilia Makonda

Serikali ya Mtaa wa Nzasa Somelo, Kata ya Zingiziwa, Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam imetumia hila kumnyang’anya shamba la ekari tatu bibi mjane mwenye umri wa miaka zaidi ya 70. Shamba hilo ambalo limetenganishwa na Mto Nzasa, kipande kimoja kikiwa Wilaya ya Kisarawe na kingine Wilaya ya Ilala ni miliki ya Theresia Vingambudi ambaye anaishi Halmashauri ya Kisarawe, ...

Read More »

Olduvai: Bustani ya ‘Eden’

Julai 17, 1959 Mary Leakey aligundua fuvu katika eneo linaloitwa FLK-zinj katika Bonde la Olduvai, Ngorongoro mkoani Arusha. Lilikuwa fuvu la zamadamu wa jamii ngeni, hivyo yeye na mume wake Louis Leakey waliita Zinjanthropus boisei. Hapa ndipo mahali kunakotambulika duniani kote kuwa ndiko kwenye asili ya binadamu. Kutoka hapa binadamu walisambaa katika sayari yote ya dunia. Mamia kwa mamia ya ...

Read More »

Sheria ya Takwimu funzo

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekamilisha mkutano wake wa bajeti wiki iliyopita. Ukiondoa mjadala wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020, masuala mengine kadhaa yalijitokeza bungeni. Mojawapo ya mambo hayo ni serikali kuwasilisha mabadiliko ya sheria ya takwimu, marekebisho yaliyolenga vifungu vya sheria hiyo kuhusu haki ya kuchapisha au kutoa taarifa za takwimu kwa umma. Mabadiliko ...

Read More »

NINA NDOTO (24)

Watu ni mtaji   Siku, wiki, miezi, miaka vinapita mbele yangu mimi kwanini nisimshukuru Mungu kwa kunilinda vyema? Nasema asante Mungu kwa zawadi ya Maisha. Naandika makala hii nikiwa na furaha sana kwa kufikisha mwaka mwingine. Ni furaha iliyoje. Asante Mungu kwa mara nyingine. Wanasema kushukuru ni kuomba tena. Tangu zamani ndoto yangu ilikuwa ni kuandika vitabu na kuwahamasisha watu. ...

Read More »

Wadaiwa sugu KCBL waanza kusakwa

Benki ya Ushirika mkoani Kilimanjaro (KCBL) imeanza msako dhidi ya watu binafsi, vikundi vya wajasiriamali na kampuni zinazodaiwa mikopo na benki hiyo baada ya kushindwa kufanya marejesho ndani ya muda kulingana na masharti ya mikopo. Msako huo unafanywa na benki hiyo kupitia Kampuni ya Tanfin Consultant E.A Ltd ya jijini Dodoma ambayo imepewa ridhaa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (20)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii kwa kuwasisitiza wafanyabiashara na wamiliki wa kampuni kuhakikisha wanafunga hesabu zilizokaguliwa na kuziwasilisha TRA. Ni imani yangu kuwa wengi kama si nyote mlitekeleza na kama hukufanya hivyo, wasiliana haraka na ofisi ya TRA iliyopo karibu yako, kwani bila kufanya hivyo unahatarisha uhai wa kampuni yako kwa faini za kisheria. Sitanii, nichukue fursa hii kulishukuru Baraza ...

Read More »

Rostam: Wafanyabiashara tuzingatie sheria

Yafuatayo ni maelezo ya mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, wakati wa uzinduzi wa kampuni ya utoaji huduma za gesi, Taifa Gas, anayoimiliki. Katika kampuni hiyo, Rostam ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi. Uzinduzi huo ulifanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli wiki iliyopita, Kigamboni, jijini Dar es Salaam. “Mheshimiwa Rais, waheshimiwa mawaziri, mheshimiwa mkuu wa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons