Monthly Archives: July 2019

JAMHURI kinara tena

Gazeti la uchunguzi la JAMHURI limetwaa tuzo mbili za uandishi bora wa habari (Excellence in Journalism Awards Tanzania – EJAT) kwa mwaka 2018, tuzo zinazotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Hatua hiyo ni sehemu tu ya mafanikio ya gazeti hilo ambalo mwaka jana liliongoza dhidi ya vyombo vingine vyote vya habari Tanzania Bara na Zanzibar vilivyohusishwa kwenye utafiti wa ...

Read More »

Tunaihitaji sekta binafsi – Rais Dk. Magufuli

Kwa hiyo sekta binafsi endeleeni kujiamini, endeleeni kufanya kazi, mje Tanzania hapa ni mahali salama kwa uwekezaji. Tunawahitaji leo, tuliwahitaji juzi, tutawahitaji keshokutwa, tutawahitaji miaka yote kwa sababu Tanzania iko hapa kwa miaka yote. Tangu leo, kesho, keshokutwa na maisha yote.” Ifuatayo ni sehemu ya maneno kutoka katika hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ...

Read More »

Ndugu Rais, anayejidhania amesimama aangalie asianguke

Ndugu Rais, kama wapo wenzetu waliodhani kuzuia Bunge kuonekana kwa wananchi moja kwa moja kutawafanya wasijue yanayofanyika ndani ya Bunge, sasa wakiri kuwa hawakufikiri sawa sawa. Lisiporekebishwa hili kabla ya uchaguzi mkuu ujao itakuwa ni kwa hasara yetu wenyewe! Udhaifu wa Bunge katika sakata la CAG, timamu gani hakuuona? Baada ya kijana wetu mahiri Stephen Masele kujitetea Bunge lilioga fedheha ...

Read More »

TPA: Usalama ni namba moja katika shughuli za bandari

Bandari ni lango la biashara kitaifa na kimataifa, hivyo ni muhimu sana kufanya biashara katika bandari zenye usalama na mazingira rafiki na yanayovutia wateja. Kwa hiyo TPA ina wajibu wa kuhakikisha bandari zote nchini ni salama kwa wafanyakazi ili waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki na salama kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi. Pia TPA ina wajibu wa kuweka mazingira ...

Read More »

Tumechimba kaburi la utalii wa filamu

Hapa Tanzania ukitamka neno ‘utalii’, haraka haraka akili za watu hukimbilia kwenye mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro labda na fukwe za Zanzibar: Basi! Hata serikali inaelekea kufikiria hivyo, ndiyo maana mkazo kuhusu utalii uko kwenye aina hiyo tu ya utalii. Namna hii finyu ya kuuangalia utalii ndiyo inayosababisha tuwe na watalii wachache licha ya kuwa na vivutio vingi nadra na ...

Read More »

Mali iliyopatikana kabla ya ndoa inahesabika ya familia?

Mara kadhaa linapoibuka suala la kugawana mali pale ndoa inapohesabika kushindikana, masuala kadhaa ya msingi na yanayohitaji uelewa huwa yanaibuka. Moja ya suala kati ya masuala ambayo huibuka ni hili la kutenganisha na kufafanua hadhi ya mali za wanandoa ili mgawanyo uweze kufanyika kwa haki. Yawezekana mwanandoa akadhani ana haki katika mali fulani lakini kumbe kisheria hana haki hiyo, ni mtazamo wake ndio ...

Read More »

Uponyaji wa majeraha katika maisha (2)

Katika familia yangu tuliwahi kupata jeraha. Septemba 14, 1999 lilitokea tukio la kuhuzunisha kwenye familia yangu. Dada yangu kipenzi, Cecilia aliuawa kikatili, na aliyetenda tukio hilo ni mumewe. Dada aliuawa akiwa anamnyonyesha mtoto wake wa kike aliyekuwa na umri wa miezi mitano. Tukio hili tulilipokea kwa mwono wa dharau. Tuliamini kwamba, mume wa dada yetu amemuua dada yetu kwa kutudharau. ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (35)

Simba akizidiwa hula nyasi, huchambua asile miiba   Kutekeleza maono ni mtihani. Maono ni kuona ambacho hakionekani.  Kuna aliyesema: “Mtu bila maono ni mtu bila wakati ujao. Mtu bila wakati ujao atageukia wakati uliopita.” Atausifia wakati uliopita. Kuna wajenzi watatu waliokuwa wanajenga ukuta. Mpita njia alimuuliza wa kwanza, mnafanya nini? Alijibu: “Tunapanga matofali.” Alimuuliza wa pili, mnafanya nini? Alijibu: “Tunajenga ...

Read More »

Kuondoka Balton ni kosa kiuchumi

Mkutano wa Rais John Magufuli na wafanyabiashara ni miongoni mwa uamuzi wa busara uliosaidia kurejesha imani ya kundi hilo kwa serikali. Kulishatanda hofu kwamba wafanyabiashara ni kama vile watu wasiotakiwa, jambo ambalo si rahisi kutokea katika serikali yoyote makini. Nchi inahitaji fedha ili iweze kujiendesha. Kuna miradi mingi na mikubwa mno ambayo yote inahitaji fedha kuitekeleza. Fedha za kutekeleza kazi ...

Read More »

Tundu Lissu ‘moto’ wa nyika

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Vincent Mashinji hivi karibuni alikutana na waandishi wa habari kuzungumzia uamuzi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai kuiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu Jimbo la Mbunge Tundu Lissu kuwa wazi. Tumenukuu sehemu ya maelezo hayo hapa. Hadi tunapozungumza (na waandishi wa habari) ikiwa ni siku tatu tangu Spika ...

Read More »

Demokrasia ya vyama vingi si uhasama

Imetimu miaka 27 sasa tangu Watanzania waamue kurejesha mfumo wa demokrasia wa vyama vingi vya siasa nchini (1992 -2019). Katika harakati za kurejesha mfumo huu, kuna hotuba nyingi. Miongoni mwao viongozi waliotoa hotuba za namna hiyo ni Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, baada ya kukubali mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha ...

Read More »

Yah: Siasa isiwepo kila mahali

Kuna siku moja katika waraka wangu huu niliwahi kuonya juu ya mambo ya kitaalamu kuwaachia wataalamu wayafanye, wale ambao ni wanasiasa wajitahidi kutembea katika nafasi yao ya kupambana na masilahi na uwezeshaji wa kupanga vipaumbele kutokana na umuhimu. Kuna mambo mengi ambayo huwa nawaza inakuwaje siasa iingie katika masuala ambayo kimsingi siasa haiwezi kutoa matunda ya moja kwa moja bila ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (4)

Wiki iliyopita hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Tatizo jingine ni pale nilipotaka kutembea kidogo; ilipaswa kule nilikoelekea watu wataarifiwe kuwa nitapita eneo hilo kwa hiyo wachukue tahadhari nisije nikawakanyaga kwa bahati mbaya nikiwa katika mishemishe zangu. Hii ilikuwa kero sana kwa wenyeji wangu.” Je, unafahamu nini kinafuata. Endelea… Hata hivyo watu hawa walikuwa weledi sana na walikuwa na teknolojia ya ...

Read More »

‘Matusi’ hayakwepeki Bongo Fleva?

Kumekuwa na malalamiko yanayozidi kushika kasi kutoka kwa wadau wa soko la muziki wa Bongo Fleva siku za hivi karibuni, kwamba nyimbo nyingi zinazotungwa na kuimbwa na wasanii wa muziki huo zimekuwa na kasoro za kimaadili, hazina viwango vya kutosha vya ubunifu na kubwa zaidi, zimesheheni lugha ya ‘matusi’. Hiyo ni mitazamo ya wadau hao ingawa kwa upande mwingine huenda ...

Read More »

AFCON acha tu

Wakati michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ikiendelea nchini Misri hii leo ili kukamilisha hatua ya makundi, makundi mawili yataingia uwanjani kupepetana ili kuungana na timu nyingine waweze kufuzu hatua inayofuata ya mashindano hayo. Makundi hayo yaliyosalia ni kundi E na kundi F. Kundi E lina timu za Mali, Angola, Tunisia na Mauritania. Mali yenye pointi nne ambao ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons