JWTZ waombwa DRC

Wananchi wa Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameandamana wakitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lipelekwe nchini humo liwakung’ute waasi wanaoua mamia kwa maelfu ya watu. Bado wananchi wengi wa DRC wanatambua na kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na majeshi ya Umoja wa mataifa ya kulinda amani yaliyoongozwa na JWTZ baada ya…

Read More

Wameitelekeza Clock Tower Dar?

Mpita Njia, maarufu kama MN, ameendelea kufurahishwa na pilikapilika za mapokezi ya wageni wa nchi mbalimbali wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). MN ameshuhudia pilikapilika za usafi katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kipande cha Barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Clock Tower ama Mnara…

Read More

CHAKAMWATA yapigwa ‘stop’

Shughuli za Chama cha Kutetea Haki na Masilahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA) zimebatilishwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Ajira baada ya  kubaini chama hicho kukosa bodi ya wadhamini. Ofisi ya Msajili imefikia uamuzi huo wakati chama hicho cha walimu kikiwa katika maandalizi ya mkutano mkuu wa dharura wa taifa uliolenga kuwachagua…

Read More

Ngorongoro wapinduana

Uongozi wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro mkoani Arusha umepinduliwa. Waliochukua hatua hiyo wanawatuhumu viongozi hao kwa ufisadi na matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za baraza hilo. Uongozi wote wa juu umeondolewa. Walioondolewa ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji, Edward Maura; Makamu Mwenyekiti wa Baraza, Shutuk Kitamwas na Katibu wa Baraza la Wafugaji, Johanes Tiamasi….

Read More

Ripoti yafichua madudu uuzwaji shamba la KNCU

Uuzwaji wa shamba kubwa la kahawa la Gararagua lililopo Wilaya ya Siha mali ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro (KNCU) umedaiwa kugubikwa na madudu mengi, ikiwamo kuuzwa chini ya thamani halisi ya bei ya soko, pamoja na kutokujulikana zilipo ekari 2,000. Shamba hilo liliuzwa mwaka 2017 na KNCU kwa dola za Marekanai milioni 4.2…

Read More

Mtikisiko ajali ya lori Moro

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameunda timu maalumu kuchunguza tukio la mlipuko wa lori la mafuta ulioua watu 71  na majeruhi 59 kwa mujibu wa takwimu za hadi Jumapili alasiri. Timu hiyo inatarajiwa kukamilisha kazi zake Ijumaa wiki hii na kwa mujibu wa maelezo ya waziri mkuu, ibainishe yeyote ambaye amezembea katika kutimiza wajibu wake kwa…

Read More