Kombe la dunia linaanza siku tisa zijazo kuanzia leo. Afrika inawakilishwa 5 katika mashindano hayo yanayochezwa nchini Urusi na wachambuzi wanasema Afrika inayo nafasi zamu hii.

Leo tunakuletea makundi ya timu hizi na wiki ijayo tutakuletea ratiba yote ya michuano ya kombe la dunia 2018 kwa ajili ya kumbukumbu yako.

Kundi A

Kundi hili lina mwenyeji wa mashindano nchi ya Urusi na Saudi Arabia, Misri na Uruguay. Ndani ya kundi hili Urusi ndio nchi pekee iliyo chini kisoka katika viwango vya FIFA ikishika nafasi ya 65 wakifuata Saudi Arabia, nafasi ya 63, Misri na Uruguay wakiongoza kundi hili wakishika nafasi ya 21 katika ubora duniani.

Tathimini inaonyesha kuwa Urusi ina kazi ya ziada kupenya kundi hili kama nchi mwenyeji kitakwimu ingawa ubora wa FIFA si kigezo cha msingi katika maandalizi kimbinu na kiufundi kwa maana ya maandalizi.

Mechi ya ufunguzi Urusi itakutana na Saudi Arabia na ndiyo mechi pekee ambayo wenyeji wana asilimia 50/50 kushinda ukiangalia ubora wa vikosi vya Uruguay ikiwa na akina Edinson Cavan na Luis Suarez, huku Mohamedi Salah akizidi kuonesha ubora wake na Liverpool.

Kundi B

Kundi hili ndilo alipo mfalme wa soka kwa sasa duniani Christiano Ronaldo na kikosi cha Ureno kitakachofungua mechi za makundi na Hispania. Hii inasadikiwa kuwa fainali ya mwisho kwa Ronaldo kutokana na umri wake.

Hispania hawakuwa bora michuano ya mwaka 2014 nchini Brazil hali iliyowafanya kushindwa kuvuka hatua ya makundi hivyo inaleta changamoto kwa Ureno, Morocco na Iran. Morocco anahitajika kuwa makini zaidi ikiwa mara yake ya kwanza tangu fainali za mwaka 1998.

Kundi D

Kundi hili nalo lina mkali wa soka duniani  Lionel Messi na kikosi cha Argentina wakiwa na nchi za Croatia, Iceland na Nigeria, kwa mtazamo wa karibu unaweza kusema Argentina wakiongozwa na Messi wanaweza kupita kwa urahisi, lakini mambo hayatabiriki.

Iceland katika fainali za Euro mwaka 2016 walimng’oa England licha ya udogo wao na hakuna asiyekumbuka maajabu ya Croatia 1998 nchini Ufaransa. Hili ni kundi gumu lisilo tabirika.

Kama hiyo haitoshi Nigeria hivi karibuni alicheza mechi ya kirafiki na Argentina na ikaifunga Agentina nyumbani kwao 4-2 hivyo licha ya kupewa nafasi finyu kupenya, lakini anaweza kusonga mbele katika kundi hili pia.

Kundi G

Hapa kuna nchi za Ubelgiji, England, Panama na Tunisia, licha ya Ubelgiji kuwa bora kitakwimu, lakini England wanapewa nafasi kubwa kusonga mbele, kutokana na maandalizi yao  wakitengeneza kizazi kipya cha soka cha akina Harry Kane.

Meneja wa England wa hivi sasa Gareth Southgate fainali za mwaka 1998 alikuwa mlinzi wa kati wa England wakiwaadhibu Tunisia hivyo atajipanga vyema kulinda ‘legacy’ yake na taifa hilo kwa ujumla.

Kundi H

Hapa kuna Senegal,  walioweza kufika hatua ya robo fainali mwaka 2002, Colombia, Japan na Poland iliyochini ya  Robert Lewandowski, ni kundi ambalo kila timu ina uwezo wa kuvuka hatua ya makundi endapo itakuwa na maandalizi mazuri.

By Jamhuri