Author Archives: Jamhuri

Mnyukano wa Spika, CAG wapamba moto

Mvutano kati ya Bunge na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, umepamba moto. Kauli iliyotolewa wiki iliyopita na bingwa huyo wa masuala ya ukaguzi wakati akiwasilisha muhtasari wa ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka 2017/2018, imemwibua tena Spika Job Ndugai. Akionekana kukasirika, Spika Ndugai amesema endapo Profesa Assad anaendelea kurudia rudia kauli ya ‘udhaifu’, ...

Read More »

Jiji waomba fursa mabasi 100 ‘mwendokasi’

Uongozi wa Jiji la Dar es Salaam umeiomba Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwapa kibali cha kuongeza mabasi ya usafiri wa haraka (mwendokasi) katika Jiji la Dar es Salaam. Lengo la kuomba kibali hicho ni kutaka kushirikiana na mkandarasi aliyepewa dhamana ya kuendesha mradi huo ili kuboresha huduma ya usafiri ya ...

Read More »

Nondo feki zazua balaa Siha

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) imeanza uchunguzi kuhusu tuhuma zinazoikabili kampuni moja ya uuzaji wa vifaa vya ujenzi mkoani Kilimanjaro, inayodaiwa kuiuzia serikali nondo feki zisizo na ubora. Kampuni hiyo ambayo kwa sasa jina lake tunalihifadhi baada ya mkurugenzi wake kutopatikana, ilishinda zabuni ya kuuza nondo kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Siha ...

Read More »

Tukio la Papa Francis Vatican latikisa dunia

Baba Mtakatifu, Papa Francis, katika hali isiyotarajiwa amebusu miguu ya Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, akimsihi pamoja na wenzake kuhakikisha nchi hiyo hairudi kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe. Papa Francis amemwomba Rais Kiir na makamu wake wa awali, Riek Machar, ambaye ameasi kwa sasa, pamoja na makamu wengine wa rais waliofika Vatican kuheshimu makubaliano waliyotia saini ya kusitisha ...

Read More »

Kauli ya Dk. Bashiru ni mwanga kwa nchi yetu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amezungumza maneno mazito ambayo kwa yeyote anayeitakia heri nchi yetu yamemgusa. Maneno aliyoyasema yanaweza yasiwafurahishe wengi, hasa ndani ya chama chake, lakini huo ndio ukweli wenyewe. Ameonya juu ya mmomonyoko wa haki miongoni mwa wananchi na vyombo vya utoaji haki, na kuonya kuwa mataifa kama Sudan ambayo utawala wake umeangushwa ...

Read More »

NINA NDOTO (15)

Mambo ni mengi muda mchache   “Muda ni kitu tunachokihitaji sana, lakini ndicho kitu tuna  chokitumia vibaya,” anasema William Penn. Siku hizi ukipita mitaani utasikia watu wakisema, “Mambo ni mengi, muda mchache.” Ukweli ni kwamba mambo si mengi wala muda si mchache. “Tatizo la muda linaanzia kwenye matumizi yetu ya muda. Linaanzia kwenye vipaumbele vyetu na jinsi tunavyoutumia. Kila dakika ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (10)

Wiki iliyopita nilieleza kuwa leo nitaeleza wakati wa kuwasilisha maombi ya leseni chini ya kifungu cha 14 unapaswa kuipitisha hatua zipi. Katika sehemu hii ya 10, naomba kufafanua hili. Fomu yako ya kuomba leseni ni lazima ianzie ngazi ya chini kabisa. Sitanii, ngazi hizi ndizo za kufanya uamuzi wa awali wenye madhara makubwa mbele ya safari. Unaanzia ngazi ya kijiji ...

Read More »

Katika kushindwa kuna mbegu za ushindi

Ushindi ni mtihani. Si kila anayepata ‘A’ darasani atapata ‘A’ katika maisha. Si kila anayepata daraja la kwanza kwenye mitihani atapata daraja la kwanza kwenye maisha. Ushindi ni mtihani. Katika kila kushindwa kuna mbegu za ushindi, na katika kila ushindi kuna mbegu za kushindwa. Kauli hii iliwahi kutolewa na mwanadiplomasia na makamu wa 42 wa Rais wa Marekani, Walter Mondale. ...

Read More »

Ndugu Rais wanashangilia tu lakini mioyo yao haiko ‘clear’

Ndugu Rais, serikali ni sawa na mwanadamu. Haiwezekani kila kinachofanywa na serikali kikawa ni kibaya. Yako mazuri yanayofanywa na serikali. Na kuna maovu yanayofanywa na serikali. Hii ni kwa serikali zote – siyo hapa kwetu tu. Timamu hasifii kila jambo linalofanywa na serikali, na wala timamu hakosoi kila jambo linalofanywa na serikali. Timamu hushauri katika kweli na kwa nia njema ...

Read More »

DAWASA: Tunazidi kuwafikia wateja wetu

DAWASA imejizatiti katika kuhakikisha inawapatia maji salama wakazi wote wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na wale wa maeneo ya Mkoa wa Pwani. Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja, amekagua miradi ya maji inayoendelea kukamilishwa. Akizungumza na Gazeti la JAMHURI kabla ya kuanza ziara hiyo, Mhandisi Luhemeja anasema ziara ...

Read More »

Serengeti Boys, tunawategemea

Haikuwa kazi rahisi kwa Serengeti Boys kutawala mchezo kwa kiwango cha asilimia 58 dhidi ya asilimia 42 ya wapinzani wao, Nigeria, katika mechi ya ufunguzi wa Michuano ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Ingawa Serengeti Boys ilinyukwa mabao matano kwa manne katika mchezo huo wa Jumapili iliyopita, Kocha wa timu hiyo ...

Read More »

Tambo zaanza kuelekea Afcon

Kocha wa timu ya soka ya taifa ya Uganda, Sebastien Desabre, amesema timu ya taifa ya soka ya Zimbabwe ina nafasi finyu katika kundi ‘A’ kwenye michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baadaye mwezi Juni, mwaka huu. Uganda itakabiliana na mwenyeji wa michuano hiyo, Misri, DR Congo na Zimbabwe katika kundi ‘A’. Kocha huyo kwa upande ...

Read More »

‘Tunateseka’

Mahabusu wawili wamemwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, wakidai wanashtakiwa kwa kosa la kuua ilhali aliyefanya mauaji hayo na kukiri yuko huru uraiani. Michael Laizer na Lucas Mmasi, wanashikiliwa katika Gereza Kuu Mkoa wa Arusha, Kisongo, tangu mwaka 2015 wakikabiliwa na shtaka hilo wanalodai kuwa ni la kubambikiwa. Barua hiyo ambayo JAMHURI imeona nakala yake, ...

Read More »

‘Mjadala wa CAG, Bunge si utekelezaji wa ilani’

Mpita Njia, maarufu kwa ufupisho wa MN, kwa wiki nzima iliyopita amesikia mijadala mingi katika mitaa kadhaa aliyopita wakati wa shughuli zake za kawaida za kila siku. Mijadala hii ilihusu Azimio la Bunge tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad. Bunge limeazimia kutokufanya kazi na msomi ...

Read More »

Sekondari ya Filbert Bayi kushtakiwa mahakamani

Baba mzazi wa mwanafunzi aliyeruhusiwa na Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi iliyoko Kibaha, Pwani kufanya mtihani wa taifa kwa mwaka jana akiwa mjamzito amedhamiria kuishtaki shule hiyo kwa kuharibu ndoto za mwanaye. Egbert Bayi, baba mzazi wa mwanafunzi (jina linahifadhiwa) anataka kuishtaki shule hiyo ili imlipe gharama zote alizozitumia kumsomesha mwanafunzi huyo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne ...

Read More »

Rais Magufuli azima umegaji hifadhi

Rais John Magufuli amekataa mapendekezo ya wanavijiji katika Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, ya kutaka wamegewe ardhi katika Pori la Akiba la Selous. Amewaonya wanasiasa ambao hutumia ghiliba wakati wa kampeni kwa kuahidi kuwa wakichaguliwa watahakikisha wanamega maeneo ya hifadhi na kuwapa wananchi. Rais Magufuli yumo katika ziara ya siku tano mkoani Ruvuma. Amesema Tanzania ina ardhi kubwa ambayo ikitumiwa ...

Read More »

BoT wamtosa mteja aliyeibiwa Ecobank

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema haiwezi kufanya chochote kumsaidia mfanyabiashara aliyeibiwa fedha kwenye akaunti yake katika Ecobank, Tawi la Uhuru, jijini Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania (Divisheni ya Biashara) imeitia hatiani Ecobank Tanzania Limited kwa kumwibia mteja wake, Kampuni ya Future Trading Limited, Sh milioni 66 kutoka kwenye akaunti yake. Fedha hizo zimeibwa kwenye akaunti hiyo kupitia ...

Read More »

Tuhuma za ufisadi zatanda Kwimba

Kumeibuliwa tuhuma za ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza. Miradi mitano ya ujenzi imekwama. Miradi iliyokwama ni ujenzi wa vyumba vya maabara wa mwaka 2014; kliniki ya mifugo na bwalo la chakula, iliyoanza mwaka 2016. Mingine ni ujenzi wa nyumba tatu za walimu katika shule za msingi za Itegamatu, Ilula na ...

Read More »

Wanaolalamikiwa warejee hotuba ya Rais bungeni

Novemba 25, mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, alifungua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kulihutubia. Katika hotuba yake hiyo, Rais Magufuli alibainisha mambo kadhaa aliyokuwa ameyabaini wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 moja kwa moja kutoka kwa wananchi. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na suala la rushwa. Akasema ...

Read More »

NINA NDOTO (14)

Muda ni mali, utumie vizuri   Watu wanaoishi ndoto zao ni wazuri sana katika suala linalohusu matumizi ya muda. Muda ni mali, utumie vizuri. Wakati mwingine utasikia watu wakisema muda ni pesa, lakini kwangu mimi jambo hilo ni la tofauti kidogo. Muda ni zaidi ya pesa, unaweza kupoteza pesa ikarudi, muda ukipita umepita. Hauwezi kuirudisha jana au mwaka uliopita. Kinachowafanya ...

Read More »

Jaji azuia waandishi kuripoti kesi ya mauaji

Jaji Firmin Matogolo anayesikiliza shauri la mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Scolastica ya Himo, Humphrey Makundi, ameingia kwenye mvutano na waandishi wa habari wanaoripoti kesi hiyo baada ya kuwapiga marufuku kutonukuu chochote juu ya mwenendo wa shauri hilo. Badala yake, jaji huyo kutoka Mahakama Kuu Divesheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi akawataka waandishi hao kuingia ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (9)

Mpendwa msomaji, leo ni siku nyingine tunapokutana hapa. Nikiri wiki iliyopita nilihitimisha makala hii na maneno haya: “Mwisho, nawaomba wasomaji wangu, mniruhusu nisiwe ninawajibu maswali yenu kwa sasa kwani ni mengi. Nikiingia katika kujibu maswali hayo kama nilivyofanya leo, hakika sitaweza kukamilisha mada hii inayopaswa kuwa na makala zisizopungua 12 zikiwa msingi wa jinsi ya kufanya biashara Tanzania. Tukutane wiki ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons