Author Archives: Jamhuri

Bwawa laua mamia Brazil

Watu 300 wanahofiwa kufariki dunia baada ya bwawa la maji kuvunja kingo zake katika mgodi wa kampuni ya chuma kusini mashariki mwa Brazil. Maji yaliyochanganyika na matope yaliwafunika mamia ya wafanyakazi wa shirika hilo. Shughuli ya kuwatafuta walionusurika inaendelea karibu na mji wa Brumadinho, katika Jimbo la Minas Gerais. Gavana wa jimbo hilo, Romeu Zema, amesema kuna hofu huenda watu ...

Read More »

Mzozo wa kisiasa Venezuela wasambaa kimataifa

Baada ya maandamano ya kumshinikiza Rais Nicolas Maduro kung’atuka madarakani kukumbwa na vurugu, kiongozi mashuhuri wa upinzani, Juan Guaido, amejitangaza kuwa rais wa mpito. Guaido amepata uungwaji mkono kutoka mataifa ya Marekani, Canada na majirani wa taifa hilo walio na ushawishi mkubwa katika Kanda ya Amerika Kusini kama vile Brazil, Colombia na Argentina. Muungano wa Ulaya umetoa wito wa kufanywa ...

Read More »

Rais Magufuli, Dk. Mpango jengeni wafanyabiashara (4)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala yangu kwa kushauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanzisha Kitengo cha Kuanzisha na Kukuza Biashara. Nimepata mrejesho mkubwa. Nimekuta kumbe vijana wengi wanataka kuanzisha biashara lakini hawafahamu ni wapi pa kuanzia. Sitanii, nimepata fursa ya kusoma kitabu cha Mfanyabiashara Reginald Mengi cha ‘I Can, I Must, I Will’. Ni vema nichukue fursa hii kumpongeza mzee Mengi ...

Read More »

Baadhi ya vipimo muhimu ambavyo wengi huvisahau

Vipimo ni muhimu sana kwa maendeleo ya afya zetu, kwa watu wa jinsia zote na rika zote. Kupitia vipimo tunaweza kutambua mustakabali wa afya zetu, hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri katika kupambana na maradhi mbalimbali. Hivi karibuni takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zilionyesha kuwa idadi ya wanaume watu wazima wanaopatiwa vipimo vya afya ni ndogo kuliko idadi ya ...

Read More »

Mikumi kuongeza shughuli za kitalii

Kutokana na sekta ya utalii kutiliwa mkazo na Serikali ya Awamu ya Tano kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi, Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo Kilosa, mkoani Morogoro imejipanga kuongeza shughuli za kitalii kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi. Hifadhi hiyo ina ukubwa wa kilometa za mraba 3,230, inasifika kwa kuwa na wanyama wa kila aina wakiwemo tembo, ...

Read More »

Tunafanya dhambi kuua hifadhi

Tanzania imetenga maeneo kwa ajili ya kuhifadhi maliasili na urithi wa taifa kwa kuwa na maeneo yaliyohifadhiwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Wizara ya Maliasili na Utalii ndiyo iliyopewa mamlaka ya kusimamia maeneo yote yaliyohifadhiwa nchini yakiwa na sifa na hadhi tofauti tofauti. Kuna mapori ya akiba, misitu ya hifadhi, mapori tengefu, ...

Read More »

Ndugu Rais busara ni kupatana, tuwezeshee maridhiano

Ndugu Rais, kama Mwenyezi Mungu alinijalia sauti inayosikika na wengi walio karibu na walio mbali ili niwasemee waja wake, basi namwomba Muumba wetu huyo huyo awajalie baraka viongozi wetu ili wasizifanye ngumu shingo zao, bali wabarikiwe na wautegee sikio ukulele huu niupigao kama mtu aliaye kutoka jangwani:  Watoweni katika hofu watu wa Mungu ili wapate kuishi kwa amani, furaha na ...

Read More »

Barua ya wazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro

Ndugu Mhariri, Naleta hoja hii ambayo inatuhusu sisi wananchi wa Wilaya ya Kilosa kupitia Umoja wa Wakulima wa Umwagiliaji Mvumi (UWAUMVU) kuhusu uharibifu wa Skimu ya Mvumi. Skimu ya Mvumi iko katika Kijiji cha Mvumi, Kata ya Magole, Wilaya ya Kilosa, ilianzishwa mwaka 2002 na ina wanachama 298 huku eneo hilo likiwa na ukubwa wa ekari 720 zilizomo ndani ya ...

Read More »

Upuuzi na manufaa kwenye mtandao

Sina hakika kama lipo suala linaloweza kumpotezea binadamu muda wake bila manufaa yoyote kama kupitia taarifa zinazotufikia kwa njia ya mtandao. Watumiaji wa mtandao duniani wanakadiriwa kufikia bilioni 3.2 na wengi wao, kila siku wanasambaza taarifa za kila aina mtandaoni. Nyingi ya hizo hazina manufaa yoyote kwa mpokea taarifa. Wanaofaidika zaidi kiuchumi ni wamiliki wa kampuni zinazodhibiti na kuuza taarifa ...

Read More »

Trafiki akiomba leseni mwambie hivi…

Ukisimamishwa na trafiki barabarani na ukawa hauna leseni mfukoni kwa muda huo si kosa. Mwambie huyo trafiki kuwa hilo si kosa. Sheria inataka kutembea na leseni tunapoendesha vyombo vya moto, lakini pia haisemi kuwa utakapokuwa hauna pale unapoombwa na trafiki ni kosa. Tunazungumzia Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168. Wapo watu wameandikiwa faini kisa wameombwa leseni wakasema hawana, au wakasema ...

Read More »

Historia ya Sikukuu ya Valentine’s Day

“Upendo huvumilia, Upendo hufadhili, Upendo hauhusudu, Upendo haujivuni, Upendo haukosi kuwa na adabu, Upendo hauhesabu mabaya, Upendo haufurahii udhalimu, Upendo hautakabari, Upendo hustahimili yote.’’ – (1Kor 13:113). Februari 14, dunia nzima inasherehekea Sikukuu ya Wapendanao, ijulikanayo kama ‘Valentine’s Day’. Ningependa leo tufahamu sote asili ya sikukuu hii. Mwanzilishi wa sikukuu ni padri wa Kanisa Katoliki ambaye Kanisa Katoliki linamheshimu kama ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (14)

Kushindwa ni mtihani, mambo magumu sana ya kushughulikia maishani ni kushindwa na kushinda. Ukishindwa ni mtihani, ukishinda ni mtihani. Kuendeleza ushindi ni mtihani, kushikilia namba moja ni mtihani, kushikilia namba ya mwisho ni mtihani. Hoja si kushindwa bali lile mtu analofanya baada ya kushindwa. Hakuna anayefanikiwa bila kushindwa,  hakuna ambaye hufanikiwa kwa sababu ya kushindwa. “Tunaogopa kushindwa sana, kushindwa ni ...

Read More »

Rais nakuomba utafakari upya (2)

Ndugu Rais, sehemu ya kwanza ya waraka huu niliishia kwenye maneno ya hekima ya uhifadhi yaliyotolewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Agosti 10, 1975. Kwa ufupi Mwalimu alieleza matokeo ya dhambi ya kuteketeza wanyamapori na misitu iliyotendwa na Wazungu katika mataifa yao. Mwalimu alituasa tusitende dhambi hiyo. Ndugu Rais, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ...

Read More »

Tuthubutu kuondoa umaskini

Mara kadhaa nimepata kumsikia Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli, akisema nchi yetu ni tajiri wakati wananchi wake ni maskini. Nchi hii imetunukiwa maliasili nyingi na Mwenyezi Mungu lakini watu wachache wametuchezea mno katika kupora mali zetu. Kauli hii inapambwa na maelezo yasemayo: “Mali hizo zingetuwezesha kuwa matajiri kama tusingechezewa na watu fulani wakiwemo ndugu zetu. Watu hawa ndio waliotufikisha ...

Read More »

Yah: Liwepo ‘bunge’ la pili la viongozi wa dini

Sijui nianze na salamu gani katika waraka wangu huu, lakini cha msingi ni kujuliana hali kwa namna yoyote ile, kwa mujibu wa waraka wangu napenda kuwajulia hali kwa namna ya salamu zenu za itikadi ya dini na protokali izingatiwe. Wiki jana Mheshimiwa Rais alikutana na viongozi wa dini pale Ikulu, kwa namna alivyokuwa akiongea nao akili yangu iligeuka na nikaona ...

Read More »

Pumzika kwa amani Oliver Mtukudzi

Mwanamuziki nguli wa muziki wa Jazz kutoka Zimbabwe, Oliver Mtukudzi ‘Tuku’(pichani juu), amefariki dunia wiki iliyopita katika Hospitali ya Avenues jijini Harare akiwa na umri wa miaka 66. Tuku alilazwa hospitalini hapo baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kabla hajalazwa mwanamuziki huyo alikuwa katika ziara nchi mbalimbali duniani. Alilazimika kukatisha ziara yake kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua. Tuku amefariki dunia ikiwa ...

Read More »

Kichwa cha mwendawazimu?

Nini kifanyike kuhusu timu za hapa nchini? Pengine ndilo linaweza kuwa swali kwa wadau wa soka. Mashindano ya SportPesa yalimalizika juzi huku tukishuhudia klabu kutoka nchi jirani zikichuana kwenye fainali. Katika mashindano hayo ambayo Yanga ilitolewa mapema tu na Kariobangi Sharks ya Kenya, hali hiyo imedhihirisha kwamba klabu za Tanzania hazijajipanga vizuri. Mashindano hayo yalihusisha timu zinazodhaminiwa na SportPesa. Wadhamini ...

Read More »

Lissu njia panda

Ofisi ya Bunge inakusudia kutangaza hatima ya ubunge wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), baada ya kutokuwapo bungeni kwa miezi 16 sasa. Uamuzi huo ukisubiriwa kutoka kwa Spika Job Ndugai, mwanasiasa huyo amekataa kuzungumzia lolote kuhusu madai kwamba ofisi yake inataka kuchukua uamuzi wa kumtangaza Lissu kuwa si mbunge baada ya kukosa mikutano mitatu ya Bunge mfululizo, hivyo ...

Read More »

Benki M yaikuza Benki ya Azania

Ukosefu wa ukwasi wa kutosha uliokuwa unaikabili Benki M umesababisha mali na madeni yake kuhamishiwa katika Benki ya Azania Ltd, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema. Uamuzi huo umefikiwa baada ya BoT kubaini kuwa benki hiyo imetetereka na kujikuta ikiwa chini ya kiwango cha ukwasi unaohitajika kwa mujibu wa sheria za benki wa Sh bilioni 15, kiwango ambacho kinatakiwa kulinda ...

Read More »

Walioondolewa Takukuru wapangiwa vituo

Waliokuwa wafanyakazi wa Taasisi ya Kuzuaia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), walioenguliwa wameanza kupangiwa majukumu katika idara na taasisi nyingine za serikali. Waliopangiwa vituo tayari ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma, Ekwabi Mujungu, ambaye amehamishiwa Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, kama msaidizi anayehusika na masuala ya utawala na Mbengwa Kasomambuto, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi, yeye amehamishiwa ...

Read More »

Kwimba wavutana ziliko Sh bilioni 2

Shilingi bilioni 2.27 zinadaiwa kutumika kinyume cha taratibu na sheria ya fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza. Fedha hizo ni mapato ya vyanzo mbalimbali ambayo hayakuwapo kwenye mpango wa bajeti ya halmashauri hiyo wa mwaka wa fedha wa 2017/2018. Ripoti ya Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Kwimba ya robo ya kwanza ya Julai – Septemba 2018/2019 ...

Read More »

Kamwe tusijisahau, tuwe macho dhidi ya magaidi

Kwa mara nyingine genge la magaidi limeshambulia na kuua majirani zetu kadhaa wa jijini Nairobi, Kenya. Imeripotiwa watu 21 wamepoteza maisha kwenye shambulizi hilo. Tunawapa pole ndugu wa marehemu, majeruhi na wote walioathiriwa kwa namna moja au nyingine na tukio hilo. Kwa namna nyingine magaidi wamedhihirisha kuwa wapo na pia dunia si salama kama baadhi yetu wanavyodhani. Hizi ni salamu ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons