Author Archives: Jamhuri

Ona wachezaji TPL wanavyoburuzwa

Wakati Ligi Kuu imeanza rasmi, yapo mambo mengi ambayo yanatakiwa kutazamwa kwa undani na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Nalo ni suala linaloendelea kujirudia kila msimu, ambalo ni tatizo la wachezaji wengi kujikuta wakishindwa kutimiziwa yale yote ambayo wanaahidiwa kupitia mikataba wanayoingia na klabu. Uelewa wa wachezaji kuhusu haki zao za msingi wanazostahili kutimiziwa ndani ya kipindi wanachokuwa wakichezea timu ...

Read More »

Kashfa nzito

Serikali ya Rais John Pombe Magufuli imo hatarini kupoteza zaidi ya Sh bilioni 120 kutokana na mradi wa kukopesha matreka kwa wakulima ambao mkataba uliingiwa siku 8 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kugeuka ‘kichomi’, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Mkataba huo unaotajwa kuwa na mazonge mengi, uliingiwa Oktoba 22, 2015 ikiwa ni wiki moja na siku moja kabla ya ...

Read More »

Wanavyobebwa walioghushi Leseni ya Rais

Kudhani kwamba Lazaro Nyalandu hayumo ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii ni kujidanganya. Bado yumo. Mtandao wake upo, na unafanya kazi kweli kweli. Baadhi ya waliokuwa wasaidizi wake leo ndio wenye uamuzi wa nani anyang’anywe, au nani apewe kitalu. Kudhani kwamba ugawaji wa vitalu kwa mnada/mtandao kunasaidia mambo, ni kujidanganya. Mfumo ndiyo mbaya kuliko hata ule wa kamati. Hili ...

Read More »

Serikali kuamua mazito Lyamungo AMCOS

Serikali imesema itachukua uamuzi mgumu dhidi ya Chama cha Ushirika wa Mazao cha Lyamungo AMCOS kutokana na chama hicho kukaidi maagizo yake kuhusu kuondoa zuio mahakamani linalohusiana na shamba la kahawa la Lyamungo. Shamba hilo limekuwa kwenye mgogoro usiokwisha kwa miaka 14 sasa kutokana na msuguano uliopo kati ya Lyamungo AMCOS na Chama Kikuu cha Ushirika Kilimanjaro (KNCU), ambapo kila ...

Read More »

Yaliyowakuta wanahabari gerezani

Hatimaye waandishi wa habari, Christopher Gamaina na wenzake wawili wa jijini Mwanza wameachiwa huru kwa dhamana ya mahakama. Wanakabiliwa na tuhuma ya unyang’anyi wa kutumia nguvu wa Sh milioni tatu, katika kesi namba 11 ya mwaka 2018. Kila mmoja amedhaminiwa na watu wawili kwa kusaini hundi ya maneno ya shilingi milioni tatu, kila mmoja. Kesi hiyo inatokana na kinachodaiwa kuwa ...

Read More »

Dhamira ya Mugabe iheshimiwe

Moja ya matukio ya kukumbukwa katika urais wa Robert Mugabe wa Zimbabwe ni lile la Julai mwaka 2017. Katika tukio hilo, Zimbabwe iliyokuwa ikiongozwa na mzee Mugabe iliuza ng’ombe wa thamani ya dola za Marekani milioni moja kwenye mnada na kukabidhi fedha hizo kwa Wakfu wa Muungano wa Afrika kusaidia kumaliza utamaduni wa kutegemea fedha kutoka kwa wafadhili wa nje ...

Read More »

NINA NDOTO (31)

Hesabu baraka zako Ukiwa‌ ‌na‌ ‌ndoto‌ ‌si‌ ‌kila‌ ‌kitu‌ ‌unachokifanya‌ ‌kitaleta‌ ‌matokeo‌ ‌unayotarajia.‌ ‌Ni‌ ‌jambo‌ ‌jema‌ ‌kuwa‌ ‌na‌ ‌matarajio‌ ‌makubwa,‌ ‌lakini‌ ‌ni‌ ‌vema‌ ‌pia‌ ‌kuwa‌ ‌na‌ ‌moyo‌ ‌wa‌ ‌kustahimili.‌ ‌ Moyo‌ ‌wa‌ ‌ustahimilivu‌ ‌ndiyo‌ ‌huwafanya‌ ‌wenye‌ ‌ndoto‌ ‌waendelee‌ ‌kubaki‌‌ katika‌ ‌mstari‌ ingawa‌ ‌muda‌ ‌mwingine‌ ‌maisha‌ ‌yatawatoa‌ ‌nje‌ ‌ya‌ ‌mstari.‌ ‌ Kuwa‌ ‌mstahimilivu‌ ‌ni‌ ‌kuwa‌ ‌na‌ ‌tabasamu‌ ‌wakati‌ ‌ambao‌ ‌unatakiwa‌ ‌kununa,‌ ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (42)

Nani ataomboleza utakapoaga dunia?   Kifo ni mtihani. Kuna aliyesema dunia ni mahali pa hatari sana, hautoki ukiwa hai. Hadithi inapokuwa nzuri kwenye gazeti wanaikatisha na kuandika itaendelea toleo lijalo. Mtu anapoaga dunia ni Mungu anakatisha hadithi ya maisha yake, ni kama anaandika kuwa hadithi yake itaendelea toleo lijalo. Hasara kubwa si kifo, bali kinachokufa ndani mwetu. “Kifo si hasara ...

Read More »

SADC imepata ‘chuma’

Jumuiya ya kimataifa pamoja na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wanasubiri kuona mageuzi makubwa yatakayoletwa na Rais Dk. John Magufuli, ambaye ndiye mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo. Tayari katika hotuba yake ya kukubali majukumu yake hayo, ameainisha mambo ambayo atayapa kipaumbele katika kipindi chake cha mwaka mmoja wa uenyekiti wake wa SADC. Mambo hayo ni ...

Read More »

Maboresho bandari Ziwa Nyasa kunufaisha Ukanda wa SADC

Miradi mbalimbali inayofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika bandari za Ziwa Nyasa, inatazamiwa kuongeza ufanisi maradufu katika uhudumiaji na usafirishaji mizigo. Hatua hiyo inaelezwa kwamba itazinufaisha pia nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika zinazopakana au kuwa karibu na ziwa hilo la tatu kwa ukubwa Afrika. Katika mazungumzo rasmi na gazeti hili, Meneja wa ...

Read More »

Ndugu Rais tulipewa Julius Nyerere lakini hatukumjua aliyetupa

Ndugu Rais, imeandikwa kuwa Yesu Kristo kabla ya kuondoka, aliwaambia wanafunzi wake, “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu kamwe hayatapita!’’ Miaka zaidi ya 2000 imepita tangu kifo chake, lakini ulimwengu unashuhudia maneno yake yangali yamesimama vilevile nukta kwa mkato mpaka leo. Na hivyo ndivyo zitakavyodumu fikra sahihi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere! Awamu zitakuja, awamu zitapita, ...

Read More »

‘Rais, pensheni yangu Brigedia Jenerali ni 100,000 tu’

Sehemu iliyopita, mwandishi alieleza kuwa kwa mujibu wa sheria ya pensheni, wakongwe wanalipwa fedha kidogo mno. Akasema wakongwe wote wanarundikwa katika kapu au fungu moja la malipo ya uzeeni – na wote wanalipwa Sh100,000 (laki moja) tu kila mwezi bila kujali mstaafu alikuwa na cheo gani au mshahara upi – alimradi alistaafu kabla ya Juni 30, 1999 basi malipo yake ...

Read More »

Afrika inahitaji mabingwa wa kusaka umoja

Mwaka 1994 akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe iliyofanyika Arusha ya kuvunja Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), Mwalimu Julius Nyerere alitoa ujumbe ambao unafaa kurudiwa. Alisema waasisi wa OAU waliokutana jijini Cairo; Mei 1964 walijipangia kutekeleza majukumu mawili: kwanza, kukomboa bara lote la Afrika kutoka kwenye tawala za kikoloni na za kibaguzi, na pili kujenga ...

Read More »

Kuomba kutambuliwa kama mzazi wa mtoto

Wako watu ni wazazi na wamezaa lakini wameyimwa watoto. Zipo sababu nyingi katika jambo hili. Matukio ya namna hii hayawatokei sana wanawake bali wanaume. Ni rahisi na kawaida mno mwanamume kuambiwa na mzazi mwenzake  kuwa huyu  mtoto si wako hata  kama  anajua kabisa huyo mwanamume ndiye mzazi halisi. Upo usemi wao kuwa mwanamke ndiye anayejua baba wa mtoto. Sitaki kueleza ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (11)

Wiki iliyopita katika sehemu ya 10 hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Nilitembea kidogo kisha nikajikuta niko kwenye himaya ya watu wa ajabu. Sielewi sawa sawa kama hawa walikuwa ni watu au la. Nilipelekwa kwenye ghorofa moja na huko nikakuta nimeandaliwa chakula. Kilikuwa eti damu ya kichwa cha mtu. Sikula na waliponibembeleza ikashindikana hatimaye waliondoka. Nikaachwa peke yangu.” Endelea… Baadaye ...

Read More »

Mbalamwezi alivyoagwa kupitia mitandao ya kijamii

Baada ya kifo cha aliyekuwa msanii nyota wa Bongo Fleva, maarufu kwa jina la Mbalamwezi aliyekuwa anaunda kundi la The Mafik,  mastaa mbalimbali wa muziki wa  Bongo Fleva nchini wametumia mitandao yao ya kijamii kama Instagram  kumuaga nyota mwenzao huyo wa muziki aliyefariki dunia Ijumaa iliyopita na kuzikwa siku iliyofuata kwao Tandika, jiijini Dar es Salaam. Msanii wa muziki wa ...

Read More »

Wanapotea kwa faida ya Simba, Yanga

Msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara umefungiliwa rasmi. Sasa, fitina, mizengwe, ujuaji, uamuzi mbovu wa waamuzi, upanguaji wa ratiba na mengi ya kero ndiyo tutakayoanza kuyashuhudia. Msimu uliopita ulimalizika huku kukiwa na malalamiko kadhaa kutoka kwa wadau mbalimbali wa soka, ambao mwisho walitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), pamoja na Bodi ya Ligi Kuu kujitathmini. Zilionekana kasoro tatu ...

Read More »

JWTZ waombwa DRC

Wananchi wa Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameandamana wakitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lipelekwe nchini humo liwakung’ute waasi wanaoua mamia kwa maelfu ya watu. Bado wananchi wengi wa DRC wanatambua na kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na majeshi ya Umoja wa mataifa ya kulinda amani yaliyoongozwa na JWTZ baada ya kuwafurusha waasi wa March 23 ...

Read More »

Wameitelekeza Clock Tower Dar?

Mpita Njia, maarufu kama MN, ameendelea kufurahishwa na pilikapilika za mapokezi ya wageni wa nchi mbalimbali wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). MN ameshuhudia pilikapilika za usafi katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kipande cha Barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Clock Tower ama Mnara wa Saa uliopo eneo la ...

Read More »

CHAKAMWATA yapigwa ‘stop’

Shughuli za Chama cha Kutetea Haki na Masilahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA) zimebatilishwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Ajira baada ya  kubaini chama hicho kukosa bodi ya wadhamini. Ofisi ya Msajili imefikia uamuzi huo wakati chama hicho cha walimu kikiwa katika maandalizi ya mkutano mkuu wa dharura wa taifa uliolenga kuwachagua viongozi wake wapya. Mkutano huo ...

Read More »

Ngorongoro wapinduana

Uongozi wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro mkoani Arusha umepinduliwa. Waliochukua hatua hiyo wanawatuhumu viongozi hao kwa ufisadi na matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za baraza hilo. Uongozi wote wa juu umeondolewa. Walioondolewa ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji, Edward Maura; Makamu Mwenyekiti wa Baraza, Shutuk Kitamwas na Katibu wa Baraza la Wafugaji, Johanes Tiamasi. Taarifa ya waendesha mapinduzi hao ...

Read More »

Ripoti yafichua madudu uuzwaji shamba la KNCU

Uuzwaji wa shamba kubwa la kahawa la Gararagua lililopo Wilaya ya Siha mali ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro (KNCU) umedaiwa kugubikwa na madudu mengi, ikiwamo kuuzwa chini ya thamani halisi ya bei ya soko, pamoja na kutokujulikana zilipo ekari 2,000. Shamba hilo liliuzwa mwaka 2017 na KNCU kwa dola za Marekanai milioni 4.2 sawa na Sh bilioni 9.24, ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons