Author Archives: Jamhuri

Mtikisiko ajali ya lori Moro

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameunda timu maalumu kuchunguza tukio la mlipuko wa lori la mafuta ulioua watu 71  na majeruhi 59 kwa mujibu wa takwimu za hadi Jumapili alasiri. Timu hiyo inatarajiwa kukamilisha kazi zake Ijumaa wiki hii na kwa mujibu wa maelezo ya waziri mkuu, ibainishe yeyote ambaye amezembea katika kutimiza wajibu wake kwa wakati kuhusu ajali hiyo ya ...

Read More »

SADC ivunje minyororo iliyowekwa na wakoloni

Agosti ya mwaka huu 2019 ni ya kipekee kwa taifa letu. Tumepokea wageni wengi wanaohudhuria Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Fursa za aina hii hujitokeza mara chache, kwa hiyo kila Mtanzania ana haki na wajibu wa kuchangamkia fursa zinazotokana na ugeni huu. SADC ni matokeo ya historia ya ukombozi wa mataifa ...

Read More »

NINA NDOTO (30)

Ukiwa na ndoto usipige kelele, kaa kimya   Mtu anapokuwa na ndoto mara ya kwanza huwa haipo katika uhalisia, bado inakuwa haijatimilika. Kwa msingi huo, unapokuwa na ndoto, kaa kimya usipige kelele. Mojawapo ya kosa kubwa alilolifanya Yusufu ni kuwaambia ndugu zake ndoto yake kuwa baadaye atakuwa kiongozi wao. Huu ukawa mwanzo wa ndugu zake kuamsha chuki zao juu Yake. ...

Read More »

Mama mkwe wa Naomi alonga

Ni jioni ya saa 11 Jumatatu Agosti 5, 2019. Nipo ofisini. Mara napata simu, namba siifahamu. Mtu huyu ananiambia anataka kuiongezea nyama habari tunayochapisha kuhusiana na mauaji ya Naomi Marijani (36), anayedaiwa kuuawa na mumewe, Hamis (Meshack) Said Luwongo (38). Mtu huyu ananieleza taarifa zinazofanana na alizonipatia awali Mchungaji Said Luwongo (76), ambaye ni baba wa Hamis, tulipozungumza naye nyumbani ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (26)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii kwa kuhoji hivi: “Je, unaelewa VAT ni nini na inalipwaje? Usikose sehemu ya 26 ya makala hii wiki ijayo.” Leo nashindwa kuanza makala hii bila kutoa pole kwa taifa letu kutokana na msiba mkubwa uliotokea mkoani Morogoro, baada ya watu zaidi ya 70 kufariki dunia na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa kutokana na lori lililokuwa ...

Read More »

Wakulima Kilombero wanufaika na kilimo endelevu

Mfuko wa Wanyamapori Africa (AWF) umesaidia wakulima wa mpunga na kokoa Kilombero kupitia Mradi wa Ukuaji wa Kilimo Shirikishi na Endelevu Kilombero katika kutoa elimu ya mnyororo wa thamani ili kuwa na kilimo chenye tija. Katika mradi huo wa miaka mitatu ulioanza mwaka 2017, AWF pamoja na wadau wengine imewezesha wakulima zaidi ya 500 katika kupata mbegu bora za kokoa ...

Read More »

Niacheni niseme ukweli japo unagharimu

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, amefuta leseni ya umiliki wa kitalu cha Lake Natron East kinachoendeshwa na Kampuni ya Green Mile Safaris (GMS). Kwenye maelezo yake hakuwa na mengi, isipokuwa amenukuu kifungu kwenye Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009; pia kwenye mitandao ya kijamii amesema amefanya hivyo kwa kuzingatia ‘masilahi mapana ya nchi’. Mara zote ...

Read More »

BANDARI ZA TANZANIA

Lango kuu la biashara za SADC   BANDARI za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara na nyinginezo nchini Tanzania ni lango kuu la biashara kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC); za Malawi, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Msumbiji na Zimbabwe. Bandari hizi zilijengwa kabla ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, na zimekuwa zikifanyiwa maboresho katika ...

Read More »

Ndugu Rais amani ya nchi yetu imetikiswa

Ndugu Rais, mwishoni mwa miaka ya 1960, tungali vijana rijali na wasomi wazuri, wahitimu wa ‘middle school’ shule ya kati, Rais Julius Nyerere alifanya ziara mkoani kwetu – wakati huo ukiitwa Mbeya. Wakati ule ukisema Rais Nyerere ilikuwa inatosha. Utaratibu wa kuanza na Mheshimiwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu, Mkuu wa nchi kisha usomi ...

Read More »

Nane Nane darasa lenye wanafunzi wachache mno

Nimetembelea hivi karibuni maonyesho ya wakulima yaliyoadhimishwa kitaifa Nyakabindi, Simiyu, kilomita 20 kutoka Bariadi. Kwa miaka kadhaa nilidhamiria kuhudhuria maonyesho hayo baada ya kujitumbukiza kwenye kilimo, nikiamini ingekuwa sehemu muhimu ya kujiongezea elimu na maarifa kwenye shughuli ambayo sina uzoefu nayo. Nimetoka huko nikithibitisha tu yale niliyoyatarajia. Mkulima, mfugaji, au mvuvi atajifunza mengi ya manufaa kwa kuhudhuria maonyesho hayo na ...

Read More »

Hasara za kufanya biashara nje ya kampuni

Mfumo wa kufanya biashara wewe kama wewe ni wa zamani mno. Ukisoma hadithi zilizo ndani ya Kurani na Biblia utaona watu wa kale walitumia mfumo huu huu katika biashara zao ambao pia na wao waliukuta. Ni mfumo ambao umezeeka kiuchumi, kisheria na kila nyanja. Baadaye watafiti wa uchumi na sheria wakaja na mfumo wa biashara kutoka mtu binafsi kwenda kampuni. ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (41)

Mazoea ni shati lililotengenezwa kwa chuma   Mazoea ni mtihani. Mwanzoni mazoea ni kama utando wa buibui, baadaye ni kama nyaya ngumu. Mwanzoni mazoea ni kama shati la pamba, baadaye ni kama shati lililotengenezwa kwa chuma. Shati la namna hiyo si rahisi kuchanika. Ukweli huu ulibainishwa na Samuel Johnson. Kwa maneno mengine: “Minyororo ya mazoea ni hafifu kuweza kuhiisi mpaka ...

Read More »

Shukrani kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Magufuli (1)

Sasa tusaidie wastaafu tunaoambulia Sh laki moja kwa mwezi   Agosti 3, 2019, mimi mkongwe mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) nilibahatika kutokea kwenye vyombo vya habari bila ya kutarajia hata kidogo. Nadhani wengi waliona kupitia runinga nikiwa Mtaa wa Kilongawima, Jangwani Beach. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alinishangaza aliponiambia umetimiza miaka 89 ya ...

Read More »

Tuwe waungwana baada ya kutimiza wajibu

Binadamu anakula matunda mbalimbali katika mzunguko wa majira ya mwaka, yakiwa ni chakula, kinywaji na tiba katika mwili wake. Baadhi ya matunda hayo ni boga, tikiti na mung’unye. Watanzania wanakula sana matunda haya kujenga siha ya miili yao. Zaidi ya kuwa ni chakula, kinywaji na tiba, wanatumia asili (maumbile) ya hali ya matunda haya kama vielelezo vya mafunzo ya tabia ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (10)

Wiki iliyopita katika sehemu ya 9 hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Maskini weee! Nilitaka niondoke haraka, kujaribu kufungua mlango haukufunguka, nikajisogeza pembeni mbali kidogo na kile kitanda. Ghafla nikasikia sauti nyororo masikioni mwangu, ilikuwa sauti ya mrembo na hata wewe rafiki yangu Bulongo ungeisikia bila shaka ungeitamani uisikilize. Moyo wangu ukajaa shauku ya kutaka kumuona mtoa sauti hiyo. Ile sauti ikaendelea: ...

Read More »

Chaka Chaka Mwanamuziki shupavu

Yvonne Chaka Chaka, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mjasiriamali, mtetezi wa haki za wanyonge na mwalimu wa wengi nchini Afrika Kusini, jina lake limeorodheshwa kwenye orodha ya wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa Afrika. Jarida la Avance Media la Marekani ambalo hujishughulisha kutafiti na kuchapisha majina ya watu maarufu wenye ushawishi kila mwaka limeweka jina lake katika orodha hiyo. Jarida hilo katika ...

Read More »

Tutatoboa tukiwathamini hawa!

AZAM, KMC, Simba na Yanga zote zimeanza safari ya ‘kuifuta machozi’ Tanzania Bara katika michuano ya klabu barani Afrika. Matokeo ya mechi zilizochezwa mwishoni mwa wiki kila mtu anajua. Lakini wakati tunataka timu hizo zipate mafanikio makubwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, kuna mahali tunajisahau. Tunataka mafanikio, lakini tunasahau kusaka watoto wenye vipaji huko ...

Read More »

Waomboleza

Familia ya Naomi Marijani (36), imefanya maombolezo kwa ibada maalumu baada ya kuthibitika kuwa binti yao ameuawa. Ingawa haijathibitika nani kamuua (kwani kesi ndiyo imeanza), pamoja na mume wake kukiri mbele ya polisi kuwa alimuua na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa nyumbani kwake Gezaulole, Kigamboni, Dar es Salaam na kisha kuzika mabaki shambani kwake Kijiji cha Marogoro, ...

Read More »

Usalama kazini tatizo Kiwanda cha Saruji Nyati

Mfanyakazi wa Kiwanda cha Saruji cha Nyati, Charles Reuben, amekufa akiwa kazini huku chanzo cha kifo kikidaiwa ni kufunikwa na kifusi cha makaa ya mawe. Reuben amekutwa na mauti hayo usiku wa kuamkia Julai 28, 2019 baada ya kuteleza na kutumbukia kwenye eneo linalopokea makaa hayo (coal mill) kwa ajili ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme na mitambo ya kuunguzia ...

Read More »

Malaria tishio Ukerewe

Maambukizi ya ugonjwa wa malaria katika Mkoa wa Mwanza yanazidi kuiweka jamii ya mkoa huo hatarini. Kwa sasa Mkoa wa Mwanza una kiwango cha asilimia nane ya maambukizi ya ugonjwa huo ikiwa ni juu ya kile cha taifa ambacho ni asilimia saba. Ugonjwa huo unaosababisha vifo vya mamilioni ya watu ulimwenguni ni dhoruba inayoiandama dunia licha ya kuwapo kampeni ya ...

Read More »

Tukipeleke Kiswahili SADC

Watanzania tumejiandaa kupokea ugeni mkubwa kwa wakati mmoja, kuanzia wiki ya kwanza ya Agosti hadi ile wiki ya tatu. Macho ya dunia yatakuwa Tanzania kufuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Wakati wageni wanaanza kuingia nchini kwa ajili ya vikao vya awali vya wataalamu pamoja na kikao cha makatibu wakuu, kabla ya kile ...

Read More »

NINA NDOTO (29)

Kufanana ndoto si kufana matendo   Watu wawili kuwa na ndoto moja haimaanishi kuwa kila watakachofanya kitafanana. Kuna aliyewahi kuimba akisema, “Hata vidole havilingani”. Vyote ni vidole, lakini vinatofautiana kwa urefu. Hata watu ambao tunawaita mapacha wanaofanana bado kuna vitu wanatofautiana. Ndoto yaweza kufanana na ya mtu mwingine, lakini mwishowe wakafanya mambo tofauti na pia wakawa na matokeo tofauti. Wakati ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons