Author Archives: Jamhuri

KLABU YA SIMBA YASITISHA RASMI MKATABA NA KOCHA WAKE MSAIDIZI

Uongozi wa Klabu umeuvunja rasmi mkataba na kocha wake msaidizi Irambona Masoud Djuma kuanzia leo Oktoba 8, 2018 Taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo imesema uamuzi huo umekuja baada ya mazungumzo kwa pande zote mbili hivyo ni kwa faida ya klabu na kwa maslahi ya pande zote Aidha, Djuma amesema kuwa hakutegemea kama siku moja angefika Simba SC, anashukuru sana ...

Read More »

Mifugo yatajwa kuwa ni changamoto ya maendeleo ya barabara Mkoani Rukwa

Meneja wa Wakala wa barabara (TANROAD) Mkoa wa Rukwa Mhandisi Msuka Mkina ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazorudisha nyuma ujenzi na matengenezo ya bararabara za mkoani humo ni uwepo wa shughuli za kibinadamu kando ya barabara hizo. Amesema kuwa uswagaji wa mifugo barabarani husababisha uharibifu mkubwa katika muda mfupi jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za serikali katika kuhakikisha inafikisha miundombinu ...

Read More »

TAKUKURU JIRIDHISHENI NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA KWA WANANCHI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa TAKUKURU wajiridhishe huduma zinatolewa kwa wananchi bila ya rushwa, watakapobaini rushwa wachukue hatua.   Pia, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wajiepushe na vitendo vya rushwa pamoja na matumizi mabaya ya fedha za Serikali katika utendajikazi wao.   Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 8, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo ...

Read More »

MHASIBU WA MAPORI AREJESHWE KWENYE NAFASI YAKE-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa Mapori ya akiba ya Buligi, Biharamulo na Kimisi Bw. Bigilamungu Kagoma amrudishe Mhasibu wa mapori hayo Bw. Adam Kajembe katika nafasi yake.   Ametoa agizo hilo baada ya Meneja wa Mapori hayo Bw. Kagoma kumuondoa mhasibu huyo  na kumteua Bibi Ruth Philemon ambaye ni Mhifadhi wa Wanyamapori kuwa mhasibu wa mapori hayo.   Ameyasema hayo leo ...

Read More »

Basi la Arusha Express, Laua Wanne , na Kujeruhi 11

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa ambapo watano kati yao hali zao ni mbaya baada ya kutokea ajali ya basi la Kampuni ya Arusha Express lenye namba za usajili T 750 BYQ katika eneo la Bonga, Babati mkoani Manyara leo Jumatatu, Oktoba 8, 2018. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Augustino Senga amesema basi hilo la kampuni ya ...

Read More »

Humphrey Polepole Atoa limiti ya Wabunge Wanaotaka Kuhamia CCM

  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema wabunge wa upinzani wanaotaka kujiunga na chama hicho mwisho wa kufanya hivyo ni Disemba, 2018.   Polepole ametoa kauli hiyo jana Jumapili Oktoba 7, 2018 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter ambapo amesema mwaka 2018 ndio mwisho wa chaguzi ndogo za ubunge, wale ...

Read More »

Kwako Waziri wa Mambo ya Ndani

Mheshimiwa Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, sisi askari wastaafu wa Jeshi la Polisi tunakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya ingawa kuna changamoto za hapa na pale. Tunakutia moyo na tunaomba Mungu akuzidishie hekima katika utendaji wako. Ndugu Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni kubwa. Inaundwa na Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la ...

Read More »

Mtoto wa rais akamatwa na mali za bilioni 36

Sao Paulo, Brazil Vyombo vya usalama nchini Brazil vimekamata fedha taslimu na mali za kifahari za mtoto wa Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema, vyote vikiwa na thamani ya dola milioni 16 (Sh bilioni 36). Miongoni mwa vito vya thamani vilivyokamatwa ni saa zilizokuwa kwenye mabegi ya msafara wa mtoto huyo. Teodoro Obiang, ambaye ni Makamu wa Rais wa ...

Read More »

Uamuzi wa Canada dhidi ya Kyi ni sahihi

Kama hujamsikia Aung San Suu Kyi, fungua macho upate somo la unafiki mkubwa unaotawala ulimwengu wetu enzi hizi. Su Kyi ni kiongozi wa Myanmar mwenye wadhifa unaofanana na wa waziri mkuu ambaye ni maarufu kama mwanaharakati aliyepinga utawala wa kijeshi wa nchi yake kwa miongo kadhaa na kusababisha kutumikia kifungo cha nyumbani kwa karibia miaka 20 hadi kufikia mwaka 2010. ...

Read More »

Korosho bado ni ‘umiza kichwa’! (3)

Wakati wakulima wa korosho wanaanza kufaidi – (kwa Kimwela ‘kupoka’) neema za korosho, mara mwaka ule wa 1973 serikali ikavunja ile bodi ya mazao, lakini ikaunda mamlaka maalumu kwa zao letu la korosho. Mamlaka hiyo ilijulikana kama CATA (Cashew Authority of Tanzania). Majukumu ya mamlaka hii yalikuwa kuweka bei za korosho, kununua na kuuza korosho. CATA ilishughulikia kikamilifu zao la ...

Read More »

TFF inazibeba Simba, Yanga

Mfumo wa sasa wa ufadhili wa ligi hauna tija kwa taifa, kwani tunaendelea kuzifadhili Simba na Yanga ambazo kitaifa hazina uwezo, wameshuka kisoka ndiyo maana hawashindi. Turudishe mfumo wa Sunlight au Taifa Cup kupata wachezaji wazalendo kutoka vijijini na wilayani. Msomaji wa JAMHURI, Pangani, 0716612960 Lindi hatuna DC Kutokuwa na mkuu wa wilaya Lindi Vijijini kunawanyima uhuru wananchi kuamua mambo ...

Read More »

Wanafunzi 12 watiwa mimba

MWANZA NA MWANDISHI WETU Wanafunzi 12 wa Shule ya Sekondari ya Igokelo, Misungwi, mkoani Mwanza wametiwa mimba ndani ya kipindi cha miezi minane ya mwaka huu. Wanafunzi hao ambao wako chini ya miaka 18 wameacha masomo. Pamoja nao, wanafunzi wengine wameacha masomo baada ya kuolewa. Januari hadi Juni, mwaka huu wanafunzi watano walibainika kuwa na ujauzito na wengine saba walibainika ...

Read More »

Nukuu: Tusivunje mlango

Nyerere: Tusivunje mlango “Ikiwa mlango umefungwa, basi yafanywe majaribio ya kuufungua; umeegeshwa, (basi) usukumwe hadi ufunguke. Katika hali yoyote, gharama ya waliyomo ndani.” Haya ni maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoyatoa Toronto, Canada, Oktoba 2, mwaka 1969. Obama: Bajeti si namba “Bajeti ni zaidi ya orodha ya namba kwenye ukurusa; ni umwilisho w Haya ni maneno ya Rais wa ...

Read More »

Jamani, walimu wanateseka!

Mwaka jana niliwaalika baadhi ya walimu wangu wapendwa walionifundisha shule ya msingi. Miongoni mwao alikuwamo aliyenifundisha darasa la kwanza. Sina maneno mazuri ya kueleza furaha niliyokuwa nayo, na zaidi ya yote, waliyokuwa nayo walimu wangu. Pamoja nao, niliwaita baadhi ya wanafunzi wenzangu tuliosoma pamoja. Lilikuwa tukio lililotutoa machozi ya furaha baadhi yetu tuliofundishwa na walimu hao miaka mingi iliyopita. Nilifanya ...

Read More »

‘Mwizi’ wa magari Moshi apelekwa Kenya

Na Charles Ndagulla, Moshi Mfanyabiashara Bosco Kyara na mwenzake Gabriel Mombuli, wanaotuhumiwa kujihusisha na mtandao wa wizi wa magari katika nchi za Kenya na Tanzania wamesafirishwa kwenda nchini Kenya kujibu mashtaka ya wizi wa gari. Kyara ni mkazi wa Makuyuni katika Mji Mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi Vijijini, wakati Mombuli ambaye anafanya shughuli za udereva, anaishi eneo la Majengo ...

Read More »

Hukumu kesi ya MV Bukoba na mafunzo kwetu leo tunapoombolez

Na Bashir Yakub (A) NAMBA YA KESI Kesi ya Jinai Na. 22/1998, Mahakama Kuu Mwanza, mbele ya Jaji (B) WASHTAKIWA 1. Kapteni Jumanne Rume Mwiru. Huyu ndiye alikuwa akiendesha kutoka Bukoba kupitia Kemondo Bay hadi Mwanza. 2. Gilbert Mokiwa. Huyu alikuwa mkaguzi wa meli, na ndiye kuikagua MV Bukoba. 3. Alphonce Sambo. Huyu alikuwa Ofisa wa Bandari ya Bukob safari ...

Read More »

Hati za makazi ‘kasheshe’ Temeke

Na Alex Kazenga, Dar es Salaam Maofisa Ardhi wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wanatuhumiwa na wananchi wa Kata ya Yombo – Makangarawe kwa kuendesha zoezi la utoaji wa hati za viwanja kwa njia za rushwa. Tuhuma hizo zinatokana na ofisi hiyo kudaiwa kuwatoza wananchi Sh 50,000 za kufuta hati za makazi bila kuwapa risiti wanapofika ofisini kufuatilia ...

Read More »

Wizi wa kutisha

Mtandao wa utapeli unaowahusisha wafanyabiashara na watendaji wakuu wa baadhi ya taasisi za serikali umebainika kuwapo kwenye biashara ya usafirishaji wa magari nje ya nchi (IT). Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI kwa miezi mitatu umebaini mtandao huo unaowahusisha baadhi ya watendaji waandamizi katika Bandari ya Dar es Salaam, Wakala wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na kampuni za bima. ...

Read More »

Waandishi wa habari washinda kesi

MWANZA NA MWANDISHI WETU   Mahakama ya Mkoa wa Mwanza imetupilia mbali kesi dhidi ya waandishi wa habari, Christopher Gamaina (Gazeti la Raia Mwema) na George Ramadhani (kujitegemea) waliotuhumiwa kujifanya maofisa wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Nchi za Ukanda wa Joto (TPRI). Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Bahati Chitepo, amewaachia huru wanahabari hao mwishoni mwa wiki iliyopita, akisema ...

Read More »

Asante Mahakama Mkoa wa Mwanza

Miongoni mwa habari tulizozipa kipaumbele kwenye toleo hili ni ile inayohusu uamuzi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza kutupilia mbali kesi dhidi ya waandishi wa habari wawili waliobambikiwa kesi. Waandishi hao walishitakiwa kwa kile kinachodaiwa kwamba walijifanya ni maofisa wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Nchi za Ukanda wa Joto (TPRI). Hakimu Bahati Chitepo amesema mamlaka zinazohusika, yaani TPRI ...

Read More »

Vyombo vya habari ni chuo cha maarifa

Vyombo vya habari (mass media) ni njia ya mawasiliano kati ya mtu na mtu, katika kuhabarishana, kuelimishana na kuburudishana. Iwe wakati wa kazi, mapumziko au starehe. Ni njia ya kufikia kupata maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika taifa lolote duniani. Kila chombo (medium) kinafanya kazi kwa maadili ya kazi, kanuni na weledi. Kushirikiana na kingine katika kupokea na kutoa taarifa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons