MAISHA NI MTIHANI (3)
Majaribu ni mtihani. Kumbuka kuwa bahari shwari haitoi wanamaji stadi. Watu wema wamefinyangwa na mitihani ya maisha yenye sura mbaya. Nakubaliana na Matshona aliyesema: “Roho zenye urembo zinafinyangwa na mapito yenye sura mbaya.” Wakati mwingine tunawajua watu wenye majina makubwa lakini hatujui majaribu makubwa waliyoyapitia. Tunajua umaarufu wao, hatujui hadithi zilizojaa huzuni za maisha magumu…