Simba jana kwenye uwanja Taifa wamechezewa sharubu zao baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 na Stand United Chama la wana, mechi hiyo ilikuwa kali sana ambapo ilikuwa funga nikufunge, simba wakishinda stand wanachomoa. hivyo mpaka dakika 90 Simba 3 – Stand United 3.
Mzunguko wa 20 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara unaendelea tena leo Jumamosi Machi 3, 2018 kwa kuchezwa mechi nne.
Njombe Mji watakuwa nyumbani Uwanja wa Sabasaba kucheza na Ruvu Shooting mchezo utakaochezwa saa 8 mchana, wakati Kagera Sugar wao watakuwa nyumbani Uwanja wa Kaitaba kuwakaribisha Majimaji ya Songea mchezo utakaochezwa saa 10 jioni.
Mechi nyingine Tanzania Prisons ya Mbeya watakuwa nyumbani Uwanja wa Sokoine kucheza dhidi ya Mbao FC ya Mwanza saa 10 jioni, Azam FC watakuwa Azam Complex ikiwakaribisha Singida United saa 1 jioni.

By Jamhuri